Natafuta connection kupata nafasi hii

Rosicky

JF-Expert Member
Sep 21, 2015
1,157
1,943
Peace and Love be upon you.

Nakuja mbele zenu nikiwa kama muhanga wa ajira za Tanzania hii baada ya kumaliza chuo na kusota mtaani with huge frustration. Nishaaply over 300+ job application lakini katika hizo moja tu ndo nilifanikiwa kuitwa interview nayo nilikosa, katika kupambana na maisha niliazisha biashara nazo zilikuja kufeli kwa sababu mbalimbali. (Wateja wetu tunawaitaji ila punguzeni kukopa mnaua biashara zetu ndogondogo)

Baada ya kusema hayo ni wazi kuwa soko la Ajira limetawaliwa na kujuana hilo nimeshindwa kulikwepa ndo maana niko hapa kuomba yoyote anayeweza kunisaidia nikapata kazi/nafasi katika shirika la IHI ambalo limetoa nafasi za ASSISTANT FIELD OFFICER au kadharika mashirika mengine nitashukuru sana.

Maisha ya kuishi bila kazi ya kueleweka ni mabaya sana sanaa na omba sana Mungu atupatie rehema na neema katika hali zote za maisha yetu. Inaumiza sana Yanatesa sana na Yanasononesha mno.Naamini hili wazo langu limekuja hapa kwa msukumo wa Mungu nikiwa na imani Kubwa kuwa yupo mtu humu anaweza kunipa msaada huo niliyouomba, usisite please hii sio bahati mbaya ni mpango wa Mungu.

N.B Ombi kwa ndugu zangu wanaosubiri kuwasaidia ndugu zao na watu wanaofahamu tu,mnakosea sana jitahidi msaidie hata yule usiyemfahamu provided anahitaji na una uwezo wa kumsaidia. Msaada wako mdogo tu unaweza okoa future ya unayemsaidia.
Someone to pull me out of this hell... please

Asanteni
" Leo nimekosa ila naamini Kesho yangu ni nzuri".​


Screenshot_20210622-121935_Adobe%20Fill%20%26%20Sign.jpg
 
Yaani kuishi maisha ya hujui kesho yako unaamkia wapi na utapata wapi riziki ya kila siku ni mateso sana asikwambie mtu.
Sonona ni nyingi mno
Nimechoka kaka kuna wakati napata mawazo ya kukata tamaa
 
Back
Top Bottom