Natafuta msichana wa kuoa ili niachane na maisha ya ukapera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta msichana wa kuoa ili niachane na maisha ya ukapera

Discussion in 'Love Connect' started by Ngoswe11, Jan 3, 2011.

 1. N

  Ngoswe11 Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wapendwa wadada wa JF,

  Kwa heshima na taadhima naomba kuwafahamisha kuwa mimi natafuta msichana ambaye na yeye anatafuta mwanaume ili kuweza kufunga ndoa na kuachana na maisha ya Ukapera. Kumpata mwenza wa kuishi nae ni jambo gumu sana lakini yote huongozwa na mungu. Nimeona nijitokeze hapa JF huenda mungu akanisaidia kumpata mwanamke ambaye huenda mungu akatujalia na kuwa mwili mmoja na hatimaye kujenga familia yenye furaha, amani na upendo.

  Mimi nina miaka 32, sijawahi oa coz muda mwingi nilikuwa nahangaika na maisha pamoja na kujipatia elimu ambayo ni msingi bora katika dunia ya leo. Nina elimu ya juu ya chuo kikuu-ndani +nje ya Tanzania, mwajiriwa, dini-mkristo-Rc, kabila -Mtanzania, urefu-168 cm, sio mnene wala sio mwembamba. Natumia kilevi - bia 1 au 2 kupunguza mawazo ya upweke coz am single.

  Sifa za mwanamke: Ningependa nimpate mwanamke mwenye sifa zifuatazo: Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 30. Haijalishi-awe mnene au mwembamba poa tu, awe serious kama kweli ana nia ya kuolewa, elimu aanzie kidato cha NNE(FORM 4) hadi masters degree hakuna shida or Phd if possible, sina ubaguzi wa dini coz linajadilika, na pia sina ubaguzi na ukabila ila ni vema awe tu MTANZANIA. Tabia njema ni silaha hivyo ningefurahi kumpata mwanamke ambaye atajua nafasi yake kama MKE.

  Kama kuna mwanamke/msichana ambaye anadhani tunaweza kumake life pamoja naomba Ani-PM na hata kama unataka tufahamiane zaidi kabla ya kufanya maamuzi yako pia unaweza ukani-PM! AM MORE THAN SERIOUS, NA WANAWAKE/WASICHANA MNAKARIBISHWA! Thanking you in advance!
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ngoswe 11 kwanza nikukaribishe maana inaonekana hii ndio post yako ya kwanza (Hata sebuleni hujafika kupiga hodi kwanza). Anyway, nalipotezea hili maana najua ni mchecheto wa kuchoka ukapera


  Swali langu ni moja tu, unaoa kwa kuwa umechoka maisha ya ukapera au kuna strong reason nyingine? Ku-feel upweke pekee na kuchoka life za ukapera pekee sio kigezo tosha cha kukufanya uamue kuoa. Sense ya responsibility ni jambo la muhimu.
  Wengi waliooa kwa kukimbia ukapera na kukimbia kuosha vyombo, kufua nguo e.t.c wamekuja kuharibu baada ya kupata wenza wao. Je unadhani uko na sense ya responsibility ya kumuaminisha mdada kuwa kweli umejiandaa kuwa responsible?

  Je uko tayari kufulfill responsibility kama mume na pia kama baba (usisahau pia kama mkwe, shemeji e.t.c). Hii ndio determinant nzuri zaidi ambayo wasichana wengi siku hizi wanatafuta kwa mtu anaetaka kuwaoa. Weka wazi hapa ili wenye kutaka hili jue wazi

  All the best na naamini utajipatia kimwana wako waego!!
   
 3. N

  Ngoswe11 Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kiongozi,
  Nakushukuru sana kwa maswali yako hapo juu. Kiukweli sababu sio kuuga ukapera bali kiukweli nimekubali yale yote yanahusiana ma responsibility ya mwanaume katika ndoa mimi nipo tayari kufanya au kuyatekeleza. Ndio maana nilisema mwanamke ambaye atajua wajibu wake kama MKE, coz mimi natambua kama mwanaume responsibility yangu ni ipi huku nikizingatia kuwa mfumo dume kwa maisha ya sasa hauna nafasi sana katika kujenga familia bora. Kifupi naomba utambue kuwa nipo tayari kama mume na nitafanya yale yote ambayo nitatakiwa nifanye kwa mke au jamii ituunganishayo kama wanafamilia/socialization within two families and taking part into it as I can ! Lakini hata umri wangu nao umenisukuma na kutambua kuwa kwa sasa ni vema tukawa wawili ili tuweze saidiana vema kimaisha katika kujenga familia iliyo bora. Asante.
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Naamini wamekusoma vema. Nikutakie kila la kheri.

  Niliuona umri wako lakini kwa wengine huwa si kigezo. Nilikuwa na jamaa mwenye miaka 37 lakini anamambo ya ajabu kwenye ndoa na akashindwa hata na mdogo wako wa miaka 34.

  All in all, may God stretch out his mighty hand and help you get one, your real life time partner, be it from JF, from your neighborhood e.t.c.
   
 5. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mnh bahati ya mtende hii mie ngoja nijitose!!.....................:embarrassed::embarrassed:
   
 6. DJ BABU

  DJ BABU JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 210
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haya masuala ya kuoa oa naona na mimi yananichanganya kichwa yangu sana siku hizi
   
 7. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Pauline mdogo wangu umeshaacha hisia za yale mambo yako yale?? Sikutibulii, nakutibia
   
 8. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  DJ ndo uchungu wa MB Dog kukumegea nini? teheteeehee, bado ni muhimu maana alietuumba aliona si vema tuake peke yetu.
   
 9. DJ BABU

  DJ BABU JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 210
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo siku hizi madem wote wasanii tu aah
   
 10. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ndio namtafuta wa kunisahaulisha.....ila serious yale mambo yana matatizo gani kwani??ikiwa ww ni mume wangu utajuaje kama sitakwambia mimi mwenyewe?
   
 11. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kweli unauchungu mwana, nikiangalia na hilo li signature lako ndo basi tena.

  Jamaa yangu mmoja alikata tamaa akawaza kwenda kuoa kibibi cha mwaka 47 eti walikuwa na maadili sana.

  Ila tulia tu mtu wangu, one day Yes. Wengine tulijeruhiwa sana na mapenzi, almost 2 times lakini mambo yaliponyooka kwangu mimi hakuna kitu kizuri maishani kama kuwa na huyu binti hapa pembeni yangu ninapoandika post hii. Very lovely and very understanind. One day Yes na usikate tamaa DJ
   
 12. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Pauline usifanye mchezo na mautamu. Kwenye kunogewa kuna kujisahau kwa hali ya juu.

  Iko siku utajikuta yamekuzidia alafu jamaa anagundua very late. Huoni msala huo?
   
 13. DJ BABU

  DJ BABU JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 210
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  you are the man! sweetest post ever
   
 14. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Binti ameniambia nikugongee lisenks la kielektronic. Tunakuombea upate wa ukweli ambae hata zinguka kama kuku mwenye kideri
   
 15. DJ BABU

  DJ BABU JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 210
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ahsante sana braza mwambie shem namsabahi
   
 16. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #16
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  mmhhhhh nilikuwa napita tu....

  we DJ Babu wewe im watching u lol......
   
 17. DJ BABU

  DJ BABU JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 210
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  afro mwana wa denzi inakuwaje kimwana?
  saluti kwako kipenzi unavyonicheki mi ma blashing ya kufa mtu huku
  kama vipi halaaa
   
 18. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa yuko serious. wanaokuzdi umri hutaki? maana wengine tuna umri mkubwa na ndoa tunahitaji. Unasemaje kwa hilo?
   
 19. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #19
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  mmhhh DJ umeniangasha sana New year Eve nilikuwa nasubiria single yako
  siku hiyo lakini mmmhh hata hukutoa...
  nway mie mizima kabisa yaani vipi maisha lakini??
  [​IMG]
   
 20. DJ BABU

  DJ BABU JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 210
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  da kumbe nahumu warembo mnakoma na swaga zangu
  kama vipi mi ndo kivile na search search
  maisha mukide si unajua miisho ya mwaka show za kufikia
  new year nlikuwepo na kachaa wangu ngwea shoo la kufariki mtu
  ndo maana kivile nini sijatimba jf
  kumbe ulikuwepo unanideki kiaina ee
  unaweza uka halaaa nini na ma pm mbona shwanga tu
   
Loading...