Natafuta marafiki wa kiume na wa kike nitao shirikiana nao kukwamuana na umasikini

Visionor

Member
Nov 9, 2017
20
14
Habari ndugu,

Mimi ni mtanzania mwenzenu najitokeza kutafuta marafiki tutaosaidizana kujikwamua na umasikini kwa kushauriana, kutembeleana.

Sifa za marafiki niwatakao;
Awe anajua kusoma na kuandika
Umri 18-na kuendelea
Sina ubaguzi wa dini,
Sina ubaguzi wa kabila
Sina ubaguzi wa mali masikini na matajiri wote ni ndugu zangu.

Utayari wangu kwako.
Nipo tayari kufika popote pale panapo mpendeza Mungu.
Nipo tayari kutumwa popote pale ambapo panampendeza Mungu nitaenda.
Nipo tayari kukusaidia kazi yeyote ile ila iwe yenye kumpendeza Mungu.
Nipo tayari kufanya chochote kile kinacho mpendeza Mungu kwa pale nitapo shauriwa/kuambiwa.
Nipo tayari kufanya kazi yeyote ile yenye kumpendeza Mungu nitakapo tumwa.
Kwakifupi nipo tayari kutekeleza mikakati/mipango tutayo iweka ile inayo mpendeza Mungu.
Nipo tayari kushirikiana na wewe katika shida na raha ili kuinuana na kumfukuza adui masikini.
Unajua unaweza kua umeajiriwa na kupata mshahara lakini hautoshi kutoshereza mahitaji yako hivo ndio wakati wa kubadilika.
Unajua unaweza kua ni masikini lakini kwa muungano huu tukainuliwa.
Unajua masikio tumepewa kazi yake ni kupokea kitu kutoka nje tunapo ambiwa au kushauriwa.
Unajua mdomo tumepewa kuongea kile kitu ambacho kipo ndani unakiwaza ila kiwe nikile cha kumpendeza Mungu.
Namalizia kwa kusema niite nami nitaitika popote pale nitafika ila ulichoniitia kiwe nicha kumpendeza Mungu.

Mwana maono mwenzangu kama upo tayari naomba ni pm kwa mawasiliano zaidi. Nawakaribisha ninyi nyote nasema karibuni.
 
Karibu sana mkuu.

Nakuona mpyaaaa
Tutashirikiana kwa pamoja.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom