Natafuta kazi ya ujenzi, nina shahada ya Architecture and Construction Management

May 3, 2019
18
15
Kwanza kabisa nitumie fursa hii kuwasalimia WanaJF wote mlio humu ndani kwa mchango wenu mkubwa wa kuwa chachu ya maendeleo ya Taifa hili la Tanzania kupitia teknolojia hii ya Habari na Mawasiliano.

A. Utambulisho
Mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka ishirini na nane (28) ambaye kwa sasa ninaishi katika Mkoa wa Dar es Salaam.

B. Elimu/ Ujuzi/ Uzoefu
Elimu yangu ni Bachelor Degree of Science in Architecture and Construction Management.

Nina ujuzi wa kuandaa, kupanga na kusimamia budget ya miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba za makazi kuanzia level ya nyumba zisizo za ghorofa (Zero storey buildings) mpaka zile za ghorofa (Multi-storey buildings).

Vilevile nina uzoefu usiopungua miaka minne (04) katika kusimamia utekelezaji wa miradi hii kuanzia ngazi za awali kabisa kama vile kuandaa michoro au ramani za ujenzi na uandaaji wa vibali vya ujenzi (Pre Construction Phase), kupanga mikakati mahususi ya kutekeleza mradi husika na kuanza ujenzi wenyewe (Construction Phase) na mwisho kabisa ni kukabidhi mradi kwa mteja husika pamoja na vibali vya kuanza kutumia jengo au nyumba (Post Construction Phase).

C. Lengo Kuu
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza hapo juu, natafuta kazi ya ujenzi nikilenga moja kwa moja tasnia ya ujenzi (Architecture and Construction Management) kulingana na taaluma tajwa hapo juu. Kwa ufafanuzi zaidi, ningependa kufanya kazi na mtu au kampuni binafsi ambaye/ambayo atanihitaji/itanihitaji kwa sasa au hapo baadae.

Aidha taarifa zangu binafsi ambazo haziko katika chapisho hili naweza kuziweka wazi kwa wale wote wenye lengo la kufanya kazi na mimi (Interested part).

D. Jitihada Binafsi
Ukiachilia mbali shughuli ndogondogo za kiujasiriamali ambazo nimekuwa nikizifanya kama vile kufundisha vijana wa vyuo program za kuchora ramani za majengo nimejaribu kuomba kazi kwenye makampuni/mashirika binafsi na ya kiserikali kama vile NHC, TBA, ESTIM Construction na kadhalika lakini kikubwa nilichokipata ni uzoefu tuu na malipo kidogo ambayo hata kwa kujikimu binafsi yalikuwa hayatoshi.

Kwa kuzingatia gharama za kuishi Mkoa wa Dar es Salaam zinavyopanda siku hadi siku nikaona si mbaya kuwashirikisha ndugu zangu WanaJF katika suala hili.

E. Mwisho
Mwisho kabisa napenda kuwashukuru WanaJF wote kwa mchango wenu mkubwa katika kusaidia na kuibua karama mbalimbali zilizomo ndani na nje ya jamii ya Watanzania kwa ujumla kupitia tovuti hii.

Pia napenda kukaribisha maswali, mawazo, maoni, mapendekezo, ushauri na mitazamo mbalimbali kutoka kwa WanaJF ikiwa inalenga kunijenga mimi moja kwa moja au wadau wengine wa Jamii Forum.

Karibuni sana……..

“Anyone can count the seeds in an apple, but only God can count the number of apples in a seed”

– Robert H. Schuller.
 
Mungu atakusaidia utapata maana ata mimi pia nipo kwenye ombwe ilo, nimesoma IT
 
Jaribu kuconnect nao insta,Facebook. wale jamaa walianza from scratch walimaliza ardhi 2015,Ninavyowaona mpaka saizi kampuni yao ilipofikia wana client base ya kutosha,hawabangaizi.

Usiniite boss mkuu.
 
uwezo wa kumjua mtu mwenye asili ya kibri ni conclussion yake

vijana ,kampuni , taasisi mbalimbali kijana mwenzetu huyo "yupo very good hata maelezo yake"
 
uwezo wa kumjua mtu mwenye asili ya kibri ni conclussion yake

vijana ,kampuni , taasisi mbalimbali kijana mwenzetu huyo "yupo very good hata maelezo yake"
Hata mm nimemkubali jamaa yuko very smart, systematic,discplined.
Vijana Kama hawa ndio wanatakiwa katika jamii sio wale jeuri wanyoa viduku.
 
Nenda site yotote anza kujenga, wakikukamata wakakupeleka kituoni , ukifika huko nako anza kujenga. Watakuelewa tu
 
Nawashukuru sana WanaJF wote mliotumia muda wenu kupitia chapisho langu.
Pia niwashukuru kwa michango mliyoitoa katika chapisho hili huku ahadi yangu ikiwa ni kuwaletea mrejesho wa yote haya mliyoyachangia.
Mzidi kuishi katika amani na upendo, nawatakieni siku njema na kazi njema.
Ahsanteni....
 
Nawashukuru sana WanaJF wote mliotumia muda wenu kupitia chapisho langu.
Pia niwashukuru kwa michango mliyoitoa katika chapisho hili huku ahadi yangu ikiwa ni kuwaletea mrejesho wa yote haya mliyoyachangia.
Mzidi kuishi katika amani na upendo, nawatakieni siku njema na kazi njema.
Ahsanteni....
Kila la kheri mkuu, kingine kuhusu Estim kazi watu hua wanapata on site usiende ofisini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom