Natabiri Lowassa kurudi CCM kabla ya 2020 na Magufuli kutawala kwa miaka 5 tu

Mungu alimuumba Lowassa kusaidia Jakaya awe Rais wa Tanzania na alimuumba Jakaya kusaidia Lowassa asiwe Rais wa Tanzania.
Lowassa ataishia kuwa Kama Maalim Seif kushikilia record ya kuwania Urais mara nyingi zaid
Kwa umri wa EL sidhani kama anaweza kufikia rekodi ya Seif ya kuwania urais.
 
Halafu atapitishwa na nani?wakati mwenyekit atakuwa---- mhuu!!mbona mnasahau
 
#HpaKaziTu imewavuruga wengi
Wamekosa Hoja, wamebaki kuota ndoto Za Mchana..... Huyo wanaesema atakuwa rais 2020 labda aumbe nchi yake akiwa na Nyumbu wenzake akawe rais huko.... Ila sio kwa watanzania wenye Akili timamu.
 
Wewe mtabiri huna taarifa za kutosha namna ya kumpata mgombea wa CCM. Iko hivi, ukisha-cross kutoka upande mmoja ukaenda upinzani tayari unakosa sifa zote za kuteuliwa kuwa mgombea sawa na Wassira na Makongoro Nyerere. Sahau Lowassa kurejea Lumumba. Atabaki tu Mikocheni.
 
Mungu alimuumba Lowassa kusaidia Jakaya awe Rais wa Tanzania na alimuumba Jakaya kusaidia Lowassa asiwe Rais wa Tanzania.
Lowassa ataishia kuwa Kama Maalim Seif kushikilia record ya kuwania Urais mara nyingi zaid

Pohamba

Lowassa keshawania urais wa TZ mara moja tu, mwaka jana 2015.

By 2020 atakuwa almost 70yrs old kama atakuwa na afya na nguvu aweza kuwania tena kwa mara ya pili na hopefully ndo itakuwa ya mwisho

Sasa atawania akiwa CHADEMA/UKAWA tena au CCM au chama kingine au kama PC hilo mimi silijui, nadhani tumwachie mtabiri Mr Hero!!

Isipokuwa Maalim Seif Shariff Hamad yeye keshawania urais wa Zenj mara tano (na kwa tafsiri yako hii ndo mara nyingi) kwa maana ya 1995, 2000, 2005, 2010 & 2015 na mara zote hizo hudaiwa ameshinda lakini huwa hatangazwi!!
 
Rafiki mambo ya kujua yatakayotokea hayaji simple simple tu. Hapa naona unajifurahisha tu.

Unatakiwa utoe critical analysis. Na hali halisi huku ukiangalia katiba na taratibu za vyama.
 
Pohamba

Lowassa keshawania urais wa TZ mara moja tu, mwaka jana 2015.

By 2020 atakuwa almost 70yrs old kama atakuwa na afya na nguvu aweza kuwania tena kwa mara ya pili na hopefully ndo itakuwa ya mwisho

Sasa atawania akiwa CHADEMA/UKAWA tena au CCM au chama kingine au kama PC hilo mimi silijui, nadhani tumwachie mtabiri Mr Hero!!

Isipokuwa Maalim Seif Shariff Hamad yeye keshawania urais wa Zenj mara tano (na kwa tafsiri yako hii ndo mara nyingi) kwa maana ya 1995, 2000, 2005, 2010 & 2015 na mara zote hizo hudaiwa ameshinda lakini huwa hatangazwi!!
Lowassa kawania urais mara moja? 1995 ulikuwa ushazaliwa kama bado waulize Wakubwa zako nani alikakatwa kwa kosa la kuwa na Mali nyingi kuliko Umri na akili zake?
 
Mi nachojua ukihama chama ukarudi tena huko baadae, watakuona huna msimamo na hutaaminika tena.
 
Jamani mimi sio mpiga ramli wala mshirikina.

Kwa hali inayoendelea ndani ya serikali na ndani ya CCM, kuna uwezekano mkubwa sana Lowassa kurudi CCM kabla ya 2020 na kuja kupambana katika kuteuliwa Jina la kupeperusha bendera ya CCM 2020.

Ukweli ni ukweli tu japo wale wafia rangi ya kijani ukiwauliza utendaji wa Magufuli wanaonaje? Kwa unafiki watasema wanamkubali kwa 100% ukweli kuwa wapo kinyume, japo hawasemi, amewabana Kila sehemu ametaka kuonekana mtawala au mfalme, sasa ni dhahiri wamemchoka lakini hayo yatakuja baadae kudhihirika.

Lowassa bado ana ushawishi mkubwa ndani ya CCM, hata akirudi nguvu kubwa anayo kuzidi Magufuli ndani ya Chama.

Tuombe uzima na afya tufike hiyo 2020.

In shaa Allah!
Hiyo ni sawia kabisa let's wait
 
Back
Top Bottom