Natafuta dawa za asili za kutibu wasiwasi

Wala ha uhitaji dawa...ni tatizo tu la kawaida sana kwa wanadamu kulingana na changamoto mbali mbali anakabiliana nazo!!!!.....

Mimi nilikabiliana na tatizo hilo kwa kusafiri sehemu ambayo sijawahi hata kufika na nilikaa huko kwa muda wa wiki mbili....ule upya wa mazingira na watu....ukaifanya akili yangu kuwa mpya na yenye mawazo mapya!!......

Jambo lingine la msingi

Don’t take people and things too seriously!!!.....

Lower your expectations towards people and things!!!......

Usipende kuweka vitu moyoni huko ni kujibebesha mzigo mzito.....ongea na watu kuhusu matatizo yako...bila kujali watakuchukuliaje kwani kati yao utapata mfariji wako.....
 
Tujuze kwanza chanzo cha huo wasiwasi ni nini hasa. Huwezi tatua tatizo bila kujua chanzo chake

yaani nakua na too much worries kupitiliza, pia woga wa judgement za watu. nadhani stress kupita kiasi ndo ilisababisha, sasa nimeshaathirika kisaikolojia mawazo yangu yamekua negative
 
Nimeona umeanzisha thread nyingi zinazofana na hii.

Nakumbuka ulileta thread hapa unatafuta tiba ya depression na wadau walijaribu kukushauri kadiri ya upeo wao.

Swali kwako. Je, ulifanyia kazi ushauri uliotolewa?

Kwauzoefu wangu watu wanaopitia matatizo ya msongo wa mawazo huwa wanashindwa kufuata ushauri wanaopewa kwa makini.

Anajaribu hili siku chache asipoona matokea anarukia jambo jingine. Na inakuwa hivyo siku zote.

Nimesoma baadhi ya thread zako na nimegundua kitu.

Wewe huna chanzo kizuri cha kukuingizia mapato na hiyo inasumbua akili yako kupelekea over thinking.

Tiba muhimu kwako si ganja au aina yoyote ya pills.

Jitahidi kutafuta kazi uwe na kipato.

Pia kama huna mwenza tafuta itasaidia kupunguza mawazo.

Mahusiano ni muhimu hasa kwa watu wanaopitia hali kama yako.
 
Back
Top Bottom