Natafuta kiwanja Mbezi beach.

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,792
1,834
Magomeni hapajanichosha, ila kubadili mazingira si vibaya.

Natafuta kiwanja Mbezi Beach.

Gharama ya kiwanja 5 milioni TZsh, tunaweza kuzungumza vile vile.

Ukubwa wa kiwanja si ajenda kubwa.

Ni wale watu makini katika swala hili tu ndio waje na maoni yao.

Asanteni.
 
Zawadi kwa bei hiyo sijui una maana gani unaposema mazungumzo yapo na ukubwa wa kiwanja si agenda. Kwa hiyo mazungumzo hayo yanaweza kwenda mpaka 23m - 40m?
 
Nadhani usiogope kwenda bunju ,mpiji,kerege au mapinga.kwa hela hiyo utapata kikubwa tu.Usiogope umbali jiji la Dar linakua kila siku.Nasikia hata Sinza zamani ilikuwa msitu na watu walikuwa wanakataa viwanja,lakni cheki sasa palivo expensive.
 
Magomeni hapajanichosha, ila kubadili mazingira si vibaya.

Natafuta kiwanja Mbezi Beach.

Gharama ya kiwanja 5 milioni TZsh, tunaweza kuzungumza vile vile.

Ukubwa wa kiwanja si ajenda kubwa.

Ni wale watu makini katika swala hili tu ndio waje na maoni yao.

Asanteni.

Kwa pesa hizo unaweza kupata kiwanja Magomeni ulipopachoka au Tandale?
Mara ya mwisho kusikia viwanja vya 5M Tz shs Mbezi Beach ilikuwa late 1980s na mwanzoni mwa 1990s
 
ahahahahahahaa...mkuu nahisi umesahau kuongezea sifuri (0) nyuma ya hiyo milion 5 uliyoandika.....naamini ukifanya hivyo utakuwa kweli na kwania ya dhati unataka kubadili ukaazi wako kwa jiji la dsm...zaidi ya hapo naona uanataka kuelekea jiji la pwani maeneo ya bagamoyo au hata kibaha.....tafakari chukua hatuaaaa
 
Kwa pesa hizo unaweza kupata kiwanja Magomeni ulipopachoka au Tandale?
Mara ya mwisho kusikia viwanja vya 5M Tz shs Mbezi Beach ilikuwa late 1980s na mwanzoni mwa 1990s
Jamani si utani, hebu niambieni wastani wa bei za viwanja huko Mbezi Beach.

Yawezekana kuwa ni kweli nimepitwa na wakati, lakini si vibaya mkinitajia bei za wakati huu. Tafadhali tajeni bei makini ili nijue nijiandae vipi.

Kikubwa ni nia mengine yanaweza fanyika. Nia ninayo, uwezo utatafutwa kwani silaha hazikosekani. Hii ni biashara.
 
Du ndugu yangu. Uko Dar es Salaam au wapi?? Mbezi Beach kiwanja kwa 5m?? Ukipata cha hivyo ujue dalali amekuingiza mjini, kina mgorogoro. Hata cha mgogoro hutapata kwa bie hiyo maana madalali fake wanajua wakisema bei ndogo utashtukia dili. Mbezi kianja kitupu ni 30-50 million kulingana na density. Kama walivyokwisha shauri wengine labda kwa hela hiyo sogea Bunju kwenye viwanja vya kupima kwa miguu na ni high density??
 
Nadhani usiogope kwenda bunju ,mpiji,kerege au mapinga.kwa hela hiyo utapata kikubwa tu.Usiogope umbali jiji la Dar linakua kila siku.Nasikia hata Sinza zamani ilikuwa msitu na watu walikuwa wanakataa viwanja,lakni cheki sasa palivo expensive.

Milioni 5 kiwanja kikubwa Bunju? You can't be serious. Mbezi Beach kama huna above 25m wala usijisumbue!
 
usiwe na wasiwasi hata laki tano unapata contact me i can assist to have a urge plot
 
Mbezi beach kama unataka kiwanja chenye eneo la kutosha ni kuanzia milioni 40- 60, ukiwa na hizi pesa utakuwa kweli na uhakika wa kupata kiwanja cha maana.
 
kama uko sirias na vya million 50 karibu uwe jirani yangu
kuna jamaa anataka kutema kikubwa pembeni yangu million 50 sichukui hata senti yako mnamalizana
Bwana awe nawe
 
Milioni 5 kiwanja kikubwa Bunju? You can't be serious. Mbezi Beach kama huna above 25m wala usijisumbue!
Nawashukuru nyote kwa maoni, ushauri na mapendekezo yenu.

Kwa muhtasari kutokana na maoni yenu, nimeelewa kuwa viwanja huko viko kwenye wastani wa 20-30M.

Ni habari za kushtusha lakini hizo ndio athari za utandawazi. Kweli UJAMAA umekufa kimya kimya.

Nazitafuta zikipatikana nitarejea ulingoni. Bado sijakata tamaa. Treni limeshaondoka na halina breki, lazima tulidandie.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom