Natabiri Lowassa kurudi CCM kabla ya 2020 na Magufuli kutawala kwa miaka 5 tu

Lowassa kawania urais mara moja? 1995 ulikuwa ushazaliwa kama bado waulize Wakubwa zako nani alikakatwa kwa kosa la kuwa na Mali nyingi kuliko Umri na akili zake?

Inawezekana nilikuwa sijazaliwa.

Hebu nikuulize wewe "mkubwa" wangu uliyekuwa umezaliwa;

Hivi aliwania Urais wa nchi gani eti?

Japo nilikuwa sijazaliwa, kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa wagombea wakubwa wa Urais wa Tanzania ktk uchaguzi wa mwaka huo waliokabana koo kisawasawa walikuwa ni;

1. B.W. Mkapa (CCM) na;

2. A.L. Mrema (NCCR Mageuzi)

Na ktk uchaguzi huo Benjamin W. Mkapa wa CCM aliibuba mshindi chini ya uchaguzi wa kwanza uliohusisha vyama vingi!!

Si hivyo tu, kumbukumbu yangu inaniambia Edward Lowassa alikuwa ni mwanaCCM bado wakati huo

Plz, hebu niambie huyu mzee yawezekana aliwania Urais wa Tanzania nisiyoifahamu mimi

Ama la, wewe unamaanisha kitu kingine.......Lowassa kuutamani Urais na kuomba ridhaa ya chama chake kimpe nafasi kuwa mgombea urais wa TZ

Kama ndivyo unavyomaanisha, basi Lowassa ameshaomba chama chake cha awali mara nyingi tu i.e CCM kimteue awe mgombea wa wa Urais wa TZ na kubali tu kuwa hiyo ni hoja tofauti kabisa na quatation yangu ya mwanzo ktk hoja yako!!
 
Mungu alimuumba Lowassa kusaidia Jakaya awe Rais wa Tanzania na alimuumba Jakaya kusaidia Lowassa asiwe Rais wa Tanzania.
Lowassa ataishia kuwa Kama Maalim Seif kushikilia record ya kuwania Urais mara nyingi zaid
Uzuri hata kugombea maranyingi hatafanya. Labda aanzishe nayeye SACCOS yake.
 
Mmeanza tena utabiri hapo Lumumba? Kwani yule mzee wa Bunda kahamishia kiringe Dar sasa eee!!!
 
Jamani mimi sio mpiga ramli wala mshirikina.

Kwa hali inayoendelea ndani ya serikali na ndani ya CCM, kuna uwezekano mkubwa sana Lowassa kurudi CCM kabla ya 2020 na kuja kupambana katika kuteuliwa Jina la kupeperusha bendera ya CCM 2020.

Ukweli ni ukweli tu japo wale wafia rangi ya kijani ukiwauliza utendaji wa Magufuli wanaonaje? Kwa unafiki watasema wanamkubali kwa 100% ukweli kuwa wapo kinyume, japo hawasemi, amewabana Kila sehemu ametaka kuonekana mtawala au mfalme, sasa ni dhahiri wamemchoka lakini hayo yatakuja baadae kudhihirika.

Lowassa bado ana ushawishi mkubwa ndani ya CCM, hata akirudi nguvu kubwa anayo kuzidi Magufuli ndani ya Chama.

Tuombe uzima na afya tufike hiyo 2020.

In shaa Allah!
Endelea kuota mkuu, huyo mtu wako akikoswa koswa na mahakama ya mafisadi itakuwa miujiza.

Kama CHADEMA mmemchoka mpelekeni CUF, nafasi ya mwenyekiti iko wazi!
 
Bado tu mnaendelea kupanga jinsi ya kumpiga pesa nyingine mzee wa watu? mwacheni make maji hayakamiwi daima. Siasa zina kikomo
 
Mnaota ndoto nyie. Lowasa kushiney kwa upotoshaji walioufanya kwa watanzania yeye na kingunge na sumaye kuwa ccm haijafanya lolote toka nchi ipate uhuru, wasahau kabisa suala la ccm.
 
Jamani mimi sio mpiga ramli wala mshirikina.

Kwa hali inayoendelea ndani ya serikali na ndani ya CCM, kuna uwezekano mkubwa sana Lowassa kurudi CCM kabla ya 2020 na kuja kupambana katika kuteuliwa Jina la kupeperusha bendera ya CCM 2020.

Ukweli ni ukweli tu japo wale wafia rangi ya kijani ukiwauliza utendaji wa Magufuli wanaonaje? Kwa unafiki watasema wanamkubali kwa 100% ukweli kuwa wapo kinyume, japo hawasemi, amewabana Kila sehemu ametaka kuonekana mtawala au mfalme, sasa ni dhahiri wamemchoka lakini hayo yatakuja baadae kudhihirika.

Lowassa bado ana ushawishi mkubwa ndani ya CCM, hata akirudi nguvu kubwa anayo kuzidi Magufuli ndani ya Chama.

Tuombe uzima na afya tufike hiyo 2020.

In shaa Allah!
hahaha kamanda naona umeoteshwa na shetani. hizi zinaitwa hekaya za abunuwasi.
 
Mnaota ndoto nyie. Lowasa kushiney kwa upotoshaji walioufanya kwa watanzania yeye na kingunge na sumaye kuwa ccm haijafanya lolote toka nchi ipate uhuru, wasahau kabisa suala la ccm.
hahaha wale wa ccm "imeishiwa pumzi" warudi kule watapokelewa na nani. labda waanzishe chama kingine tu
 
CCM tumeshaweka Get Valve. Anayetoka ni ngumu kurejea tena. Lowasa akirudi CCM ni kwa mapenzi hake ila sisi hatumhitaji tena. Hata ujumbe wa nyumba kumi hawezi kupata
Aliyemkata lowasa ni kikwete peke yake akiwa na nia ya kumpenyeza Membe mdogo wake si kwamba CCM hawakumpenda.
 
Lowassa akirudi CCM na CCM ikampokea mimi nitaingia Chadema na kugombea ubunge jimbo la Arusha
 
Endelea kuota mkuu, huyo mtu wako akikoswa koswa na mahakama ya mafisadi itakuwa miujiza.

Kama CHADEMA mmemchoka mpelekeni CUF, nafasi ya mwenyekiti iko wazi!
Hiyo mahakama itakuwa na majaji toka Ulaya? Waanze na kesi za ununuzi mabehewa mabovu ya Mwakyembe, Lugumi, Pesa za NIDA, uuzaji nyumba za serikali nk
 
Ni mjinga pekee anayeweza kuamini Lowassa atakuja kuwa raisi wa nchi hii.
JAPO MUDA MWINGINE FIKIRA ZA KIJINGA HUPITA
 
Ni mjinga pekee anayeweza kuamini Lowassa atakuja kuwa raisi wa nchi hii.
JAPO MUDA MWINGINE FIKIRA ZA KIJINGA HUPITA
Kwani hujui kuwa lowasa alishinda lakini uchakachuaji ukampora ushindi na mwaka 2020 kutakuwa na Dawa ya uchakachuaji ya kisasa.
 
Back
Top Bottom