Natafuta lawyer wa kuniandikia mikataba ya wapangaji wangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta lawyer wa kuniandikia mikataba ya wapangaji wangu

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Mbwambo, May 11, 2012.

 1. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Naomba Lawyer /mwanasheria wa kujitegemea au aliyeajiriwa ajitokeze atakayenisaidia kuandika mikataba ya wapangaji wangu jumla wako 8 kwenye biashara yangu ya kupangisha.
  Naomba awe na bei nafuu maana sina hela sana jamani.
  Majibu yafanyike kwa kunitumia "private message" jamiiforums, au awasiliane nami kwa email: ak_abduel@yahoo.com.
  NInaamini nimeeleweka
  :A S 465:
   
 2. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Je nikupe copy ya mkataba? kama wahitaji pm
   
 3. Micha

  Micha JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 269
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama hauna hela fanya hivi; mikataba ya kupangisha iko mingi sana na hata humu jf nafikiri watu waliwahi kuiweka, tafuta copy ya mkataba usome na ubadilishe kulingana na mahitaji yako, baada ya hapo mtafute lawer for rumber stamp only, kwa sababu hata lawyer wengi wana copy ya mikataba wanachofanya ni ku copy na kupaste halafu wanabadilisha kufuatana na unavyotaka lakini akija kwako atakwambia nimekuandalia mkataba ili akuchaji hela ndefu.
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,791
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Umuhimu wa azimio la arusha kurejewa!nyerere alikemea mtu kukunja 4 na kahawa kwa kupangisha majumba
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Watu wengi hawajui kuwa nyaraka nyingi hao wanasheria hutumia templates tu. Ni kiasi cha kubadili badili vitu vichache tu kama tarehe, majina, na kadhalika. Laiti watu wangejua wala wasingekuwa wanaingia gharama ambazo hata si za lazima....
   
 6. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  mkuu contract yoyote sio mpaka aiandike mwanasheri au hata iwe na stamp ya mwanasheria

  wewe andika tu

  leo tarehe _____________________ ninafunga mkataba baina ya _________________________(mwenye nyumba) na _______________________ mpangaji


  Pande zote zinakubaliana yafuatayo:-

  Kwamba
  a)
  b)
  c).....

  (hapo unaongelea terms na condition mfano kodi itakuwa ngapi, kama mpangaji atalipia maji na umeme, muda wa kutoa notice kama anataka kuvunja mkataba, muda wa kutoa kama anataka kuendelea na mkataba, kalipa kiasi gani na kodi ni kiasi gani kwa mwezi na mwaka.., elezea kama haruhusiwi kupangisha wengine, elezea kama haruhusiwi kufanya biashara yoyote, elezea kama matengenezo yatahitajika ni nani atagharamikia... n.k. (yaani elezea yote yale unayotaka kulingana na nyumba yako, hata kama hutaki mifugo unaweza kuweka hapo), pia elezea kama mpangaji atatakiwa kulipa pango lote kwa mwaka au kwa installments.


  Mkataba huu umesainiwa leo tarehe___________________________ na wafuatao:-  hapo chini weka sehemu za majina ya mwenye nyumba na mpangaji na sehemu za kuweka sahihi pia weka sehemu za mashahidi wawili au wanne wawili wa mwenye nyumba na wawili wa mpangaji au mmoja mmoja kwa kila upande
   
Loading...