Natafuta mke wa kuoa jamani, namaanisha maana umri unanikimbiza. *nipo serious*

Matokeo1

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
231
42
Wapenzi wa jf mimi ni kijana wa 29yrs ni mhitimu wa chuo kikuu lakini kazi bado, natafuta mchumba wa kuoa namaanisha, awe mkristo, mcha Mungu, ajali familia yetu kama ilivyo yao, awe ametulia sio kiruka njia, kikubwa zaidi awe na shape nzuri maana maishani natamani kua na mkee aliejazia, simaanishi aliejazia sanaaa, sura nzuri sana sijalishi, sibagui elimu wala kabili ila awe na umri kuanzia 20-29, nawasilisha ndugu zangu, mbarikiwe.
 
Kikubwa zaidi awe na shape nzuri maana maishani natamani kua na mkee aliejazia
Utampata tu, shaka ondoa kabisa.
Hii ndio Jf bhana!!!!

ANGALIZO: Yakikukuta yakukukuta usije ukatoa ma-ringtone ya ajabu.
 
Watafuta mke huku Jf???....kisha kazi huna..mbona mashaka sasa...?
 
Watafuta mke huku Jf???....kisha kazi huna..mbona mashaka sasa...?

Kazi kweli bado, ila maisha ya ndoa sio kigezo lazima uwe na kazi tu, maa kwa wale wasio na kazi wasingeoa, enda ikawa kuna source nyingine ya income lakini sio kivileeee.
 
Mmmh.... Kujazia? Ngoja niku pm m4aana nimejazia VIGIMBI!!
 
muulize baba yake dullysykes ana miaka mingapi na hana mpango wa kuoa,age ain't nuthing but a number men,mitaani kote wa kuwaoa hujawaona,umeambiwa jf ni kijiwe cha kutafutia wachumba,heshimuni jukwaa nyie,alaaaah
 
sasa kaka huyo mke utamuweka wapi, utamlisha nini, watoto utawatunzaje? Nijuavyo mimi, kuoa sio suala la umri peke yake, kuna material support kwa familia utakayoanzisha. Na zaidi ya yote, mkeo nae atakuja na matatizo yake na ya kwao. Uki-"confuse" na yako bila kibarua mjini hapa utaishije?

You have to be matured emotionally and financially before starting thinking about marriage. Ni hayo tu
 
Mkuu hapo ushasema baba ake dullysykes inamaana kashaoa au kashazaa na mwanamke sa unataka niwe kama huyo mzee? hatuigaji mabaya ila mazuri ya kumpendezesha Mungu
 
Mbona haujasema unatafuta mke wa shida na raha? Manake tulio wa raha tupu tutajisumbua hapa.

Kweli kama wewe ni mtu wa raha tupu hii haitakuhusu, hongera mama umezaliwa kwenye raha, sisi tumezaliwa kwenye shida nafikiri hapa utajisumbua kweli
 
We umetaja sifa za demu unemtaka mara ajazie, sura nzuri, we mbona cv yako imeishia kwenye umri na kidigrii au ndugu yangu sura yako kama Pinda & Wassira Co. Kama huna kazi dem wa kazi gan، wanawake hawana uhaba wa mwanaume ppumbbu wanataka mwanaume wallet! Bora ungeanzisha thread ya kutafuta kazi kuliko hii ya kutafuta nyuchi shauri yako utaambulia u.chi pori!
 
Mmh! Ina mana shule ya mcngi hukupata,secondary,chuo,kansan,mtaani,ktk jumuiya, barabarani,harusini,beach! Kote huko hujapata tu mke! Mwe! Mwe! Mwe! Mwe! I think utakuwa na tatzo!
 
sasa kaka huyo mke utamuweka wapi, utamlisha nini, watoto utawatunzaje? Nijuavyo mimi, kuoa sio suala la umri peke yake, kuna material support kwa familia utakayoanzisha. Na zaidi ya yote, mkeo nae atakuja na matatizo yake na ya kwao. Uki-"confuse" na yako bila kibarua mjini hapa utaishije?

You have to be matured emotionally and financially before starting thinking about marriage. Ni hayo tu

Umri nao unamatter mkuu hujawahi kusikia umri ukipita sana unaweza zaa watoto wenye upungufu wa akili? pia sitaki kuoa na umri mkubwa sana maana watoto watakosa malezi mazuri si unajua watoto wa kidigitali wakikosa strong person watakuaje? kuhusu financially hiyo sio tatzo kuna source nyingine ya income ila sio kubwa sanaaaaa.
 
Mmh! Ina mana shule ya mcngi hukupata,secondary,chuo,kansan,mtaani,ktk jumuiya, barabarani,harusini,beach! Kote huko hujapata tu mke! Mwe! Mwe! Mwe! Mwe! I think utakuwa na tatzo!

Huko kote muda ulikua hujafika ila naona muda umewadia kwa sasa mpendwa
 
We umetaja sifa za demu unemtaka mara ajazie, sura nzuri, we mbona cv yako imeishia kwenye umri na kidigrii au ndugu yangu sura yako kama Pinda & Wassira Co. Kama huna kazi dem wa kazi gan، wanawake hawana uhaba wa mwanaume ppumbbu wanataka mwanaume wallet! Bora ungeanzisha thread ya kutafuta kazi kuliko hii ya kutafuta nyuchi shauri yako utaambulia u.chi pori!
Mbona unaniogopesha tena mkuu, kuhusu kazi haijalishi maana kama kipato ninacho tena fresh tu, kusema sina kazi haimaanishi sina pesa namaanisha mi sio mwajiriwa.
 
Mbona unaniogopesha tena mkuu, kuhusu kazi haijalishi maana kama kipato ninacho tena fresh tu, kusema sina kazi haimaanishi sina pesa namaanisha mi sio mwajiriwa.
Hata mimi nilikua na mashaka nikafikiri huna kipato kabisa . Hapo sasa umefunguka vizuri, kumbe una vyanzo vingine vya mapato . Uwe mvumilivu tu mwaego utampata ua la moyo wako kua mpole tu. Si unajua mvumilivu hula mbivu lkn uwe mwangalifu usije ukala zilizooza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom