Natafuta msichana wa kazi mwenye sifa hizi

TensorFlow

JF-Expert Member
Feb 11, 2020
812
969
Sifa ya kwanza ni kuwa natafuta msichana maridadi/ mrembo/ mchangamfu anayeishi Dar ili tuweze kufanya biashara ya kutuma na kupokea fedha - mhusika ataanza kufuatilia michakato yote na kusimika hii biashara kwa usaidizi wangu. Biashara itafanyika katika moja ya suburbs za mji wa Dar.

Awe ni mtu anayependa kujifunza na kufundishika kwa haraka kwa sababu biashara yetu huko mbeleni itahusisha teknolojia. Naorodhesha sifa chache anazotakiwa kuwa nazo, zingine atazisema yeye na kuprove kuwa anazo, jambo ambalo litanishawishi kuwa yeye anafaa:

1. Ajue kuwasiliana vizuri na kwa umaridadi mkubwa
2. Ajue hesabu za kawaida za fedha
3. Sifa zingine utaniambia wewe

Mshahara wako utakua kwa kadri biashara na faida vitakavyokua.

Usije ukiwaza kuniibia, utaishia jela. Kutakuwa na mkataba wa kueleweka, na lazima uwe na wadhamini wanaoeleweka ili ukileta fyokofyoko nalala na wewe na wao mbele.

NB: Kama wewe ni tapeli kaa mbali, vinginevyo utaishia jela bila kufaidika hata kidogo na unachotaka kufanya.

Tuma PM kama una interest na kudhani una sifa sitahiki.

Tafadhali wadau ambao mmewahi kutafuta wafanyakazi humu, tujuzane mambo muhimu ya kuzingatia ili kuepuka au kuzuia masahibu mliyokutana nayo. Nipe tahadhari yoyote bila kumumunya maneno.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom