Natafuta mkopo binafsi jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta mkopo binafsi jamani

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ABEDNEGO, Jan 29, 2010.

 1. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mtumishi wa Wakala wa Serikali,Mshahara wangu kwa mwezi ni 2M ++ Mwajiri hakubaliani na dhana ya kuingia mkataba na Benki ili watumishi tukopeshwe.Sina colletaral zaidi ya mshahara wangu, Nisaidieni ni wapi naweza kukopeshwa(Personal loan) Nikatwe katika mshahara kwa mwezi ?
   
 2. B

  Bweha mweupe Member

  #2
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nenda benk zifuatazo NBC,ACB,au Accesses onana na maafisa mikopo . peleka salary slip yako ya miezi mitatu na barua ya mwajiri wako. watakukopesha hata mara kumi ya mshahara wako kwa sharti kwamba mshahara wako wa mwezi upitie kwao. ni rahisi tu
   
 3. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Si kweli lazima mwajiri asign barua inayoitwa "Letter of undertaking" na kama unavyojua perosal loan ni ani unsecured loan na mabenki mengi yameibiwa sana ikiwemo Barclays na Kenya Commercial recovery yake ni expensive mtu akishaacha kazi utampataje?? Na sisi watZ sijui kwa nini hatupendi kulipa madeni hata baadhi ya lectures/dr.profs unakuta wana default....
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Huyu mwajiri itabidi akusainie fomu ya makubaliano kati yako na Bank ..
  au hapo atakataa pia?
   
 5. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #5
  Feb 1, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hapo ndipo pagumu kwa mwajiri kusaini barua ya dhamana kwa Benki vinginevyo ingekuwa rahisi sana kupata mikopo kutoka NMB,NBC,CRDB,Community Banks nk.
   
 6. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hapo huna ujanja,Inabidi jidhamini mwenyewe au rafiki yakoakudhamini kwa hati ya nyumba ,kiwanja au shamba.
   
 7. I

  Isae Member

  #7
  Feb 1, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kampuni ninayofanya kazi tunachukua mkopo akiba commercial Bank ila LAZIMA mwajiri asaini fomu ya mkopo. ACB wamerahisha hamna cha barua ILA Kampuni iko complicated wanachofanya wanaandika barua kueleza kuwa watapitisha mshahara kwa muda wote wa mkopo na iwapo mfanyakazi atahama au kushindwa kulipa kampuni haihusiki bali mtu mwenyewe, so go to Akiba Commercial Bank for more clarifications
   
 8. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Lazima mwajiri aweke sign kwenye form hata kama anatoa partial guarantee
   
 9. f

  furahaeliud Member

  #9
  Feb 1, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lah pole saana, ni kweli kabisa kama mdau alipochangia yaani kama mwajiri hataki kuwasania mkataba na benki ni problem kabisa unajua tene hizo ni unsecured loans lazima guarantee ya mwajiri ongeeni na mwajiri vizuri na mjue ni kwanini hataki wafanyakazi wake wakope benki maan ndio njia pekee
   
 10. f

  furahaeliud Member

  #10
  Feb 1, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama ndugu au jamaa akikuwekea dhamana ya nyumba na mshahara uupitishie benki husika japo mlolongo wake ni mrefu kidogo inawezekana kupata
   
 11. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Acheni kamba jamani. Mnatoa masharti utafikiri nyie ni ma-benki? Jamaa hata hajasema anataka kukopa kiasi gani? Wacheni roho za korosho, mkuu nenda Benki kama jamaa moja hapo juu alivyosema then angalia masharti yao, vile vile kiasi unachotaka kukopa kitakuwa kigezo kikubwa cha wao kukuambia wanahitaji vitu gani.
   
 12. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Pole, hii na mie ilinitokea mwaka juzi. Bosi alikataa kabisa, badala yake aliona aniongezee mshahara kiasi kilekile ambacho ningekatwa kwa mwezi. Access wanatoa lakini uonyeshe hati ya nyumba, shamba, biashara au mifugo au kadi ya gari afu wanaanzia hela ndogo sana. Wengine Sero ila hizi bank zote zinataka barua na signature. Mi nimejifunza kuweka taratibu.
   
 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
   
 14. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Acha hizo Malila, unajua mara nyingine mtu unaenda kuomba mkopo kwa kitu ambacho unaweza pia kufanya kwa kutumia mapato yako tu ila kwa kuona urahisi unataka hela ya haraka. Sasa mie nilipoulizwa vizuri nilielekezwa bora utumie mshahara. Halafu mleta mada awe open atapata ushauri mzuri, mkopo kiasi gani na unafanyia au kununua nini. Siku hizi kuna bank na hata watu wanakopesha hela kwa watu binafsi. Kuhusu kuwa mwajiriwa wa serilkali sidhani kwani uko mie sijawahi kusikia wanakataliwa signature.
   
 15. M

  Malila JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ok mama Joe,na mimi nitaweka kibubu changu kama wewe ili nikwepe taabu za bank
   
 16. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Poor arguement...hapa uko na watu wengi na wana tumia majina bandia so hujui mtu anaprofessional gani unasema eti nyie ndio Bank? Yaliyosemwa na wadau kuhusu mikopo ya benki yote ni ya kweli na mikopo ya mabenki ya TZ ni migumu sana kwa vile wengi wetu tunaona ufahari kuto kulipa na sio kulipa mikopo. Interest rates zinaanzia 16(tena hapa ni kwa group loans)hadi 30 imagine unajua kiasi gani watu wanaumia?? India highest interst rates za loan ni 7 wakatu kwa TZ hio ni kwa ajili ya Bank staff Loan tena wa benki kama NBC na sio bank zote? upo hapo????

  Ila kuna taasisi ukiwauliza salary slips zao hawazionyeshi kutokana na kazi zao zilivyo so inakuwa ngumu kupata mikopo labda nahisi wanakopeshwa huko serikalini-na sio bank.
   
 17. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  ABEDNEGO has chosen not to receive private messages or may not be allowed to receive private messages. Therefore you may not send your message to him/her.

  If you are trying to send this message to multiple recipients, remove ABEDNEGO from the recipient list and send the message again.


  Sasa mtu akitaka kuwasiliana na wewe kwa PM atumie njia gani??
   
 18. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #18
  Feb 7, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante ndugu yangu Nguli sasa naweza kupatikana ni PM tu
   
 19. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #19
  Feb 7, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  ABEDNEGO amenena....!
  nimepata tabu kweli kukopa kwenye benki zetu....!
  labda uwe INDIAN ndo watakupokea kwa mikono miwili-miwili na utapewa double-share....!
  zunguka na kapu la pesa huku ukiweka na kuzitoa.....wenyewe wanasema unatengeneza BANK STATEMENT nzuri...!
   
 20. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Si kwamba ASIAN wanapendelewa kwenye mikopo la hasha wanalipa mikopo kuliko sisi, tunakasumba ya kutokulipa na ndio maana interest rztes ziko juu kutokana na risk ya ku-recover loans TZ. Tena hii recession ya juzi imezua excusses za kutokulipa acha mchezo.

  Kuhusu kuzunguka na kapu si kweli policy za kuanalise mkopo zinasema kwamba lazima mkopaji/client awe na good conduct of account hii unaweza kujua kwa kuangalia bank statement kutoka Bank yeyote. E.g mtu ana taka 10m ukiangalia turn over yake kwa mwezi ana laki 1 tu. Akipewa mkopo lets say kwa 3 yrs atatakiwa kulipa installment ya TZS 300,000 je hizo laki 2 atazipata wapi na mostly facilities have no grace period?? na atakula nini??expenditures and whatsever??

  Nafikiri ningeshauri elimu ya mikopo ianzishwe kwa uma kwa vile nachoona hapa watu hawana elimu ya mikopo.
   
Loading...