Natabiri: Vigogo wa CHADEMA kuhama chama kabla ya 2015

Ni chizi na machizi bora wabaki na machizi wenzao

Batilda mbona alikuwa akitembea mitaani kuomba kura, alikuwa akinunua mihogo na mahindi ili naye kujionesha ni mtu wa kawaida, kumbe kavaa
ngozi ya kondoo, baada ya kupigwa chini hakuonekana tena.
 
" if wishes were horses, beggers would ride"

" If ifs and ands were pots and pans,The tinker would never work"
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kaka una post 4 tu kaa macho au uko kazini kama hao wanao bwabwaja ? Mtangojea weee mtachoka .Chadema wakigundua wewe ni gugu unakatwa mara moja .Yule Mbung gani sijui mwache uone akatavyo katwa.Watu wako kimya wanafanya kazi wewe endeklea kuota huko security guard .
Mtoa mada anaonekana kama gamba hivi!! Tena inawezekana katumwa.
 
wamepata mbadala wa shehe yahaya anzisha na wewe utabiri wa nyota...lakini cdm inakuwa kila kukicha sijui utabiri wako umetowa wapi au umetumia vigezo gani?
ccm ya jk 2005 kura 80% 2010 kura 61% ,igunga 2010 kura 35,ooo 2011 kura 26,000 cdm kura 0-24,000 ndani ya mwaka.wabunge na madiwani increased
 
Hata kada hatulitaki, CDM tunaprefer zaidi kuitana MAJEMBE rather than Makada, Makada inakuwa ni kama yale mabwanyenye ya CCM. Neno kada limepoteza sifa na mvuto kwa CDM.

Makamanda ndilo linanoga zaidi.......hili chama kikosi maalumu

Anyway, achana na Green Guard huyo
 
Baada ya vugu vugu kubwa la uchaguzi na harakati nyingi na majungu mengi pamoja na vurugu za hapa na pale baina ya vyama vya siasa na mengineyo,naweza KUTABIRI wazi kutokana na habari nilokuwa nazo ( usiniulize nimezipata wapi ) kuna kila aina ya dalili kutoka kwa baadhi ya vigogo wa chama cha CHADEMA kuhama chama kutokana na baadhi ya viongozi hao kutokubaliana na mwenendo wa chama hicho...

Naweza nikataja majina ya baadhi ya viongozi hao lkn inawezekana nikawaharibia harakati zao hizo ama nikazidisha fitna ni bora tu wakayamaliza wenyewe.

Ila ninachowaomba tu endapo watahama ni bora kuhamia vyama vyengine vya upinzani kuliko kwenda kwa mafisadi wa CCM,kwani wakenda huko laana tu ya wananchi itawakumba kama ilivowatokea wenzao walopita,nafikiri mifano ipo Wawaangalie kina Tambwe hiza,Atiki ( wamekutwa wanagombana kwa kulipa mishkaki ) salum msabah ( yupo hoi kitandani ). Nafikri wadau mtawakumbusha na wengine walowahi kutokea.

Bora kina Lwakatare na Pr Safari hata kama hawatajiki kama mwanzo lkn bado heshima zao zipo juu sana na wanakubalika popote,ndio maana nikasema bora kama wana dhamira hiyo basi waende vyama vyengine vya upinzani ama wabakie tu CHADEMA kuliko kwenda CCM

umenoa, halitokei hilo.
 
Nimerudi kidogo baada ya kupitia comments za wadau tofauti, kwangu naona ipo haja ya viongozi wa CHADEMA ambao humu jamvini wamo,waje wakanushe hili na mimi nitakuja na ushahidi wangu. Ili tuondeo dhanna ya kutoaminiana kwa hili tunaloongea, nasema nina dhamira ya dhati,najulikana msimamo wangu humu JF ni mpinzani na msimamo wangu dhidi ya hili dudu CCM.\

Dhamira yangu kuu maisha ni kuukuza upinzani na hasa ushirikiano baina ya vyama vya upinzani,naamini wanaonijua humu kwa muda mrefu basi wakirudisha nyuma kumbukumbu zao watakumbuka baadhi ya thread zangu za ushirikiano wa upinzani.
 
MKASA WA MWAKYEMBE NA WAUAJI WA KUKODI TAYARI UMETUFUNDISHA MENGI MNO JUU YA SHEIKH YAHAYA NA CHIMBUKO LA 'TABIRI' ZAKE KUKIDHI AZMA ZA VIJIWE VYA SIASA NCHINI

Hata sheikh Yahaya tumegundua janja zake kutokana na mkasa wa Dr Mwakyembe kuwa alikua ni MBURUDISHAJI JAMII TU KWA KUCHEZEA AKILI ZETU huku akitumika kama kipaza sauti kutangaza uchuro wa baadhi ya mipango ya mauaji uvunguni laki kutaka kuaminisha umma kwamba ati katabiri.

Hakuna Mtanzani yeyote atakayeamini tena ghiliba zaidi za 'Tabiri' za Sheikh Yahaya mamboleo kuwa 'msemaji' wakijiwe chochote cha kisiasa nchini kama ambavyo tulivyozoeleka kuingizwa mjini hadi pale ambapo Dr Mwakyembe alipotufunuli
PAKA MWEUSI WA MWEMBECHAI(nalo pia likatolewe TAMKO) na janja zake mchana kweupe.

Nasema katika makundi hasimu mbali mbali ndani ya CCM, kundi litakaloibuka mshindi ni kundi lile litakalochagua kuunda genge na Mafisadi na badala yake kuwa upande mmoja na sisi wananchi.

Kundi mshindi kati ya makundi yote ya CCM ya hivi leo litakua ni kundi litakaloibuka mshindi lile kundi LITAKALOWEZA KUKIRIDHISHA CHADEMA kukubaliana na itikadi yetu ya UTAWALA WA MAMLAKA YA UMMA kuenziwa dhidi ya ufisadi hata wakajiunga kwetu wa kwanza kabla ya makundi mengineo kufanya hivo.

Wala sintostaajabu makada wawili watatu KULIPIWA MAHARI YA THAMANI KUBWA ama kuozwa huko huko CCM au kule kwenye CHAMA-KITENGO cha NCCR Mageuzi. Na huo ndio ukweli kuhusu jaribio la kumuondoa Mhe Mbatia ili huyo MWALI KUTOKA CDM akakutane na WACHUMBA WAKE MAFISADI huko huko.

Kama hii kamari ndio unaiona mchezo mpya kwako wewe hapo basi bora ungeomba msaada ukamegewe vipande mara kumi zaidi juu ya hili. Hata hivyo, Watanzania wa leo si wajinga; ndoa ya aina hii ambayo mpango unasema ufanyike wakati wowote kabla ya 2015, tayari ni ndoa haramu kuliko hata ile ya KAFU na CCM.

Mh.Majimarefu umeamua kumrithi Sheikh Yahaya???
 
Dhamira yako ni nzuri. Lakini utashirikiana na nani? Mbatia? Cheyo? CUF? Afadhali Chadema waendelee kuchanja mbuga wakiwa solo kwa sababu hakuna upinzani mwingine ulio makini Tanzania.
 
Hivi hata kam ni utabiri huu umezidi! Kwa nini usitabiri CCM itakufa muda si mrefu kwa kuwa ina migogoro iliyo wazi kabisa. Lakini yote hayo hujaoni unakimbilia CDM ambako hata kama kuna migogoro siyo kama ya wanaCCM! Jamani tuwe tunafikiri kabla ya kupost.
 
Baada ya vugu vugu kubwa la uchaguzi na harakati nyingi na majungu mengi pamoja na vurugu za hapa na pale baina ya vyama vya siasa na mengineyo,naweza KUTABIRI wazi kutokana na habari nilokuwa nazo ( usiniulize nimezipata wapi ) kuna kila aina ya dalili kutoka kwa baadhi ya vigogo wa chama cha CHADEMA kuhama chama kutokana na baadhi ya viongozi hao kutokubaliana na mwenendo wa chama hicho...

Naweza nikataja majina ya baadhi ya viongozi hao lkn inawezekana nikawaharibia harakati zao hizo ama nikazidisha fitna ni bora tu wakayamaliza wenyewe.

Ila ninachowaomba tu endapo watahama ni bora kuhamia vyama vyengine vya upinzani kuliko kwenda kwa mafisadi wa CCM,kwani wakenda huko laana tu ya wananchi itawakumba kama ilivowatokea wenzao walopita,nafikiri mifano ipo Wawaangalie kina Tambwe hiza,Atiki ( wamekutwa wanagombana kwa kulipa mishkaki ) salum msabah ( yupo hoi kitandani ). Nafikri wadau mtawakumbusha na wengine walowahi kutokea.

Bora kina Lwakatare na Pr Safari hata kama hawatajiki kama mwanzo lkn bado heshima zao zipo juu sana na wanakubalika popote,ndio maana nikasema bora kama wana dhamira hiyo basi waende vyama vyengine vya upinzani ama wabakie tu CHADEMA kuliko kwenda CCM

...kwani shek Yahaya amekurithisha mikoba?,hapa JF utabiri hauna nafasi,nenda kafanye utafiti utuletee habari za uhakika na za-kweli,achana na matunguli na majini yanakuzeesha kijana...
 
Hivi hata kam ni utabiri huu umezidi! Kwa nini usitabiri CCM itakufa muda si mrefu kwa kuwa ina migogoro iliyo wazi kabisa. Lakini yote hayo hujaoni unakimbilia CDM ambako hata kama kuna migogoro siyo kama ya wanaCCM! Jamani tuwe tunafikiri kabla ya kupost.

Ndugu CCM haina haja ya kuitabiri,hicho kinaeleweka wazi,mpaka kaburi tushachimba bado kuifukia tu. Tunachoangalia hivi sasa ni sisi wapinzani tusije tukajikwaa sehemu then tukawapa nafasi haya mafisadi. Hili unaliona dogo lkn hujui athari yake,CCM ndipo wanatumia mwanya sehemu kama hizi.

Najua nini ninachokiongea,na kama hatujajadili namna gani ya kulizuwia hili,Nakuhakikishieni maisha vyama vya upinzani havitakuja juu. Tuangalie wapi makosa yetu ili tuweze kuhakikisha tunaling'oa fisadi CCM,tumechoka nao.

Nitaendelea kuleta habari ambazo kama hizi zinazonitia kichefu chefu,lkn ambazo nitakuwa nina hakika nazo.
 
MKASA WA MWAKYEMBE NA WAUAJI WA KUKODI TAYARI UMETUFUNDISHA MENGI MNO JUU YA SHEIKH YAHAYA NA CHIMBUKO LA 'TABIRI' ZAKE KUKIDHI AZMA ZA VIJIWE VYA SIASA NCHINI

Hata sheikh Yahaya tumegundua janja zake kutokana na mkasa wa Dr Mwakyembe kuwa alikua ni MBURUDISHAJI JAMII TU KWA KUCHEZEA AKILI ZETU huku akitumika kama kipaza sauti kutangaza uchuro wa baadhi ya mipango ya mauaji uvunguni laki kutaka kuaminisha umma kwamba ati katabiri.

Hakuna Mtanzani yeyote atakayeamini tena ghiliba zaidi za 'Tabiri' za Sheikh Yahaya mamboleo kuwa 'msemaji' wakijiwe chochote cha kisiasa nchini kama ambavyo tulivyozoeleka kuingizwa mjini hadi pale ambapo Dr Mwakyembe alipotufunuli
PAKA MWEUSI WA MWEMBECHAI(nalo pia likatolewe TAMKO) na janja zake mchana kweupe.

Nasema katika makundi hasimu mbali mbali ndani ya CCM, kundi litakaloibuka mshindi ni kundi lile litakalochagua kuunda genge na Mafisadi na badala yake kuwa upande mmoja na sisi wananchi.

Kundi mshindi kati ya makundi yote ya CCM ya hivi leo litakua ni kundi litakaloibuka mshindi lile kundi LITAKALOWEZA KUKIRIDHISHA CHADEMA kukubaliana na itikadi yetu ya UTAWALA WA MAMLAKA YA UMMA kuenziwa dhidi ya ufisadi hata wakajiunga kwetu wa kwanza kabla ya makundi mengineo kufanya hivo.

Wala sintostaajabu makada wawili watatu KULIPIWA MAHARI YA THAMANI KUBWA ama kuozwa huko huko CCM au kule kwenye CHAMA-KITENGO cha NCCR Mageuzi. Na huo ndio ukweli kuhusu jaribio la kumuondoa Mhe Mbatia ili huyo MWALI KUTOKA CDM akakutane na WACHUMBA WAKE MAFISADI huko huko.

Kama hii kamari ndio unaiona mchezo mpya kwako wewe hapo basi bora ungeomba msaada ukamegewe vipande mara kumi zaidi juu ya hili. Hata hivyo, Watanzania wa leo si wajinga; ndoa ya aina hii ambayo mpango unasema ufanyike wakati wowote kabla ya 2015, tayari ni ndoa haramu kuliko hata ile ya KAFU na CCM.

Hata Ibrahimu alipokuwa akigombana mara kwa mara na binamu yake Loti alimwambia kuwa kwanini mimi na wewe kushindana wakati sisi ni ndugu? Kwa amani yetu basi nakuomba chagua upande unaotaka kwenda ukisema mashariki mimi nitaenda magaribi na ukisema magaribi mimi nitaenda mashariki....Loti kwa akili za mwili asitambue kuwa macho ya roho ndiyo yanaona mpaka invisibles akachagua upande ambao kuna miji mikubwa ya Sodoma na Gomora na akamwachia Ibrahimu upande ambao ni wa jangwa..Lakini Ibrahimu kwa kujua kuwa anaagano na yule ambaye kwa neno lake moja tu aweza geuza mambo yote na tazama kwakua moyo wake na dhamira yake ilikuwa njema huyo Yahwe kabla ya kuiangamiza Sodoma na Gomora akamjulisha mtumishi wake Ibrahimu mipango yake. Ibrahimu akamkumbuka Loti ndugu yake kwa maombi makubwa akaomba kwaniaba yake ili asiangamizwe ndani ya Sodoma na Gomora.....

Vile vile nasi tunawatakia kila laheri hao ndugu wachague wanapotaka kwenda ili sisi tubaki na amani yetu kwani hata wakienda huko bado sisi tutawaombea wasije angamizwa pamoja na hiyo mi Giant ya ufisadi maana katika macho yetu ya ndani kabisa kazi yao imeshamalizika na anguko lao ni matter of time! Kama vile mti unyaukavyo ndivyo ilivyokwao kwa sasa...

Ingekuwa ni mimi ningeamua kuwa kama Ruthi kwakujua kuwa Naomi ni Mwebrania na kwamba kokote aendako anaenda na baraka ndani mwake akamwambia mama mkwe wake huyo kuwa uendako ndiko nami ntakwenda watu wako watakuwa watu wangu na utakapozikwa nami nitazikwa huko huko...Kwakuambatana na Naomi akajikuta pamoja na kuwa mmataifa asiye na agano la baraka za Ibrahimu alijikuta akiwa mmoja wa bibi zake mwana wa Mungu bwana Yesu meaning authority yote ya mbinguni inampa heshima ya pekee kama mbeba maono yakimungu...Lakini kwa habari za duniani pia aliolewa na mwanaume tajiri sana Yeroboam....

Mhubiri amewafungua macho hao watu ya kimwili na yakiroho lakini tabia ya kimungu ni kuwa uchaguzi wa mwisho unakuwa niwa mhusika lakini neno linabaki kuwa ushahidi mpaka mwisho wa dahari....

A word of King has power and Kings rule by decrees! I decree and declare hakuna chama kitaishinda CDM 2015 katika kuchukua dola by hooks and crooks!
 
Ndugu CCM haina haja ya kuitabiri,hicho kinaeleweka wazi,mpaka kaburi tushachimba bado kuifukia tu. Tunachoangalia hivi sasa ni sisi wapinzani tusije tukajikwaa sehemu then tukawapa nafasi haya mafisadi. Hili unaliona dogo lkn hujui athari yake,CCM ndipo wanatumia mwanya sehemu kama hizi.

Najua nini ninachokiongea,na kama hatujajadili namna gani ya kulizuwia hili,Nakuhakikishieni maisha vyama vya upinzani havitakuja juu. Tuangalie wapi makosa yetu ili tuweze kuhakikisha tunaling'oa fisadi CCM,tumechoka nao.

Nitaendelea kuleta habari ambazo kama hizi zinazonitia kichefu chefu,lkn ambazo nitakuwa nina hakika nazo.

Hofu ni silaha ya adui ili kutengeneza panic na hatimaye akuangamize...Kuwa na amani mpendwa this time watu tuko full equiped kuanzia usiyoyaona mpaka unayoyaona. Umeshaambiwa CDM imeshavuka level ya public procurement (Infant) yaani ile stage ya pilot/testing imefika kwenye commercial (market) stage where demand na supply ndiyo rule inayo govern exchange...Ndiyo maana watu wakisikia maandamano ama mikutano wanaweweseka maana wanajua ni bidhaa adimu na dau lake linazidi kupanda day after day. Wewe chakufanya hangaika na promotion tu kwa consumers ili wengi waonje na waone how sweet and quality is the new product; hayo mengine waachie CCM iliyofikiwa level ya increasing at a decreasing rate.
 
Back
Top Bottom