Natafuta mdhamini wa kunipatia bajaji kwa makubaliano ya kumletea kiasi kadhaa kila siku Mbeya Mjini

David Kilas

Member
Nov 29, 2020
14
15
Habari.Mimi naitwa David Benjamin.

NI muhitimu wa chuo kikuu IFM kilichopo Dar as salaam ambapo nilipata degree ya Social protection and Actuarial studies.

Toka nimehitimu nimekua nikitafuta ajira bila mafanikio yoyote mpaka sasa licha ya kuwa na matokeo mazuri katika masomo. Nilifanikiwa kuanzisha biashara ya mgahawa dar eneo la mawasiliano nikishirikiana na rafiki yangu lakin biashara haikwenda vizuri na hatimaye ikashindwa kuendelea..

Kutokana na changamoto hizo sikuweza kumudu gharama za maisha dar hivyo ikabibid nihamie Mbeya ambapo nilifikia kwa wajomba zangu..Nimeendelea kutuma CV na applications katika mashirika mbalimbali lakin so far no success yet..

Maisha yanahitaji kuendelea hata kama sijapata ajira..Nahitaji kumsaidia mama angu na kumsupport mwanangu mdogo hivyo nilianza kuangalia baadhi ya fursa hapa Mbeya na kuona fursa ya usafirishaji kwa kutumia bajaji itanifaa hivyo nilianza kujifunza na hatimaye nikawa napewa day worker baadhi ya Siku hivyo kwa sasa naomba mdhamini wa kuninulia bajaji ili niweze Fanya kazi kila siku na ntakua namletea fedha tutakayokubaliana kwa uaminifu Mkubwa sana. Namba zangu 0766542373/0783367426
 

Attachments

  • DAVID BENJAMIN KILAS.docx
    17.8 KB · Views: 9
  • DAVID BENJAMIN KILAS.docx
    17.8 KB · Views: 3
  • DAVID B. KILASI.docx
    97.5 KB · Views: 4

Similar Discussions

Back
Top Bottom