Natafuta kazi ya afisa masoko ama usimamizi wa biashara

Master Kutu

Member
Jun 8, 2021
77
174
Habari ya leo wakuu,
Mimi ni kijana wa kiume,
umri wangu miaka 29 .
Nna mke na mtoto 1,
Naishi Dar Es Salaam
Elimu yangu kidato cha nne
Nimejitokeza hapa kuomba kazi ya sales and marketing ama usimamizi wa biashara na masoko.

UZOEFU WANGU
Mwaka 2013 nilianza kazi ya kusajili laini kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo ambayo nili fanya mpaka mwaka 2015 mwezi wa 9 pia nikiwa na kampuni hiyo nili patiwa mafunzo ya mauzo yaliyo kuwa yakitolewa kwa kila freelancer wa Tigo yaliyo itwa Tigo Sales School.

Mwaka 2015 October 15 nili pata nafasi ya Team Leader Katika kampuni ya Vietel Tanzania Limited ya mtandao wa simu wa Halotel ambayo nili fanikiwa Kutengeneza team imara ya mauzo iliyo kuwa miongoni mwa team bora za mauzo
Nili fanya kazi hiyo mpaka mwaka 2018 November 22

Mwaka 2019 nili pata kazi ya usimamizi wa tawi la duka la kampuni ya vinywaji aina zote.
Majukumu yangu katika kazi hiyo yalikuwa ni,

1. Kusimamia oda za wateja na kuhakikiSha zina wafakia maaana tulikuwa tuna fanya free delivery maeneo yote ya karibu.
2. Kusimamia malipo ya kila oda na ku record jina la mteja, number yake ya simu na sehemu anako tokea ili siku zinazo fata tumpigie simu na kumpelekea mzigo mpaka sehemu yake ya biashara lengo likiwa ni kudumisha mahusiano mazuri na wateja ili kukuja mauzo.

3. Kutunza kumbukumbu zote za wateja kwa vinywaji walivyo chukua na malipo yaliyo fanywa kila siku ili kuepusha lawama za wateja maana wapo baadhi ya wateja anaweza sema kitu flani haja chukua na kumbe ame pewa inakuwa hasara kwako wewe manager.

4. Kutoa oda za vinywaji toka kwa wasambazaji wa Viwandani siku 1 kabla kuzuia kukosekana kwa vinywaji maana itakuwa tatizo kwa wateja wanao hitaji na ili kuepusha mteja kuhama nahakikisha vinywaji vyote vipo store.
Maana samaki ili umpate muwekee anacho hitaji hivyo hata wateja ni muhimu kuwa wekea bidhaa zote ili kuwa nao karibu kila siku.

5. Kufunga Hesabu Ya kila Siku
Nilikuwa nafanya hesabu ya kila Siku katika sheet ya tarehe husika ili kupata hesabu ya siku husika.
A. Kuingiza vinywaji vilivyo ongezwa kwa siku hiyo na kuweka jumla yake na vilivyo baki jana.
B. Kuhesabu vinywaji vilivyopo baada ya mauzo jioni
C. Jumla ya vinywaji vilivyo ongezwa na vilivyo baki jani toa idadi ya vinywaji vilivyo baki leo baada ya mauzo ili kupata ni kiasi gani vinywaji vime uzwa na thamani yake.
D. Kupata jumla kuu ya pesa baada ya hesabu ili kujua ni kiasi gani kinatakiwa kuwepo baada ya mauzo kisha nalinganisha na cash niliyo nayo mkononi ni sawa na inayo takiwa kuwepo kwenye sheet ama la,ikiwa cash ina pungua napiga hesabu ya matumizi ya siku husika kisha na andika Katika sheet ili kumpelekea Mkurugenzi kila siku na yeye ana pitia sheet ya jana na leo kubaini kama kuna udanganyifu.

Ujuzi mwingine nilio nao ni kufanya matangazo ya biashara kwa njia ya mtandao (Social Media Marketing) Facebook, Instagram na WhatsApp ambao ni zaidi ya ule wa kutangaza matangazo ya biashara yako tu nna mbinu za kutangaza bidhaa au huduma itakayo mfanya mteja aje mwenyewe kwa kutangaza suluhisho la huduma au bidhaa yangu inayo tatua changamoto aliyo nayo mteja.
Ikiwa ntaweza kukufaa unaweza kuni tafuta kwa number yangu 0684601370.

Asante sana 🙏🙏🙏
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom