Natafuta business partners kwenye biashara ya Magari

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,128
8,648
Habari,
Leo ningependa kwenda moja kwa moja kwenye mada ni kwamba unapotaka kufikia mafanikio basi fanya kazi kwa bidii lakini kama ukitaka mafanikio makubwa zaidi basi inakupasa kushirikiana na wengine na kufanya kazi kama team.
Mimi ki upande wangu ninajihusisha na uuzaji wa magari used ambayo yametumika ndani ya Tanzania,Biashara hii kiukweli inasaidia kupata chochote kitu na inafanywa na wengi lakini wengi wanaifanya locally kiasi kinachopelekea wengi tupate hela ya kula tu wakati ikifanywa ki utaalam inaweza kuingiza kipata kizuri kwani uhitaji ni mkubwa na wanaohitaji ni wengi

Team ninayoitaka
1.Vijana wawili wenye uwezo wa masuala ya IT hasa websites/na graphics kwa ajili ya uandaaji na shughuli za IT

2,vijana wawili ambao watakuwa kwenye upande wa marketing hawa watakuwa wanahusika zaidi.

NB: Siangalii jinsia au umri wa mtu bali ninachoangalia ni uaminifu sababu ndo silaha ya biashara hii pia commitment ya kazi.

MALENGO YA TEAM
Malengo makubwa ya kutaka kuundwa kwa Team hii ni kuhakikisha kuwa tunakuwa tunafungua ofisi na kampuni ambayo itakuwa inauza magari yenye ubora yaliyotumika Tanzania pia iwe ni kampuni ambayo itaongoza kwenye uuzaji wa magari hata kutoka nje.

Malengo ya awali
Kufungua blog
kufungua application
kufungua ofisi
kujisajili
kujitangaza

Pia unaweza kuwa umelipenda wazo langu na una uwezo wa kuwekeza fedha yako kwa mkataba maalum tunaweza kuonana na nikafanya kazi chini yako,huku kampuni ikiwa chini yako kulingana na mkataba tutaokubaliana kumbuka mpka sasa hakuna kampuni hata moja inayohusika na uuzaji wa magari used ndani ya Tanzania japo kuna demand kubwa sana ya magari used.

kwa maswali unaweza kuniuliza na kwa wale watakaopenda kuungana nami ili tuwe partners mna karibishwa pm kwa kujieleza unafit vip kama ukichaguliwa
cha mwisho kwa wale wataokuwa tayari ni kwamba tutachangia gharama sawa na kuwa na profit share sawa

karibuni
 
IMG_1486.JPG

upatikanaji wa magari kwa ajili ya uuzaji ni wa uhakika kwani tutakuwa na group zaidi ya 140 za magari za whatsapp pia zipo nyingne kwenye social media nyingne hivyo mteja hawezi kukosa bidhaa ya gari anayoitaka
 
Wazo zuri sana,nakupa pongezi:-
  • Ningekushauri utumie njia ya shea au hisa,mfano labda unahitaji milioni 50
  • unaweza ukaigawa kwa 10,000 ukawa na shea 5000
  • Kila shea 1 unaiuza 10,000,atakayeweza kuchukua 100, 500 n.k wachukue
  • Ugawaji wa faida uwe katika utaratibu unaoeleweka
  • Sajili kampuni yako,huku ukiwa na website/blog n.k
  • Fungua akaunti ya kampuni
  • Ikiwezekana kuwa na mwanasheria/wakukodi
 
nashukuru kwa ushauri wako but nmefanya hivi sababu ninataka kuwa na watu ambao tutaanza from scratch nafanya hivi sababu najua baada ya kusajili kama kampuni kila partner atakuwa na displine ya kazi sababu atakuwa na uchungu na kampuni
Pia kwenye mtaji wale haiwezi kufika gharama zote hizo gharama za the whole project zitakuwa ndogo lakini zenye kuleta faida kubwa sana ndo maana nkasema naomba wenye nidhamu na commitment
 
Kwa sasa, huyo partner anatakiwa awe na kiasi gani?
 
na pia unaweza kuwekeza huku ukifanya shughuli zako nyingine lakini kwenye share kidogo hautakuwa sawa na wale ambao wataparticipate kwa 100%
 
kwa sasa haitazidi laki 5 na fedha hyo inaweza kurudi ndani hata ya week2 kutokana na strategy tutazikuwa nazo(goals)
Ofisi inakuwa iko mkoa gani?kwa sababu wengine pia kutokana na majukumu mengine ushiriki wetu unaweza kuwa nusu
 
ofisi itakuwa dar,pia hta wa mkoani anaweza kuwa partner cha muhimu ni makubaliano tu tutayoingia ya kisheria,kwa maana unaweza kuwa na kazi yako but mwisho wa siku inavuna na huku kama mwanachama
 
Ofisi inakuwa iko mkoa gani?kwa sababu wengine pia kutokana na majukumu mengine ushiriki wetu unaweza kuwa nusu

kwa maana leo unaweza kuchangia laki tano kwa mfano kama start up capital but na ukawa unapata labda faida ya laki 5 mpka 1m kwa mfano but after 6 au 7 months ukawa unaingiza mpka 10m per month kulingana na profit unayoiweka inshort ni kama uwekezaji unaoendelea kwa maana ya hela yako inajizalisha na kuendelea kupata faida miaka yote
 
Marketing nipo hapa...ngoja niendelee kusoma nielewe kwanza kihusu hilo
 
watu wa IT ambao nimewaomba wao watasaidia hasa kwenye masuala mazima ya kuengeneza matangazo na hata apps za ofisi pia kwa wale wa marketing wao watakuwa wanakazi ya kuhakikisha kuwa ofisi inatambulika kila mahali ndani ya Tanzania pia kutafuta order za wateja.
Mfano kusambaza vipeperusha/banners kwenye ofisi tofauti tofauti na hata kutangaza ofisi sehemu mbali mbali online na hata physical.
 
Nina uhakika itakuwa ni ofisi ya kwanza na kampuni ya kwanza Tanzania ambayo itakuwa inahusika na uuzaji wa magari used ndani ya Tanzania,kwani hakuna kampuni inayojihusisha na kazi hii hivyo uwezo wa kukuua ni mkubwa na connection ya upatikanaji wa wateja na magari upo mkubwa
 
Hayo magari muuzaji atakuwa analeta ofisini nyie ndio mna uza au mtakuwa mnachukua magari haya ambayo yanamadalali tayari na yako mitandaoni?

Mtawezaje kumuunganisha mteja aliye Mtwara na gari ipo Kigoma ili aweze kununua? Fafanua

Nitarudi kwa maswali ya nyongeza!
 
Sawa naitaji kagari aaina ya kiriku kichwa kikubwaa naweza pata used plate kuanzi c na kuendeleaa ..
 
Hayo magari muuzaji atakuwa analeta ofisini nyie ndio mna uza au mtakuwa mnachukua magari haya ambayo yanamadalali tayari na yako mitandaoni?

Mtawezaje kumuunganisha mteja aliye Mtwara na gari ipo Kigoma ili aweze kununua? Fafanua

Nitarudi kwa maswali ya nyongeza!

upo mfumo maalum wa kupata magari direct kutoka kwa wamiliki i hope mfumo huo utakuwa unatumika na marketing officers wetu.
Pili gari itakayouzwa nasi inaweza kukaa ofisini na hata kwa mwenyewe kulingana na mkataba tutaoingia nae pia gari kabla ya kuiweka sokoni sisi kama sisi tutaikagua na kuiweka verified label kwa maana ya gari nzima na ilokidhi vigezo sera yetu inatukataza kuuza gari mbovu ili kukenga soko,hii itatusaidia kwenye utekaji wa soko na kukubalika zaidi
 
mpka sasa hakuna kampuni hata moja inayohusika na uuzaji wa magari used ndani ya Tanzania japo kuna demand kubwa sana ya magari used.
Nieleweshe, unamaanisha hapa Tanzania zile show room tuzionazo haziuzi gari ama ni mpya na sio used?
 
Back
Top Bottom