Natafuta kazi mimi ni mwalimu wa shule za msingi kiwango cha elimu diploma ya 4.6 gpa

Creah

Member
Apr 6, 2018
75
79
Mimi ni mwalimu ambae sina kazi, hivyo kwa yeyote mwenye mchongo wa shule au center na anauhitaji wa mwalimu tuwasiliane. Nina diploma ya elimu ya msingi na nimebobea kwenye masomo ya HISABATI NA SAYANSI. Nipo teyali kufanya kazi mkoa wowote Tz ,na nikijana wa miaka 25 na sijaoa. kwa sasa nipo DODOMA
No. 0659103997
Email mgogotv69@gmail.com
 
wapi nilipoandika kihuni kuwa mwazi
Nimeshakwambia jifunze kwanza kuandika lakini up to this point umeendelea kuharibu. Mwazi maana yake nini? Kama kuandika kwenyewe hujui, je hao watoto utawafundisha nini kama siyo ujinga?
Kwa uandishi wako hufai hata kidogo kuwa mwl hata kama ni kwa level ya kindergarten bali unapaswa kuwepo darasani ufundishwe mwandiko na namna ya kupangilia hoja zako
 
Mimi ni mwalimu ambae sina kazi, hivyo kwa yeyote mwenye mchongo wa shule au center na anauhitaji wa mwalimu tuwasiliane. Nina diploma ya elimu ya msingi na nimebobea kwenye masomo ya HISABATI NA SAYANSI. Nipo teyali kufanya kazi mkoa wowote Tz ,na nikijana wa miaka 25 na sijaoa. kwa sasa nipo DODOMA
No. 0659103997
Email mgogotv69@gmail.com
Jaribu kufungua shule yako, ya msingi
 
Mwalimu gani wewe unaandika kihuni huni. Jifunze mwandiko kwanza
Kama mtu huna la kumsaidia ni bora ukakaa kimya, maana huwezijua mwenzako anapitia wakati gani mpaka kufikia kuandika shida yake humu ndani....
Pia mkuu kwa ushauri wenye kujenga ulitakiwa kumsitiri mtu kwa kumfuata inbox na sio hivi....
Tusaidiane kupunguziana stress

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye mwenyewe ana stress unazani atamsaidia nini mwenzie zaidi ya kumuongezea stress tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuwa active na website za ajira kule uhakika wa ajira ni mkubwa, hapa JF wadau wamekuwa wa kukatishana tamaa tu....Goodlucky
 
4.6 GPA, Hivi ndiyo first class?

Ukweli usemwe uandishi wake unatia shaka na gpa yake hiyo.
 
Kama mtu huna la kumsaidia ni bora ukakaa kimya, maana huwezijua mwenzako anapitia wakati gani mpaka kufikia kuandika shida yake humu ndani....
Pia mkuu kwa ushauri wenye kujenga ulitakiwa kumsitiri mtu kwa kumfuata inbox na sio hivi....
Tusaidiane kupunguziana stress

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati mwingine maumivu yanaweza mkomboa mtu.Kama sio wa kukombolewa hata akifuatwa PM bado hatasaidika.Nafikri ni muhimu kwa mleta mada kufanyia kazi ushauri wa mchangiaji mintarafu ujengaji wa hoja.JF ni mahali pa kujifunza na kukosolewa ni sehemu ya burudani.na kuongezeana maarifa.Kama hataki kukosolewa basi asiandike.Mleta Mada Ongeza bidii katika kujieleza kwani wewe ndo mwenye shida.Unatakiwa uoneshe kwamba una cha kipekee katika maelezo yako.GPA ya 4.6 halafu hujajieleza vizuri inazidi kushusha heshima yako.Unapoomba kazi ya ualimu unatakiwa ni nini ulicho nacho cha kipekee ambacho kitamfanya mtu akuajiri wewe na sio mtu mwingine.Nini unafanya kwa wakati huu,umewahi kufundisha wapi,umehitima mwaka gani,na taarifa nyingi uwezavyo ili mtu aone kwamba unastahili
 
4.6 GPA, Hivi ndiyo first class?

Ukweli usemwe uandishi wake unatia shaka na gpa yake hiyo.
Mkuu wala usitishike na gpa yake ya 4.6 hawa ni wale waliosomea diploma ya elimu ya awali(DECE) kwenye matokeo yao mtu aliyefeli ana gpa ya 4 point something Lakini kile kilichomo vichwani mwao hakiakisi kabisa uhalisia wa gpa walizopata
 
Back
Top Bottom