Chunusi: Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Tafuta hiyo dawa...
images (2).jpeg
 
Kitu kingine usichojua ni kwamba unapotumia medicated soap kwa muda mrefu unaua wadodo Kinga ambao walipaswa kupambana na baadhi ya wadudu wabaya. Hivyo wanapopata wasaa was kukuingia hawana upinzani hivyo kukupa au kuafanya shida yako kuwa endelevu.

Pia pamoja na ushauri uliopewa hakikisha kill siku Kabla ya kulala unaosha uso kwa sabuni ya kawaida, foronya ya mito na mashuka yanabadikishwa ikiwezekana kill baadae ya siku moja mpaka utakapoona Hali inatengemaa.

Pia umri wako unaeeza kuwa chanzo kwani kuanzia umri was kubalahe Hadi 25 hormonal changes zinaweza pelekea chunuzi. Ila umepita happy angalia mahusiano yako na mpenzi wako....

Pia Kama ni wakike Kuna baadhi ya magonjwa UTI hupelekea hiyo Hali chunguza Hilo pia.

Ni Mimi bush Dokta kutoka Makete
 
Boss dawa ni nying but kunywa remycin itatoa vijidudu kwenye damu. Tumia clindamycin gel kuua vijidud kwenye ngozi dawa ya kuondoa madoa utachagua mwwenyewe kati ya ulizotajiwa juu but huaga nashauri sana watu watumie adepalene gel kwa matokeo ya haraka zaid

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hello! Mambo vipi?

Leo itakuwa siku poa sana kwako kama unasumbuliwa na chunusi au madoadoa usoni yatokanayo na chunusi. Kama husumbuliwi na matatizo hayo sio mbaya pia kwa sababu utajiwekea akiba na kusaidia ndugu, jamaa na marafiki zako.

Unajua kwamba madoadoa ya chunusi kwa kiasi kikubwa yanasabishwa na kupasua chunusi? Pia je, unajua kwamba chunusi huweza kusababishwa na vipodozi vyako mwenyewe ambavyo unatumia hata kama ni salama na vimesajiliwa na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)?

Unajua kwamba vipodozi kama Carotone, Caro light, Bronze tone, Extra Clair, Maxi White nk huchangia sana kusababisha chunusi na hatimaye madoadoa?

Kama ulikuwa hujui basi habari ndo hiyo. Kuna mambo mengi zaidi ya hayo na nitaendelea kukuelimisha na kukushauri kadiri muda utakavyoruhusu.

NINI HUSABABISHA CHUNUSI?
Chunusi huweza kusababishwa na kuongezwa na moja kati ya vitu vifuatavyo:
1. Maambukizi ya bakteria wa chunusi
2. Homoni nyingi za uzazi mwilini, ujauzito na dawa za kupanga uzazi
3. Vipodozi vyenye kemikali kali na vile visivyoendana na ngozi yako
4. Vyakula vyenye mafuta mengi na viungo vya kwenye chakula
5. Msongo (Stress)
6. Mafuta mengi usoni
7. Vumbi na uchafu mwingine kuziba matundu ya ngozi (ya kutokea mafuta)

Sawa?

Sasa kama umeelewa hayo basi kwenye kuzuia itakuwa rahisi maana utakuwa unayapunguza au kujiepusha nayo tu (Kwenye ujazuito sijui utafanyeje …… )

JINSI YA KUZUIA CHUNUSI ZISIENEE WALA KUKUACHIA MADOADOA
Zaidi ya miaka mitano sasa tumekuwa tukiwaelimisha na kuwashauri kuhusu ngozi na vipodozi na maendeleo yamekuwa mazuri. Tumekuwa tukikushauri usipasue chunusi, badala yake tumia dawa vizuri na chunusi zitanywea na kukauka zenyewe bila kukuachia vidonda wala madoadoa.

Pia tumekuwa tukikushauri kama unasumbuliwa na chunusi na mafuta mengi basi ni muhimu sana kudhibiti mafuta kwanza kabla ya kuanza kushambulia chunusi kwa nguvu kubwa na kupata matokeo polepole.

Matibabu ya chunusi hutofautiana kati ya mtu na mtu kutegemea na chanzo cha chunusi, aina ya ngozi, umri na mtindo wa maisha hivyo unatakiwa kupata ushauri wewe kama wewe na kutumia matibabu yanayoendana na mazingira yako.

Ukitaka kuzuia chunusi zisienee wala kukuachia madoadoa fanya mambo yafuatayo:
1. Pata ushauri hospitali au kwa mtaalam ili kujua jinsi ya kudhibiti vizuri zaidi chunusi zako na kuanza matibabu haraka. Kama chunusi zako zimesababishwa na bakteria utapewa dawa ya kuua bakteria hao na kukusaidia chunusi zako kuisha haraka badala ya kuenea na kukuachia madoadoa
2. Usipasue chunusi zako, maana kupasua chunusi ni kama kumwagia petrol kwenye moto

3. Tumia face wash/facial cleanser au sabuni za kusaidia kuondoa uchafu na vijidudu kwa ufanisi mkubwa zaidi kuliko sabuni za kawaida. Pia tumia poda kwa ajili ya kukausha mafuta na kukusaidia kuiweka ngozi yako iwe laini.
4. Punguza kiasi cha mafuta na viungo unavyokula – epuka vyakula vyenye mafuta mengi, epuka vyakula vyenye viungo vingi na pikia kwa mafuta na viungo kiasi cha wastani tu
5. Pambana na msongo (Stress). Hii haitakusaidia katika kudhibiti chunusi tu bali hata kwenye magonjwa ya moyo, presha, sukari, akili, vidonda vya tumbo, nguvu za kiume na kadhalika.
6. Acha kutumia vipodozi vyenye sumu na pia usitumie vipodozi visivyoendana na ngozi yako. Hii watu wengi wenye ngozi ya mafuta wamekuwa wakikosea sana kwa kutumia losheni au mafuta kwa ajili ya ngozi kavu na hatimaye kutokwa na vipele na chunusi kuongezeka.

Unaona? Mambo ni rahisi tu kama hivyo na ndani ya wiki moja tayari unaanza kufanikiwa kudhibiti chunusi zako.

Sasa kazi ni kwako kuchagua – kuendelea na mazoea au kufuata ushauri wa kitaalam.
AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS tunakushauri uachane na stori za kitaa na ufuate ushauri wa kitaalam. Pia usile kila kitu unachokutana nacho mtandaoni, vingine sio kwa ajili yako.

Uwe na siku njema!

Kama unatumia whatsapp na ungependa kupata madarasa ya afya, urembo na vipodozi; orodha ya vipodozi visivyo salama; matatizo ya ngozi nk basi tucheki tu kwa namba 0719326693 na tutakutumia. Free for you!

Pia kama unahitaji kujifunza zaidi kuhusu afya, urembo na vipodozi kila siku hadi mwisho wa mwezi basi tutumie meseji whatsapp kwa namba hiyo hiyo na kisha tutakutumia link ya kujiunga na group letu la whatsapp na utapata elimu na ushauri zaidi. Free for you!

Kama unasumbuliwa na tatizo (afya, urembo au vipodozi) na unahitaji kuondokana nalo sasa tupigie simu au tutumie meseji au whatsapp na tutakushauri pia. Mawasiliano ya haraka ni 0743422883 na 0719326693; email ni afyazaidi@gmail.com

See you next time!

madoadoa.jpg
 
1.Nenda hospitali kwa dokta wa ngozi.
Au nunua acnotin mg20 kunywa 1×2 kwa siku 30

Nawia sabuni ya jamaa au sabuni yoyote isiyo na kemikali sana
Pakaa Hydrogenperoxide (dawa ya vidonda) na pamba usoni kaa nayo kwa dakika 20 then nawa na maji ya uvuguvugu
Pakaa Epiderm Cream Usoni asubuhi na jioni


Acnotin ni kwaajili ya chunusi
HydrogenPeroxide na Epiderm cream ni kwa madoa


Usipopona ndani ya mwezi basi umerogwa ndugu.
1.Nenda hospitali kwa dokta wa ngozi.
Au nunua acnotin mg20 kunywa 1×2 kwa siku 30

Nawia sabuni ya jamaa au sabuni yoyote isiyo na kemikali sana
Pakaa Hydrogenperoxide (dawa ya vidonda) na pamba usoni kaa nayo kwa dakika 20 then nawa na maji ya uvuguvugu
Pakaa Epiderm Cream Usoni asubuhi na jioni


Acnotin ni kwaajili ya chunusi
HydrogenPeroxide na Epiderm cream ni kwa madoa


Usipopona ndani ya mwezi basi umerogwa ndugu.
mkuu lotion au mafuta mazuri y kutumia pind unapotumia tiba hii ni IPI?
 
1.Nenda hospitali kwa dokta wa ngozi.
Au nunua acnotin mg20 kunywa 1×2 kwa siku 30

Nawia sabuni ya jamaa au sabuni yoyote isiyo na kemikali sana
Pakaa Hydrogenperoxide (dawa ya vidonda) na pamba usoni kaa nayo kwa dakika 20 then nawa na maji ya uvuguvugu
Pakaa Epiderm Cream Usoni asubuhi na jioni


Acnotin ni kwaajili ya chunusi
HydrogenPeroxide na Epiderm cream ni kwa madoa


Usipopona ndani ya mwezi basi umerogwa ndugu.
Zipo maduka ya dawa na vipodoz??
 
Mkuu, chukua liwa, manjano, kiini cha yai (bichi). Liwa vijiko 2 na manjano 2. Koroga na ujipake ikishaganda lala nayo. Nusu bakisha utajipaka kesho. Kesho kutwa weka tena mixer yako. Mpaka utakapoona umepata nafuu. 14 daya maximum utakuwa umepona.

Jiandae kuchafua matandiko.
 
Kuna Acnotin za 10mg and 20mg. Kama tatizo lakobni kubwa yani una chunusi nyingi unatumia 20mg na kama unazo za kawaida basi unaweza tumia za 10 mg. Bei ya 10mg kwenye pharmacy nyingi ni 15,000-18,000 kwa vidonge 10. But kuna pharmacy ipo kkoo mtaa wa kongo (in case upo dsm) bei yao ipo chini kidogo. Vidonge thelathin wanauza 36,000 if not 39,000. Halafu 20mg inarange kwenye 18,000-20,000.
Bei vipi??
 
Back
Top Bottom