Natafuta kazi, nimesomea IT nina uzoefu wa masuala ya Sales

Ndugu zangu nimekuwa msomaji wa mada mbalimbali humu jukwaani muda mrefu na nimeona nijiunge rasmi ili niweze kuchangia nilichonacho. Lakini pia nina moja la kuwashirikisha naamini nitapata msaada.

Nilikuwa na kibarua fulani kwenye kampuni moja ya wakenya kule mikocheni lakini bahati mbaya mambo ya kodi hayakuwaendea vizuri na pia biashara kwa TZ hazikuwa poa wakaona warudi nchini Kenya, nikakaa mtaani kwa muda wa miezi kadhaa nikaja kupata sehemu nyingine ya muda, sasa juzi kati wakasema hawawezi kuendelea na mimi kwani muda wa kufanya kama temporary umeisha(nimekaa zaidi ya miezi 6) na hawapo katika position ya kuajiri officially kwa sasa(hawana budget) hivyo nisubiri waweke mambo sawa internally then watanijulisha kama kuna lolote.

Ninapokaa kodi inaisha mwezi huu mwishoni na kwa kweli sijui itakuwaje, kiasi nilichokuwa nacho kidogo kiliishia kwenye matibabu ya mzazi wangu pekee(mama) na pia mimi kuna kipindi niliumwa.

Naombeni msaada(sio wa pesa) wa kibarua chochote at least niweze kusukuma siku mbili tatu mbele nikisubiri majibu ya huku ninapoapply kila siku au kule nilipokuwa kama mambo yakiwa mazuri. Nimesoma mambo ya IT(bachelor's degree) lakini pia nimewahi kufanya kama sales.

Mwenye duka, stationary, bucha, au ofisi yoyote anisaidie. NIPO TAYARI KUFANYA KAZI KWA BIDII ILI KUFANIKISHA MALENGO YA BIASHARA YAKO NA MALENGO YANGU PIA, Naishi Kigamboni, akipatikana mtu wa huku wa kunishika mkono nitashukuru sana.

Kwa mlio maofisini kama unaona wanahitaji mtu wa IT naomba nijulishe ili nitume CV haraka.
Akiba niliyonayo sijui hata kama next week itafika, ila naamini Mungu atasaidia.

Nawashukuru sana na Mungu awabariki,mnisamehe kama uandishi utakuwa na makosa napitia kipindi kigumu.
Nipigie 0712359510
 
bado unahitaji kazi?
Nitumie CV yako au tuwasiliane 0717157640
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom