Natafuta matokeo ya uchunguzi wa majengo yalioanguka Dar ws salaam hasa lile la mjini kwa lengo la kujifunza

Silicon Valley

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
1,048
2,000
Kwa nia njema ya kujifunza, na kama ijulikanavyo likitokea kosa au tatizo kwenye jamii ni vema uchunguzi kufanyika ili kubaini chanzo cha tatizo kwa lengo la kuepuka lisijitokeze tena.

Kwa upande wa majengo magorofa hapo nyuma kidogo yalianguka mengi kiasi hata kwa wenzetu kenya na kusababisha vifo.Naomba kujua ni wapi nitapata matokeo ya hizo uchunguzi?
 
kunguni wa ulaya

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
4,125
2,000
NATAFUTA MATOKEO YA UCHUNGUZI WA MAJENGO YALIOANGUKA DAR ES SALAAM HASA LILE LA MJINI KWA LENGO LA KUJIFUNZAKwa nia njema ya kujifunza, na kama ijulikanavyo likitokea kosa au tatizo kwenye jamii ni vema uchunguzi kufanyika ili kubaini chanzo cha tatizo kwa lengo la kuepuka lisijitokeze tena

Kwa upande wa majengo magorofa hapo nyuma kdg yalianguka mengi kiasi hata kwa wenzetu kenya na kusababisha vifoNaomba kujua ni wapi nitapata matokeo ya hizo uchunguzi ?
Ripoti zote zinakaliwa na aluyeunda tume.
Kwahiyo usitegemee kuiona in public maana itaumbua watu.
 
Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
5,023
2,000
Mimi naitafuta ile report ya ajali iliyouwa wafanyakazi wa Azam Media.
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
42,590
2,000
NATAFUTA MATOKEO YA UCHUNGUZI WA MAJENGO YALIOANGUKA DAR ES SALAAM HASA LILE LA MJINI KWA LENGO LA KUJIFUNZAKwa nia njema ya kujifunza, na kama ijulikanavyo likitokea kosa au tatizo kwenye jamii ni vema uchunguzi kufanyika ili kubaini chanzo cha tatizo kwa lengo la kuepuka lisijitokeze tena

Kwa upande wa majengo magorofa hapo nyuma kdg yalianguka mengi kiasi hata kwa wenzetu kenya na kusababisha vifoNaomba kujua ni wapi nitapata matokeo ya hizo uchunguzi ?
Taarifa ya awali kwamba:-

1.Nondo na ratio waliyotumia ni JAHU,hauwezi kutumia nondo za mm 10 kujenga column za kubeba ghorofa 16.
2.Ratio ilikuwa mbovu mchanga ulikuwa mwingi sana.
3.Walikuwa wanajenga kwa bandika bandua,wanapiga slab leo baada ya siku 3 au nne wanatoa marine na mirunda wanaenda floor nyingine badala ya kusubiri mwezi/siku21 za kumwagilia jamvi,
 
Silicon Valley

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
1,048
2,000
Taarifa ya awali kwamba:-

1.Nondo na ratio waliyotumia ni JAHU,hauwezi kutumia nondo za mm 10 kujenga column za kubeba ghorofa 16.
2.Ratio ilikuwa mbovu mchanga ulikuwa mwingi sana.
3.Walikuwa wanajenga kwa bandika bandua,wanapiga slab leo baada ya siku 3 au nne wanatoa marine na mirunda wanaenda floor nyingine badala ya kusubiri mwezi/siku21 za kumwagilia jamvi,
Shukran sana mkuu, je hakuna mahala popote walipoweka au pa kupata hayo matokea kwa upana ?
 
munkango

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
353
1,000
Nakumbuka Kuna majengo matatu yamewahi kuanguka. Kuna Chang'ombe Village Hotel, Kuna jingine lilikuwa jirani na CBE na lile la mtaa wa Indira Ghandhi jirani na Msilikiti.

Kila ajali ilipotokea ziliundwa tume na watu kufunguliwa mashtaka lakini sijawahi kusikia watu wamehukumiwa kutokana na kesi hizo.

Tatizo ninaloliona Ni kwamba bado haijulikani ni Mamlaka gani inashughulikia maswala ya ajali za ujenzi. Je Ni OSHA, CRB, ERB, Au Manispaa iliyotoa kibali Cha ujenzi?.

Pamoja na kuwa kuna ajali zimetokea matokeo yake bado hayajaweza kutolewa na kuwa chanzo cha kujifunza na kuepuka kurudia makosa yaliyosababishwa na ajali hizo.

Kwa kuwa umeamua kutafuta taarifa bila shaka utatuletea mrejesho. Nafikiri sehemu ya kuanzia ni Manispaa huko unaweza kupata mwelekeo wa wapi utapata ripoti kamili.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom