Natafuta kazi katika Sekta ya Kilimo na Uvuvi

Feb 15, 2021
72
81
Habari zenu ndugu,

Mimi ni Kijana wa kiume umri miaka 24 na mhitimu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) katika shahada ya Sayansi Aqua na Uvuvi (Bachelor of science in Aquatic sciences and fisheries).

Naishi Ubungo Dar es salaam kwa sasa. Ninatafuta kazi katika Rekta resmi na isiyo rasmi, Serikalini au penginepo nchini inayohusiana na fani yangu au isiyohusiana kabisa na fani yangu.

Akili yangu ni adaptive, ntakuwa tayari kujifunza kitu kipya katika fani nyingine ambayo sjasomea. Uzoefu nlionao ni pamoja na kufundisha masomo ya Sayansi hasa Physics, Chemistry na Biology kw O level na A level. Pia nmekuwa muuzaji katika kampuni ndogo huko Mwanza hivyo naweza fiti kwenye sales.

Nina uzoefu mkubwa wa matumizi ya Computer application kama vile Microsoft Excel. Word, Acess na Powerpoint. Pia Statistical knowledge ya SPSS na ANOVA naijua kiasi.

Uzoefu katika taaluma yangu ni pamoja na ufugaji samaki, uzalishaji wa vifaranga na usafisishaji wa brooders, utayarishaji na usafishaji wa mabwawa na Artifitial propagation ya kambale na sato.

Utayari na Ushirikiano na wengine wenye uzoefu zaidi nauahidi kuutoa ili kufikia malengo husika. Kwa yeyote mwenyeconnection au kwa namna moja ama nyingine anaweza nipatia kazi nitashukuru akinisaidia.

Namba yangu ni 0757942975 na 0656208659.

Ahsanteni sana.
 
Napenda watu ambao hawachagui kazi.

Ushauri: weka kipengele cha kukaribisha mtu/watu wenye interest ya kuwekeza kwenye samaki muungane na kuanzisha/kuendeleza mradi wa pamoja halafu mnagawana faida.

Wapo wanaohitaji kuwekeza kwenye ufugaji wa samaki lakini hawana fedha ya kulipia utaalamu kila mwezi au mshahara (kawaida kwa biashara inayoanza from ground)
 
Napenda watu ambao hawachagui kazi.

Ushauri: weka kipengele cha kukaribisha mtu/watu wenye interest ya kuwekeza kwenye samaki muungane na kuanzisha/kuendeleza mradi wa pamoja halafu mnagawana faida.

Wapo wanaohitaji kuwekeza kwenye ufugaji wa samaki lakini hawana fedha ya kulipia utaalamu kila mwezi au mshahara (kawaida kwa biashara inayoanza from ground)
Nashukuru sana ndugu yangu kwa ushauri wako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom