Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Mosi,vigogo na watumishi wengi kwenye taasisi za umma kukimbilia kwenye mabenki kuchukua mikopo kukamilisha shughuli mbalimbali walizokuwa wamezianza au walikuwa wanaziendeleza katika awamu iliyopita kama vile shughuli za ujenzi wa nyumba za kuishi, kukamuilisha malipo ya ununuzi wa viwanja na miradi mingine ya binafsi waliyokuwa wakiiendesha kwa kutegema posho za safari, vikao, semina,makongamano na mambo mengine ya aina hiyo.
Pili, natabiri kudorora kwa kiasi kikubwa kwa shughuli za ujenzi kwenye maeneo mengi yenye shughuli za ujenzi.
Tatu,natabiri mapato ya serikali yanayotokana na kodi ya mauzo ya vifaa vya ujenzi kushuka sana.
Nne,natabiri mafundi wengi na vibarua wengi wa shughuli za ujenzi kukosa kazi maana wa kuwapa kazi nao mifuko imekauka.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba watu wengi humudu kufanya shughuli za ujenzi,hasa ujenzi wa nyumba za kuishi, ununuzi wa viwanja,n.k, kwa kudunduliza hela za semina,safari,vikao, makongamano,madili ya maofisini na mikopo ya benki(sasa watalazimika kukopa zaidi).
Naomba kila mtu afanye tathimini ya speed na kiwango cha shughuli za ujenzi kwenye maeneo yaliyopimwa kwa ajili ya shughuli hizi kwa kulinganisha na miezi 7 iliyopita.