Natafakari sana kwanini Uncle Kijo yupo makini lakini hana bahati

Babumawe

JF-Expert Member
Sep 12, 2014
2,540
2,000
Habarini,

Kuna suala moja linanitatiza sana kila nikitafakari sipati jibu kabisa. Kipindi cha nyuma kidogo miaka 10 ilopita nilipata kuwafahamu watu wawili ambao walikuwa karibu sana na familia yetu hadi ikafikia kuwaita wajomba kwa majina mmoja alikuwa anaitwa kijo na mwingine alikuwa anaitwa solomoni. Walikuwa na ukaribu sana na familia kiasi cha kwamba mzee alikuwa anawashirikisha kwenye baadhi ya biashara zake binafsi.

Kijo alikuwa mtu smart sana kichwani mchapakazi alikuwa makini sana na mambo yake na alikuwa anaipangilia hela kwa umakini sana lakini cha ajabu alikuwa hana bahati hata kidogo yaani alikuwa hana kismart cha kupata madili wala alikuwa haleti big impacts kwenye masuala ya faida.

Kwa upande wa solomoni huyu jamaa alikuwa yupoyupo tu hajali kazi kihivyo hajali pesa yani matumizi yake yaovyo sana kwa ujumla alikuwa hayupo smart hata kidogo lakini cha kushangaza huyu ndio alikuwa na kismati cha kupata madili sana akisimama kwenye business za mzee na alikuwa anafanikisha biashara za mzee kwa kiasi kikubwa kwenye upande wa sales pamoja na kwenye suala zima la faida.

Nilikuwa najiuliza sana kiasi cha kwamba nilikuwa nakaa namuuliza mzee alikuwa hana cha kunijibu. Kijo na solomoni wote baadae waliondoka home na kwenda kutafuta life lao wenyewe kila mmoja na wakati wake japokuwa range ya muda wa kuondoka ulikuwa unalingana.

Sasa mwezi wa 12 mwaka jana niliwaona wote kwa mara ya kwanza tangu waondoke, walikuja kutusalimia cha kushangaza uncle kijo ambae alikuwa smart sana alikuwa hana chochote kile alikuwa anaonekana mtu ambae life limempiga lakini uncle solomoni yeye alikuwa yupo vizuri financially alikuja anadrive BMW x5 huku akimpa lift uncle Kijo.

Swali fikirishi hapa ni why yule alie smart alionekana kapigwa na life wakati aliekuwa anaonekana roughly amewin life?
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
14,480
2,000
Angalia movie moja ya Nollywood inaitwa Dangerous Twins, amecheza Ramsey Noah.

Kwa kifupi hao wazee wa kismati unaosema ni waongeaji sana, wazee wa deal na watoa mlungula sana mambo yaende.

In short wanakula na watu.
 

covid 19

JF-Expert Member
May 9, 2014
1,522
2,000
Watu wanaoendesha maisha yao kwa principle utawapenda Kama Wana ajira rasmi tofauti na hapo hawajiwezi kabisa ila wale wazee wa zima Moto wao ni connection na deals ndio zimawatoa wakiwekwa sehemu/vitengo ambavyo vinavyoitaji priciples wanakuwa dolooo yaan ata kazi wanaweza acha.

Binadamu tunautofauti Sana..

Hivyo kwa ufupi tu uncle wako joh hakuwa mahala sahihi kwa style yk ya maisha ila huyo mwingine alikuwa mahala sahihi toka awali.
 

Babumawe

JF-Expert Member
Sep 12, 2014
2,540
2,000
Angalia movie moja ya Nollywood inaitwa Dangerous Twins, amecheza Ramsey Noah.

Kwa kifupi hao wazee wa kismati unaosema ni waongeaji sana, wazee wa deal na watoa mlungula sana mambo yaende.

In short wanakula na watu.
Labda
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom