natafuta mbwa walinzi

drphone

JF-Expert Member
Sep 29, 2009
3,542
281
wakuu heshima mbele ninatafuta mbwa 2 wakufuga wale wanaosemaga wa police wenye mafunzo ya kupambana na wahalifu najua hapa jamvini akikosekani kitu pls wenye kujua haya tujuzane
 
Mkuu unahitaji mbwa mwenye umri gani mkuu?manake kwa breed unayohitaji kwa mbwa mwenye miezi miwili ni Tshs laki 3,pia mafunzo mbwa anapewa akiwa na umri wa miezi kuanzia mitano,kwa mbwa ambaye tayari ana mafunzo hapo si chini ya 1mil.kwa mbwa mmoja.so weka vigezo vya mbwa unayetaka ili nikueleze pa kumpata.
 
Parachichi bana......we drphone nenda poshti huwa nasikia wanauzaga wu wu wu zao au kama vipi tafuta wu wu unayoiona iko fiti uwapelekee poshti wanaweza kukufunzia makarate na makungfu.....hata kutegua mabomu wanafundishwa
 
mtoto wako wa kike kavunja ungo nini?
 
Mkuu unahitaji mbwa mwenye umri gani mkuu?manake kwa breed unayohitaji kwa mbwa mwenye miezi miwili ni Tshs laki 3,pia mafunzo mbwa anapewa akiwa na umri wa miezi kuanzia mitano,kwa mbwa ambaye tayari ana mafunzo hapo si chini ya 1mil.kwa mbwa mmoja.so weka vigezo vya mbwa unayetaka ili nikueleze pa kumpata.

mkuu sina uzoefu wowote juu ya jambo hili ningefurai zaidi endapo ungenisaidia maushauri 1m ni nyingi
 
Parachichi bana......we drphone nenda poshti huwa nasikia wanauzaga wu wu wu zao au kama vipi tafuta wu wu unayoiona iko fiti uwapelekee poshti wanaweza kukufunzia makarate na makungfu.....hata kutegua mabomu wanafundishwa

nimeona wale wanauza barabarani jirani yangu akanitisha kwamba alinunuaga alipokuwa kumbe mbwa mwitu kwa police ni sehemu gani niwafatilie binamu
 
Nenda kwenye malango ya Supermarkets kuwa utakuta matangazo...wanauzwa for $500...hapa shoppers wapo wa3
 
Pia ukienda pale Vet Dispensary ya Morroco wanakuwaga na matangazo ya mbwa on sale. unaweza pata au kama uko serious unaacha namba akitokea mtu anauza wanakushtua. Pole kwa uwizi na vibaka
 
wakuu heshima mbele ninatafuta mbwa 2 wakufuga wale wanaosemaga wa police wenye mafunzo ya kupambana na wahalifu najua hapa jamvini akikosekani kitu pls wenye kujua haya tujuzane

dr phone ndg yangu mbwa bei ghali sana ila kwa vile wewe ni ndg yangu tuwasiliane privately nikupatie kamoja mchanganyiko wa German shepherd na Bull dog ila ujiandae kwa chakula huu mkorogo maalumu unakula chakula sana na sio makombo inabidi uwape super dog na matibabu mara kwa mara.
 
Jaribu pale Kituo cha basi cha Victoria kama unakwenda mwenge.Pale utawapata na bei yake ni poa.
pita pale wakati wa saa kumi jioni na kuendelea
 
Dr Pole kwa vibaka. Mbwa kwa sasa ni ghali sana. Wa miezi 2 wanafikia kama laki 3 hivi. Wakizidi hapo wanafika mpaka 6 hadi 7. Kwa sasa mbwa waliofundishwa hufika hata 1m kama member 1 alivyosema. Ukinunua hawa wa miezi 2 unawakuza wakifikia kufundishwa unamtafuta mwalimu anafundisha kwa mwezi 1 ni 120,000. Mwezi mmoja unatosha kabisa kama mwalimu ni mzuri.

Huku Moshi wanapatikana ila lazima uwe mwangalifu sana kuchagua.

Mimi kwa sasa ninao wale pet dog (wa urembo). Pure white bolognise. Wana miezi miwili kwa sasa and very active. Kwa wanaohitaji wani PM
 
Nina jike la hiyo Bolognise nahitaji mpandaji
 
ninayo mchanganyiko wa giant schnauzer na German shepherd . ila bei ni kubwa kama una $ 1000 kwa pupies tafadhali ni pm. hii mbegu ni balaa .ukicheza wanakutafuna hata wewe .
 
Mkuu ukitaka kupata mbwa mzuri usikubali kununua mbwa bila kuwaona wazazi wa hao mbwa wenyewe!mimi kuna kijana aliniingiza mjini kaniuzia mbwa wa Iringa sijui kama unawafahamu!wana manyoya mengi!!!!kanidanganya ni wa kipolisi na mimi kwa kuwa nilikua na shida ya mbwa na pia siwafahamu nikapigwa changa la macho laki 2 mbwa wawili!yanh mbwa hawabweki wala nini!jamaa nikimuuliza anasema bado wadogo!sasa nikawa nashangaa mbwa wanabweka wakiwa na umri gani?

Nikaja kwenda kwa jamaa yangu yeye anao pure Germany Sherpherd akaniambaioa hao wa kwako sio , akanigizia nikaenda kununua wawili walikua na umri wa mwezi mmoja kila mbwa mmoja nilinunua kwa laki 2!walikua wadogo sana kiasi kwamba niliwawekea bill ya maziwa kwani walikua hawawez kula!ila kwa sasa wana mwaka mmoja yanh huamini!ni wakali vibaya mno!

Sasa cha kushangaza mbwa ana mwez mmoja anabweka wakat nilikua na hao wa Iringa walikua na miezi karibia mitano no kubweka wala nini.

Nime ku PM chek msg yako mkuu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom