Namna ya Kuanzisha na Kuendesha Biashara ya Kufua Nguo | Laundromat Business

carmel

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,837
262
Wash.jpg

Tafadhali wana jamvi, nauliza kuhusu biashara ya dry cleaning, yani kwa mtu mwenye mtaji basic tu wa kuanzia, ina weza kucost shilingi ngapi? Na pia inalipa? Tfadhali, naombeni mawazo yenu maana sina idea yoyote kabisa.

Thanks

WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUELEWA BIASHARA HII
Wakuu, nataka kufanya biashara ya dry cleaning. Naomba kujua kwa mjuvi wa biashara hii anisaidie kunipa taarifa ni vitu gani nahitaji ili niweze anza.

Msaada wenu unahitajika great thinkers
OTIS
The Illuminati
Hello wadau!

Nataka kuanzisha biashara ya dry cleaning somewhere in this country lkn nataka kuanza kwa small scale ili kutest biashara!nataka kujua mtaji kiasi gani ambao unaweza kuhitajika kwenye hiyo bussiness pia ni machine gani ambazo natakiwa kuwa nazo!na hz machine zinaweza kucost sh ngapi na zinapatikana nchini au mpk niagize na km kuagiza wakina nani ni reliable suppliers.
Natazamia kufungua biashara ya kufua nguo kwa hiyo nahitaji mashine kwa kazi hiyo. Tafadhali naomba mwenye kujua bei zake na mahali kwa kuzipata anipe taarifa.

Mashine ni kama zifuatazo

1. Dry cleaning machine (16kg)
2. Packaging Machine
3. Ironing table - aspiration with boiler, height adjustable
4. Stain removing machine
5. Industrial washing machine (16kg) - for blankets etc
6. Wringer (8kg)
7. Domestic washing machine
8. Semi-silent compressor

Natanguliza shukrani
Habari wakuu,

Nataka kuanzisha biashara yakufua nguo kwa mashine (dry cleaner) Naomba mwenye uzoefu wa hii biashara anipe maufundi kidogo yavitu kama, mtaji, faida naipaje pamoja na changamoto zake.

Shukrani.

MICHANGO NA USHAURI WA BAADHI YA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
UKWELI KUHUSU BIASHARA HII

Assumption - Unaangalia uwezekano wa kuanzisha hiyo biashara Dar.

Kulipa kwake kutategemea na nguvu za kiasi gani utawekeza kwenye kuiba wateja wa drycleaning ambazo tayari zina majina. Kuna mlolongo wa drycleaning stores jijini ambazo zimeshakamata sehemu na wateja muhimu wa hiyo huduma.

Hii biashara ni moja ya biashara ambayo soko la ukua polepole sana. Hii ina maana kiwango cha namba ya wateja wapya kujiingiza kwenye uhitaji wa huduma hii ni ndogo sana. Hii inatokana na kuwa, huduma hii bado inaangaliwa kama huduma ya 'anasa' kwa asilimia kubwa ya watu. Kwa hiyo, utakuta asilimia kubwa ya wateja ni hao hao miaka nenda miaka rudi.

Hivyo basi, ili uweze kufanikiwa, itakubidi usuke mbinu za kuwaiba wateja wa drycleaning zingine. Kitu ambacho kinaweza kuwa kigumu sana ukizingatia kuwa hizo drycleaning zimekuwa karibu sana kiuhusiano na wateja wao kiasi kwamba ni vigumu kwa wateja hao kuzikimbia.

-o-o-o-o-o-

Sasa basi, kuangalia upande mwingine wa shillingi, hii biashara inaweza kufanikiwa kama utajaribu kuongeza upana wa biashara yenyewe. Unachoweza kufanya ni kuweka mashine za self-service.

Yaani pamoja na kutoa huduma ya drycleaning, pia unaweka washers na dryers kwa wateja ambao wangependa kuosha nguo zao wenyewe. Kitakachotokea wateja watakuja na nguo zao, wataziosha, watazikausha, na kuondoka nazo papo hapo.

Wewe unachofanya ni kuwachaji gharama za utumiaji wa mashine zako tu. Mfano, unaweza kuwachaji load moja kwenye washer inagharimu kiasi kadhaa, na dyer kiasi kadhaa. Au ukaweka chaji moja kwenye combination ya utumiaji wa washer na dryer moja.

Vitu vinne muhimu vya kuzingatia kwenye self-service hii ni:

1) Kuhakikisha gharama za utumiaji wa mashine ni nafuu kuliko za drycleaning.
2) Kunakuwa na maji na umeme wa uhakika
3) Kuziweka hizo mashine katika hali ya usafi muda wote
4) Kuna usimamizi wa utumiaji wa hizo mashine ili zisiharibiwe na waharibifu

Well, ningependa kugusia suala la maji na umeme. Kama hii huduma ikichanganya, basi ujue kuwa itakugharimu maji na umeme zaidi kuliko kodi ya fremu. Kwa hiyo itabidi ujiandae vilivyo kwenye hivyo vitu viwili. Na kama unavyojua, maji na umeme ni matatizo sugu ambayo yako kwenye top 5 nchini mwetu. Na hiyo biashara bila ya hivi vitu viwili haiendi. Unajua hilo! Kwa hiyo, utakubidi uweke matanki na jenereta za kutosha.

Pia, itakubidi uwe mwangalifu kwenye suala la usafi wa maji. Kama unavyojua, maji ya dar ni maji tope. Kwa hiyo, ili usijekujikuta na lundiko la malalamiko kutoka kwa wateja kuhusu nguo zao kuchafuka zaidi (badala ya kusafishika), itakubidi utafute njia ya kuya-filter hayo maji. Nafikiri wizara ya maji ina ma-engineers ambao wanaweza kupatia mbinu ya ku-filter maji.

~~
ENEO NI MUHIMU. PUNGUZA GHARAMA ZA UENDESHAJI

Bado unaweza kuanza, kimkakati - mkoani sidhani kama italipa.

Kama upo Dar chagua eneo moja la kuhudumia kwa mfano vyuoni ukaanzania Mlimani ukaunganisha na vyuo vya jirani au nenda kwenye hostels kubwa kubwa. Hauhitaji kufungua duka ila unatakiwa kununua bajaj moja kuifanya kuwa duka la kutembea. Bajaj yako jaribu kuijengea ka-body and then tenga sehemu mbili; upande mmoja ya kuchukulia nguo chafu na upande wa pili kuchukulia nguo safi zinazorudishwa.

Kwa kuanza huhitaji mashine, ili kukupunguzia gharama za uendeshaji. Ajiri watu wawili wa kufua na mmoja wa kunyoosha na ku-pack nguo vizuri. Kazi hizi unaweza kuzifanya kutokea nyumbani (kama haukupanga chumba). Maji Dar ni mgao itakubidi kununua tank la kuhifadhia maji, ukipata ya kubeba lita 5000 itafaa sana. Ajiri mlinzi mmoja kukuangalizia nguo zilizoanikwa.

Hii ni biashara kama zingine hakikisha unapata vibali na kujitambulisha kama mlipa kodi ili kuhalalisha shughuli zako. Tafuta label yako ya kukutambulisha eg DOWANS Laundry Services. Label na contact zako zote ziweke kwenye bajaj, zing'arishe kadri utakavyoweza. Kazi kubwa utakayofanya mwanzo mwanzo ni kutambulisha biashara (promotion) na kazi hii itabidi uifanye bila kuona aibu. Kwa huo mtaji nakushauri kazi ya promotion ufanye mwenyewe na jinsi hiyo itakubidi pia uwe dereva bajaj.

Nakutakia mafanikio mema.
WAWEZA KUANZA NA MASHINE NDOGO. HAKIKISHA OFISI INAVUTIA

Mayu nataka nikutie moyo kuwa unaweza kabisa kufungua hiyo biashara kwa huo mtaji wako wa m7 (nahisi ni hela yako ya uhamisho ).

Chakufanya kwanza anza na mashine ndogo ya wastani najua mkoani wateja mwanzo hawatakuwa wengi kivile, nunua washing mashine ya kama m1 hadi m2, inatosha sana kwa kufulia nguo za kawaida kama mashati, suruali, magauni, sketi, bauzi.pia mashuka, mapazia,nk.

Makoti hayafuliwi na washing mashine yana utaratibu wake wa ku dry clean, waweza tafuta kuna dry cleaner simple kwa aajili ya kusafishia makoti manual.

Pia tafuta mshine ya kusafishia makarpet ya kama lk5 inatosha sana nahii unaweza kuwafuata wateja hata majumbani si lazima walete ofisini.

Cha umuhimu tengeneza ofisi kali inayovutia nje na ndani, weka muudumu smati hakikisha unatoa muda sahihi kwa mteja kuja kuchukua nguo zake.

Hakikisha unapata mifuko ya plastiki na enga simple kuwekea nguo za wateja.

Siku za mwanzo uwe kipromotion zaidi kwa kutoa viofa vya hapa na pale mfano, mteja kaleta nguo kumi basi mbili mwambie unamfanyia free.

Mikoani kuna tv cable zinafanya matangazo bei powa sana, peleka matangazo,tengeneza vipeperushi vizuri jisifie sana kuwa unafua kutumia mashine na utaalamu wa kisasa zaidi.

Kaunta ukiweza weka ka pc pale, feed kila kitu ili uwe unatoa risiti nk utaonekana makini na smati zaidi.

Hakikisha at start zoezi unalisimamia wewe mwenyewe na hakikisha customer care ndio silaha yako no moja.

Jitahidi upate ofisi sehemu nzuri kama katikati ya mji, unahitaji ofisi kwa maana ya sehemu ya kupokelea na kutoa nguo, hii ndio inayohitajika iwe ya viwango.

Pia unahitaji sehemu ya kufulia na kuanikia hii inaitwa factor, hapa inaweza kuwa hata nyumbani kwako kama utakosa sehemu utakayoshindwa kuigawa ofisi na factory.

Pia kuwa mjanja si kila mara uwe unatumia washing mashine wakati mwingine tumia watu wako kufua kawaida labda kwa nguo maalum.

Google namna mbali mbali za kufua aina mbali mbali na kupiga basi even how to dry clean suit nk jifunze mwenyewe kisha wafundishe watu wako na wasimamie.

Mwisho nakutakia kila la heri ndugu yangu na usisite kurudi ukumbini kutujuza yaliyojiri
VIFAA VINAVYOHITAJIKA KATIKA BIASHARA

Mashine zinazohitajika kwa kuanzia ni kama zifuatazo, (ingawa itategemea hasa mtaji ulionao na aina ya huduma unazotarajia kutoa)

1. Dry cleaning machine - 16kg kwa kuanzia inatosha kwa population ya watu 40,000
View attachment 42877

2. iIroning table - aspiration with boiler (height adjustable)
View attachment 42878
3. Stain removing machine
View attachment 42879
4. Packaging machine
View attachment 42880
5. Industrial washing machine (16kg inafaa kuanzia) - hii ni mashine kwa ajili ya kufulia mablanketi nk
View attachment 42881
6. Domestic washing machine (16kg)
View attachment 42882
7. Wringer (8kg) - kwa ajili ya kukausha nguo

8. Compressor
View attachment 42886
9. Computer equipment (cash register, ticket printer etc)

10. Clothes rack - kwa ajili ya kuning'iniza nguo - hii unaweza itengeneza kwa kutumia local materials hapo hapo dukani
 
carmel,

Assumption - Unaangalia uwezekano wa kuanzisha hiyo biashara Dar.

Kulipa kwake kutategemea na nguvu za kiasi gani utawekeza kwenye kuiba wateja wa drycleaning ambazo tayari zina majina. Kuna mlolongo wa drycleaning stores jijini ambazo zimeshakamata sehemu na wateja muhimu wa hiyo huduma.

Hii biashara ni moja ya biashara ambayo soko la ukua polepole sana. Hii ina maana kiwango cha namba ya wateja wapya kujiingiza kwenye uhitaji wa huduma hii ni ndogo sana. Hii inatokana na kuwa, huduma hii bado inaangaliwa kama huduma ya 'anasa' kwa asilimia kubwa ya watu. Kwa hiyo, utakuta asilimia kubwa ya wateja ni hao hao miaka nenda miaka rudi.

Hivyo basi, ili uweze kufanikiwa, itakubidi usuke mbinu za kuwaiba wateja wa drycleaning zingine. Kitu ambacho kinaweza kuwa kigumu sana ukizingatia kuwa hizo drycleaning zimekuwa karibu sana kiuhusiano na wateja wao kiasi kwamba ni vigumu kwa wateja hao kuzikimbia.

-o-o-o-o-o-

Sasa basi, kuangalia upande mwingine wa shillingi, hii biashara inaweza kufanikiwa kama utajaribu kuongeza upana wa biashara yenyewe. Unachoweza kufanya ni kuweka mashine za self-service.

Yaani pamoja na kutoa huduma ya drycleaning, pia unaweka washers na dryers kwa wateja ambao wangependa kuosha nguo zao wenyewe. Kitakachotokea wateja watakuja na nguo zao, wataziosha, watazikausha, na kuondoka nazo papo hapo.

Wewe unachofanya ni kuwachaji gharama za utumiaji wa mashine zako tu. Mfano, unaweza kuwachaji load moja kwenye washer inagharimu kiasi kadhaa, na dyer kiasi kadhaa. Au ukaweka chaji moja kwenye combination ya utumiaji wa washer na dryer moja.

Vitu vinne muhimu vya kuzingatia kwenye self-service hii ni:
1) Kuhakikisha gharama za utumiaji wa mashine ni nafuu kuliko za drycleaning.
2) Kunakuwa na maji na umeme wa uhakika
3) Kuziweka hizo mashine katika hali ya usafi muda wote
4) Kuna usimamizi wa utumiaji wa hizo mashine ili zisiharibiwe na waharibifu

Well, ningependa kugusia suala la maji na umeme. Kama hii huduma ikichanganya, basi ujue kuwa itakugharimu maji na umeme zaidi kuliko kodi ya fremu. Kwa hiyo itabidi ujiandae vilivyo kwenye hivyo vitu viwili. Na kama unavyojua, maji na umeme ni matatizo sugu ambayo yako kwenye top 5 nchini mwetu. Na hiyo biashara bila ya hivi vitu viwili haiendi. Unajua hilo! Kwa hiyo, utakubidi uweke matanki na jenereta za kutosha.

Pia, itakubidi uwe mwangalifu kwenye suala la usafi wa maji. Kama unavyojua, maji ya dar ni maji tope. Kwa hiyo, ili usijekujikuta na lundiko la malalamiko kutoka kwa wateja kuhusu nguo zao kuchafuka zaidi (badala ya kusafishika), itakubidi utafute njia ya kuya-filter hayo maji. Nafikiri wizara ya maji ina ma-engineers ambao wanaweza kupatia mbinu ya ku-filter maji.

~~
 
Umeme na maji ni issue hapo, Biashara yeyote TZ inayotegemea umeme kutoa product zake ni ngumu sana kufanikiwa. Ndio maana bila umeme wa kuaminika na bei nzuri maendeleo nchi ile ni ndoto maana kila kitu kinategemea umeme!
 
Habari wana jamvi, mimi ni mwanamke mjasiriamali, bado niko kwenye utafiti, maandalizi na huku nikiendelea kutafuta wateja naomba mnishauri pale mnapoona muhimu.

Ninaanzisha biashara ya kufua nguo(lakini ofisi yangu iko nyumbani na nitakuwa nafulia kwa mashine hapa nyumbani) na pia kufanya usafi majumbani kwa wateja.

1.Kufua nguo - Najua kuna baadhi ya watu wanapata challenge kutokana na mahousegirl kutokufua nguo vizuri hasa zile nguo muhimu kama za kazini, mashuka n.k hivyo nimepanga kuwa nawafulia na kupiga pasi nguo za wateja, ambapo mteja akijiandikisha atakuwa akilipa mwisho wa mwezi kwa bill, mimi nitakuwa nafuata hizo nguo kwake naenda kuzifua na kupiga pasi kisha narudisha nitafanya hivyo mara nne kwa mwezi yani kila wiki kwa wateja wacontract na gharama haitakuwa kubwa itarange kutoka 65,000Tshs+ kwa mwezi kutokana na ukubwa wa kazi yake. pia nitakuwa nachukua na wasiokuwa kwenye contract hao tutakubalina bei.

2. Kufanya usafi majumbani, ninafahamu kuna watu nyumba zao zinafanyiwa usafi usioridhisha na mahousegirl, pia nitakuwa na contract ambapo nitakuwa ninafanya usafi kila wiki mara 4 kwa mwezi kwa wateja wangu wa mkataba na cost itaanzia 120,000+ kwa mwezi pia nitachukua wateja wa maramoja bei tutakubaliana na huduma itainclude:

a) Kusugua tiles/sakafu/sahani ya choo/ masink
b) Kuosha kuta madirisha n.k
c) Kuosha vyombo vyote kabatini na kupanga
d) Kupanga sitting,dining room na kusafisha vyumba vyote vya ndani mteja akipenda
e) Kwa ujumla usafi wote wa nyumba kama nitakavyokubaliana na mteja.

Nimeanza kununua vifaa na kutrain kikundi changu lakini ninawateja wachache sana ambao wameconfirm wanahitaji mpaka sasa na bado ninawasiwasi na jinsi ya kupata wateja na nimeona hapa jamii forum mwaweza kunishauri kuanzia jinsi ya kutoa huduma hadi jinsi nitakavyopata wateja zaidi. Nitaanza rasmi January 2011 hapo naamini team yangu itakuwa imejipanga vizuri. tafadhali ushauri na maoni yenu ni muhimu sana kwa hii biashara yangu mpya.
 
Hii post wameisoma wengi lakini naona hakuna hata mmoja aliyetoa maoni, lakini nina imani utapokea maoni ya utosha tu watu wakitoka kwenye jukwaa la siasa! Kwanza nikupongeze kwa KUTHUBUTU! Biashara kama hii sijaisikia hapa Bogo (Ni jambo la ubunifu lenye matumaini makubwa sana hapo mbele). Naomba nikushauri mambo kadhaa!
  1. Bei: binafsi naona kama umeanza na bei ya juu kidogo, ungeanza na hesabu ambayo iko chini, kisha bei kupanda kulingana na ukubwa wa familia na Nyumba! Biashara ikishaenda vizuri unapandisha bei taratibu.
  2. Nashauri usiwe na mabinti kibaao, watu wataona ni heri house girl! Kuwa na staff ndogo ya vijana wanaojiheshimu.
  3. Kwa bei hiyohiyo pia unaweza kuweka huduma ya dry cleaning.
  4. Tangaza biashara yako: Pita katika majumba na maofisi eleza faida ya kutumia huduma zako, toa bizcards na brochures.
Amini nakwambia, utafanikisha, KEEP IT UP!
Wakati bado naishi mjini niliwahi kuwaza kuanzisha huduma ya glass washing kwa maghorofa marefu ya vioo! Wadau wakanishauri majengo
 
Kwa mfumo wa maisha tunaokwenda nao sasa hivi,hii ni biashara nzuri na itakulipa sana,isiwe majumbani tu,nadhani hata maofisi mengi siku hizi wanatumia mtindo huu. Mi si mtalaam wa biashara,mchango wangu utakuwa ktk manpower yako,hasa usafi wa vijana wako kimwili na kiroho. Ukifaulu hapo,utashangaa itakavyo panuka( usisahau kuwa na gardener japo mmoja ktk team yako)
 
Yaap!! Amoeba, many congrats for comin out with something! Additional advice is "Please make sure you have VETTED PROPERLY "those workers manake uaminifu wa hali ya juu unatakiwa for such bussiness , otherwise wizi na udokoaji wa mali kwenye maeneo ya kazi unapokwenda fanya hizo services or upotevu wa nguo ulizochukua za wateja unaweza haribu biashara yako hiyo kabisaa!
 
Thanks Superstar usijali utazipata, nitaanza rasmi January sasa hivi tunajifua january nitaadvertise,

Bei: binafsi naona kama umeanza na bei ya juu kidogo, ungeanza na hesabu ambayo iko chini, kisha bei kupanda kulingana na ukubwa wa familia na Nyumba! Biashara ikishaenda vizuri unapandisha bei taratibu. - Thanks Nafanyia kazi suala la bei, wadau wengine mnasemaje kuhusu bei??
  1. Nashauri usiwe na mabinti kibaao, watu wataona ni heri house girl! Kuwa na staff n
  2. dogo ya vijana wanaojiheshimu. Nina 1 girl 2 Boys so far lakini ni kweli itakuwa haimeki sense
  3. Kwa bei hiyohiyo pia unaweza kuweka huduma ya dry cleaning. good idea, Nafikiri nahitaji kujua zaidi kuhusu Dry cleaning
Malila na bunsen burner nashukuru kwa ushauri wenu. Napata moyo sana.
 
Kwakeli ni ubunifu mzuri mtaani kwetu yupo kijana anafanya kazi kama yako yy anafanya kufua na kupiga pasi jioni anakuletea japo yupo kiloko ila kwa jinsi yako naamin una maono makubwa na utafanikiwa zaidi kwani wengi awtakuwa na haja ya mausigeli tena.
 
Hongera sana ndugu kwa ubunifu wa huduma inayohitajiwa na wengi.Ila kama alivyosema Amoeba hapo juu, anza kidogo kidogo kwa maana ya bei.

Kumbuka kwa wale wenye kuzoea kupeleka nguo dry cleaners hutumia karibia kiasi hicho hicho na wengi wenye kuweza kukulipa kiwango hicho wanazo machine zao za kufulia nyumbani.

Watakaopenda huduma yako ninavyoona ni wale wasiokuwa na mbadala na wengine wanao dobi wanaowafanyia kazi hiyo ama majumbani au kuchukua nguo kwenda kuzifua na kuzirudisha.

Bei za dobi nadhani siyo ghali sana kama bei uliyopanga.

Kuhusu usafi wa majumbani pia wapo wanaofanya na kwa mwezi kutegemeana na uzito wa kazi ikiwemo ukubwa wa nyumba huanzia 50,000/= hadi 500,000/=

Ila usiache kuifuatilia biashara hii maana inalipa.
 
Wadau naombeni msaada wenu wa mawazo kwani naamini yupo mwenye kujua kuhusu hili.

Nini capital kama 7milion nataka kuanzisha dry cleaner katika sehemu ambayo hakuna kabisa hiyo kitu. Je, capital hiyo inaweza kutosha, pia sijui ni mashine gani nzuri ya kufulia bei ya wastani.

pia nahitaji kujua nahitaji washing machine kama ngapi kuanzia labda ya kufulia nguo za kawaida suti, na kusafisha macarpet.

Nawasilisha
 
Labda ungeongeza hiyo capital maana hapo pango bado machines ni bei kidogo kama ukiagizaa kuna watu wanagiza au kama unaweza uagize mwenyewe ila kwa 7m nakushauri uongeze kama 7m zingine, la sivyo badilisha biashara! Nunua bajaj 2 ndio size yako...kwa pesa hiyo. Ni ushauri wangu tu. Nami nilifanya research 2yrs back.
 
Thanks,

Hata mie nina wazo la hiyo biashara. Sasa ni vizuri umesema umefanya research miaka miwili iliyopita. Unaweza tumegea mchanganuo wake japo roughly?

Thanks
 
Thanks,

Hata mie nina wazo la hiyo biashara. Sasa ni vizuri umesema umefanya research miaka miwili iliyopita. Unaweza tumegea mchanganuo wake japo roughly?

Thanks

Asante mkuu namimi nilitaka kujua hivyo.

Mimi yangu nataka kufungulia mkoani na haswa kinacho nitatiza ni suti, siitaji kubwa sana kama za huku dar siunajua tena mambo ya mkoa.
 
Wana JF wajasirimali.

Kwanza unatakiwa ujue kuwa kila dry cleaner machines zina kilo tofauti bei yake inatokana na hizo kilo kuanzia 10kg and above.

Kama unataka ziwe mbili ina maana utaagiza set hizo 2 na machine za kusuuza kunyooshea pia.

Nawapa link kwanza msome mjue hata zina hitaji nini, pia umeme lazima uwe 3phase line.

Dry Cleaning Machine (Series CBC-4) - China Dry Cleaning Machine, Washing Machine, Dryer Machine in Washing & Drying Machine

Dry Cleaning Machine (22kg) - China dry cleaning machine, industrial dry cleaning machine, industrial washing machine in Cleaning Machine

Sasa anzia pango la sehemu..vibalii. umeme na kuagiza kutoa bandarini na kuzifunga, then cost za ndani sasa, abuni etc.

Jipange sawa sawa. All the best$
Uliza bei kwa hizo link watakupa haraka sana ila FOB ni kama 5,000 hivi dola
 
Wana JF wajasirimali...kwanza unatakiwa ujue kuwa kila dry cleaner machines zina kilo tofauti bei yake inatokana na hizo kilo kuanzia 10kg and above....

Kama unataka ziwe mbili ina maana utaagiza set hizo 2 na machine za kusuuza...kunyooshea...pia...

Nawapa link kwanza msome mjue hata zina hitaji nini...pia umeme lazima uwe 3phase line...

Dry Cleaning Machine (Series CBC-4) - China Dry Cleaning Machine, Washing Machine, Dryer Machine in Washing & Drying Machine

Dry Cleaning Machine (22kg) - China dry cleaning machine, industrial dry cleaning machine, industrial washing machine in Cleaning Machine

Sasa anzia pango la sehemu..vibalii umeme na kuagiza kutoa bandarini. na kuzifunga, then cost za ndani sasa, sabuni etc.

Jipange sawa sawa. All the best$
Uliza bei kwa hizo link watakupa haraka sana ila FOB ni kama 5,000 hivi dola

Good info:

Hebu saidia zaidi
1) Hii machine inanyoosha nguo automatically? Naona kwenye hiyo ya 22Kg inaonyesha hivyo.
2) Ina hitaji chumba cha ukubwa gani kwa mujibu wa utafiti wako?
3) Nini conditions zingine ambapo hiyo machine inatakiwa iwekwe?

1.Ukubwa unategemea na unataka machine ngapi na pia machine huwa zinakaa kwa nyuma. Kumbuka mbele si mapokezi unaweka partition ili wakati mchakato(usiku) unafua, wateja hawaoni pia lazima kunakuwa sehemu kutolea mvuke.

Hiyo machine ni ya kisasa zaidi na ndio ya katikati. Kwa kuanzia sio mbaya.

Wakati mwingine unahitaji generator(onana watalam wa umeme na size hizo ujue ukubwa wa generator). Kama umeme unasumbuaa maana kazi za watuu zitalala.
 
1.Ukubwa unategemea na unataka machine ngapi...na pia machine huwa zinakaa kwa nyuma...kumbuka mbele si mapokezi...unaweka partition...ili wakati mchakato(usiku) unafua..wateja hawaoni....pia lazima kunakuwa sehemu kutolea mvuke...

Hiyo machine ni ya kisasa zaidi...na ndio ya katikati...kwa kuanzia sio mbaya..

Wakati mwingine unahitaji generator(onana watalam wa umeme na size hizo ujue ukubwa wa generator)...kama umeme unasumbuaa maana kazi za watuu zitalala...

Mkuu asante kwa info nzuri sasa umenipa mwangaza zaidi, nadhani nimepata pa kuanzia.
ingawa bei inaonekana kama imesimama, vipi uliwahi kujaribu kucheck amazon na ebay kwa used mashine?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom