Natafuta kazi

Gota8s

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
203
189
Siku imekaa vema,
Afya yangu pia ni njema.
Vipi kwa upande wako?

Basi Wakuu bila kuwachosha, kichwa cha habari kinahusika moja kwa moja. Mimi ni kijana mhitimu wa chuo kikuu mwaka huu, nimesoma degree ya Sanaa na Elimu. Masomo ya Lugha. Nimekuja hapa jukwaani kuwaomba iwapo kuna yeyote mwenye connection inayoweza kunifanikishia hitaji langu nitamshukuru sana. Kazi ninayoitafuta si lazina niliyosomea tu. Hata mgahawani sawa tu. Stationery, dukani, sokoni, shuleni, au hata kiwandani.

Ninahitaji kazi japo niweze kupata chochote kitu kwani, mimi ni kijana ninayejipigania tangu mwaka 2013 nilipopoteza wazazi wangu. Nimekuwa nikisoma kwa udhamini wa halmashauri mbalimbali kitengo cha ustawi wa jamii na pia chuo kikuu nikafanikiwa kumaliza masomo chini ya udhamini wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB). Kufikia wakati huu naishi nikitafuta kibarua, au hata kazi ya muda ili nipate riziki inshaalaah.

Mimi ni kijana mwaminifu, mpole na mwenye hofu ya Mungu. Sio mwizi wala tamaa sio kariba yangu. Naombeni tafadhali ikiwa kuna mwenye tetesi za wapi naweza kupata hitaji hili anisaidie, nae atabarikiwa.

Nashukuru sana kwa muda wenu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom