Chunusi: Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

1.Nenda hospitali kwa dokta wa ngozi.
Au nunua acnotin mg20 kunywa 1×2 kwa siku 30

Nawia sabuni ya jamaa au sabuni yoyote isiyo na kemikali sana
Pakaa Hydrogenperoxide (dawa ya vidonda) na pamba usoni kaa nayo kwa dakika 20 then nawa na maji ya uvuguvugu
Pakaa Epiderm Cream Usoni asubuhi na jioni


Acnotin ni kwaajili ya chunusi
HydrogenPeroxide na Epiderm cream ni kwa madoa


Usipopona ndani ya mwezi basi umerogwa ndugu.
Umenena mkuu! Nilisumbuliwa na chunusi kwa zaidi ya miaka kumi. Nilimaliza hizo persol zote, oriflame ma package kwa ma package, dawa za asili, hosp nilienda mpaka nikachomwa masindano nsiyoyajua ila hatimae mwaka huu nikaenda kujaribu kwa prof mgonda aghakan....sina la kusema ila kila mtu haamini akiniona! Acnotin ni vidonge mujarab kwa machunusi sugu maana mimi yalikuwa makubwa makubwa, yakicharuka napata mpaka homa!! Nilikuwa na chunusi zinatunga usaha basi hata kula na watu nlikuwa naona tabu maskini ila nw...kweli mungu ni mwema! Ila ushauri wangu ni kwamba asinywe mpaka amuone dr, mi nilianza na 1×2, mpaka 3×2 na prof alinambia namnukuu 'tatizo sio hosp ngapi umeenda au dawa gani umekunywa, tatizo ni utoaji dozi lazima uwe na utaalam nao...'
 
Daah Tusaidieni basi wahanga wa haya mambo,

Mnatuchanganya Mjue mara tumia hichi mara nenda kule full mvuruganooo. which is which????
Natamani ningetuma picha zangu za before na after ila ndo hivo tena tushaamua kujificha nyuma ya pazia ila kwa herufi kubwa nakwambia Acnotin vidonge ni the best ila upate dr apime uzito wako na ukubwa wa tatizo lako then akupangie dozi. Utakuja kuturingishia humu. Hizo biashara za watu tupa kule zitawapotezea hela na muda mi walinila si haba!
 
Umenena mkuu! Nilisumbuliwa na chunusi kwa zaidi ya miaka kumi. Nilimaliza hizo persol zote, oriflame ma package kwa ma package, dawa za asili, hosp nilienda mpaka nikachomwa masindano nsiyoyajua ila hatimae mwaka huu nikaenda kujaribu kwa prof mgonda aghakan....sina la kusema ila kila mtu haamini akiniona! Acnotin ni vidonge mujarab kwa machunusi sugu maana mimi yalikuwa makubwa makubwa, yakicharuka napata mpaka homa!! Nilikuwa na chunusi zinatunga usaha basi hata kula na watu nlikuwa naona tabu maskini ila nw...kweli mungu ni mwema! Ila ushauri wangu ni kwamba asinywe mpaka amuone dr, mi nilianza na 1×2, mpaka 3×2 na prof alinambia namnukuu 'tatizo sio hosp ngapi umeenda au dawa gani umekunywa, tatizo ni utoaji dozi lazima uwe na utaalam nao...'
mmmh mimi mwaka wa 13 huu nasumbuliwa na hilo tatizo,sema nimegugo hiyo dawa hadi nikaogopa.

side effects zake ni nyingi na zinatisha kwa kweli tena esp kwa sisi wanawake(inapelekea infertility),nahisi ndomana madoctor wengi hawarecommend hiyo dawa.
 
mmmh mimi mwaka wa 13 huu nasumbuliwa na hilo tatizo,sema nimegugo hiyo dawa hadi nikaogopa.

side effects zake ni nyingi na zinatisha kwa kweli tena esp kwa sisi wanawake(inapelekea infertility),nahisi ndomana madoctor wengi hawarecommend hiyo dawa.

Kwan wewe ni KE?
 
CHUNUSI ni tatizo la kawaida la ngozi linalowaathiri watu kipindi fulani cha maisha yao. Chunusi husababisha vipele vidogo vya mafuta kwenye ngozi na wakati mwingine hufanya ngozi kuwa na maumivu au kuhisi kuungua. Mara nyingi hutokea maeneo ya usoni, mgongoni na kifuani ambapo asilimia 15 ya wanaosumbuliwa na tatizo hili huwa na aina hii ya chunusi.
chunusi.png

Kwanini unapata chunusi?

Mara nyingi chunusi huhusianishwa na mabadiliko ya kiwango cha homoni kipindi cha balehe. Hata hivyo, zinaweza kuanza katika umri wowote. Baadhi ya homoni zilizo jirani na vinyweleo vya ngozi hutengeneza kiwango kikubwa cha mafuta. Mabadiliko haya hufanya bakteria wanaoishi kwenye ngozi bila kusababisha madhara kukasirika na kusababisha vipele vyenye usaha.

Pia, homoni hufanya utando mnene chini ya vinyweleo vya ngozi na kusababisha kuziba kwa vijitundu vya ngozi hatimaye kusababisha chunusi. Kuosha ngozi hakusaidii kuondoa tatizo la vijitundu kuziba.

Unaweza pia kurithi tatizo la chunusi. Ikiwa baba na mama yako walikuwa na chunusi kipindi fulani cha maisha yao basi kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuwa na chunusi.

Mabadiliko ya homoni yanayotokea kipindi cha hedhi au ujauzito yanaweza kusababisha chunusi kwa wanawake. Hakuna uthibitisho kuwa lishe, uchafu au ngono huchangia kutokea/kutotokea kwa chunusi.

Kina nani huathirika zaidi?

Chunusi hutokea zaidi kwa vijana. Takribani asilimia 80 ya watu wenye chunusi wana umri kuanzia miaka 11 hadi 30. Chunusi hutokea zaidi kwa wasichana kuanzia miaka 14 hadi 17 na kwa wavulana ni kuanzia miaka 16 hadi 19.

Chunusi huja na kuondoka kwa watu wengi kwa miaka mingi ambapo miaka michache baadae hali hii huanza kupungua. Watu wengi hupona kabisa tatizo hili wakiwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea.

Nifanye nini nikiwa na chunusi?

Usioshe sehemu ya mwili yenye chunusi zaidi ya mara mbili. Kuosha mara kwa mara kunasababisha mikwaruzo na kufanya hali kuwa mbaya.

Osha sehemu ya mwili kwa sabuni kidogo ukitumia maji ya uvuguvugu na si maji ya moto au baridi kupita kiasi kwa sababu hufanya chunusi kuwa na hali mbaya zaidi.

Usijaribu kuviminya vipele au kuvisugua kwa nguvu kwa sababu hufanya ngozi kuuma na kutengeneza makovu ya kudumu. Jiepushe kutumia vipodozi na manukato kwenye ngozi yenye chunusi. Tumia bidhaa za urembo zisizoziba matundu madogo ya ngozi yako.

Ondoa vipodozi vyote ulivyopaka kabla ya kwenda kulala. Ikiwa una tatizo la kukauka ngozi ni vyema kuchagua mafuta/vipodozi vinavyopendekezwa na wataalamu wa ngozi.

Kufanya mazoezi hakuondoi chunusi ila husaidia kuboresha hisia za kujipenda zaidi. Ni vyema kuoga haraka iwezekanavyo baada ya kufanya mazoezi, kwa kuwa jasho husababisha ngozi kuwasha. Kama una nywele ndefu ziweke katika hali ya usafi mara kwa mara na epuka kuzifanya ziguse usoni.

Matibabu ya chunusi yanaweza kuchukua hadi miaka mitatu ili kuanza kuonyesha kupona, usitegemee kupata matokeo mazuri kwa usiku mmoja tu. Ingawa chunusi haziwezi kutibiwa, ila zinaweza kudhibitiwa kwa matibabu mbalimbali kama mafuta na losheni.

Ni vyema kuwasiliana na mtaalamu wa ngozi au mfamasia kabla ya kutumia dawa yoyote. Wakati mwingine kiuavijasumu(antibiotiki) huhitajika hasa chunusi zikizidi kifuani na mgongoni.

Chanzo: Mtanzania
 
Nina sumbuliwa na chunusi yapata miaka saba sasa,nilishauriwa nisipake mafuta yoyote usoni lakini bado haijasaidia.Naona usoni nimekua na madoa na chunusi bado zipo. Nimeshauriwa nitafute clairmen cream,lakini naona ina hydroquinone ambayo wataalam wanasema so nzuri kwenye ngozi. Msaada wenu tafadhali, cream/lotion ninayoweza kutumia maana Uso hautamaniki. Mimi ni mwanaume,rangi ya ngozi yangu,maji ya kunde.
mkuu vp tatzo lako ulipatia ufumbuz?
 
Husika na kichwa cha thread hapo juu,lengo la huu uzi ni kutaka kusaidiana juu ya dawa zilizoweza kutumiwa na watu mbalimbali humu na kupona chunusi..Karibuni.
 
Daaaaah kuna mwanangu enzi hizo za kidumu na mfagio darasa zima yeye ndo alikuwa bingwa wa chunusi, zilimfanya akose kujiamini mbele ya wasichana hata wavulana wenzake, baada ya miaka mingi nimekutana nae dooooh kabadilika kabisa kawa soft mbaka sijaamini.
 
Husika na kichwa cha thread hapo juu,lengo la huu uzi ni kutaka kusaidiana juu ya dawa zilizoweza kutumiwa na watu mbalimbali humu na kupona chunusi..Karibuni.

Binafsi huko nyuma nilikuwa na ' michunusi ' kibao utafikiri ' Fenesi ' limeiva na nikawa nanunua dawa za bei / gharama kabisa ambazo nilikuwa nikiambiwa na wenye ' Mafamasi ' yao hapa mjini lakini sikuweza kufanikiwa kupona ila siku moja kuna ' Msela ' mmoja tu ambaye mwanzoni nilimdharau kama ambavyo Watanzania bila kusahau Waafrika huwa tunapenda kudharauliana na kuchukuliana poa aliniambia kuwa dawa nzuri ya kuondoa ' chunusi ' hasa katika nyago / uso ni hizi Sabuni mbili ambazo ni za bei nafuu sana ya FAMILY ambayo ni Tsh 500/= au ya CITRUS tena ile ya njano ambayo sasa ni Tsh 700 huku Kwetu ' uswazinyo / uswahilini ' na Tsh 800/= mpaka Tsh 1,000/= huko Kwenu ' uzungunyo / uzunguni '. Huwezi amini huu sasa ni mwaka wa tatu au wa nne natumia moja wapo ya hizo Sabuni na sijui zile ' Chunusi ' zangu nyingi zimekimbilia wapi kwani uso wangu ni safi hauna chochote hadi sasa ' Mademu ' wanajigonga tu wenyewe kwani ' nuru ' inaonekana usoni na Mwanamume ninang'aa ile mbaya.

Ukiona hizo Sabuni mbili tajwa hapo juu hazijakusaidia kuondoa ' Chunusi ' zako basi jua ya kwamba mwenye dawa nzuri ya kuziondoa atakuwa ni Shetani Mkuu tu Lucifa kwani utakuwa una dalili zote za kuwa na Pepo la Chunusi ambalo limetukuka kabisa katika mwili wako na hasa usoni.

Kila la kheri Mkuu ila mambo yote ni Sabuni za FAMILY Medicated Soap au CITRUS kwa matatizo ya Kutukuka ya Chunusi.
 
hyo citrus, nishawah ickia pia kuhusu hiyo

Wewe ukiona GENTAMYCINE ama anasifia kitu fulani au Mtu fulani au anakisiliba au anamkosoa basi jua 100% ni correct kwani huwa sibahatishi na sijawahi kubahatisha. Kwa matatizo ya ' Chunusi ' kama huna aina yoyote ile ya ' Pepo ' au ' Nuksi ' basi Sabuni za Family au Citrus ndiyo ' Kiboko ' yake.
 
Kama una tatizo au kusumbuliwa na chunusi kwa muda mrefu bac umepona, nakupa dawa ya bei ndogo kabixa naamini huwezi shindwa, nunua asali mbichi iwe safi, nunua pia mdalasini uliosagwa kisha chota vijiko sita vya asali (tumia kijiko cha kulia) na uchukue vijiko vitatu vya unga wa mdalasini(tumia kijiko cha chai) changanya vizuri kwenye chombo safi kisha upake kabla ya kulala kaanayo kwa muda wa dk 60 yaani 1hr then osha uso kwa maji ya uvuguvugu, kwa siku7 utakuwa na mabadiliko makubwa xana Ahsanteni
 
Wewe ukiona GENTAMYCINE ama anasifia kitu fulani au Mtu fulani au anakisiliba au anamkosoa basi jua 100% ni correct kwani huwa sibahatishi na sijawahi kubahatisha. Kwa matatizo ya ' Chunusi ' kama huna aina yoyote ile ya ' Pepo ' au ' Nuksi ' basi Sabuni za Family au Citrus ndiyo ' Kiboko ' yake.
umewah kubahatisha kitu flani hiviii,, ikabd nikushushe cheo ,toka captain had v 2
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom