Natabiri kuna siku Bernard Membe atarudi CCM

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Machi 1995 mwaka wa uchaguzi, Augustine Mrema aliondoka CCM akasema atagombea urais upinzani.

Julai 2015 miezi michache kabla ya uchaguzi Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu aliondoka CCM akatangaza atagombea urais upande wa upinzani.

Julai 2020 mwaka wa uchaguzi, Membe Waziri Mambo ya Nje Mstaafu kaondoka CCM, kasema atajiunga upinzani na atagombea urais. Mwaka 2025 (nani?) ataondoka CCM ataomba kugombea upinzani, naye atarudi CCM?

Agosti 2015, Frederick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu, alijiondoa CCM baadae akaomba kugombea Uenyekiti wa CHADEMA akakosa akarudi CCM.

Tofauti na hao kuna ambao walijiondoa CCM lkn wakabaki na misimamo yao, Kambona (RIP), Kingunge (RIP), Babu (RIP), Mtei, Maalimu Seifu nk.

Membe, hata kama italazimika upinzani kumpokea, ni sawa, lkn wawe makini sana wanapofanya naye siasa, kumbuka Membe ni jasusi mbobevu kama alivyo Mrema huwa hawasitaafu, akikosa anachokitafuta atarudi CCM kama kina Mrema, Lowassa, Sumaye na wengine wengi waliokuwa watumishi wa serikali.

Huu ni utabiri wangu tu, zingatia staili aliyoondoka nayo ya kuishukuru CCM ni kama anaweka mazingira mazuri pindi atakapoomba kurudi.

Wakati ni mwalimu mzuri sana.

Quinine.
===========≠
IMG_20200709_124534.jpg
 
Mkuu, itashangaza kuamini kuwa Membe kajiondoa CCM.Itashangaza zaidi kusikia CHADEMA wanafikiria kumchukuwa huyo kachero mbobezi na hasa ukizingatia ina watia nia waliojitosheleza.
 
Kwann asirudi wakati ni pandikizi la kuvuruga upinzani Kama sumaye na Lowasa,hizi Ni triki za ccm kila ukikaribia uchaguzi,rudisha kadi ni geresha tu
 
Mkuu, itashangaza kuamini kuwa Membe kajiondoa CCM.Itashangaza zaidi kusikia CHADEMA wanafikiria kumchukuwa huyo kachero mbobezi na hasa ukizingatia ina watia nia waliojitosheleza.
Awarudii kosa, mgombea ni lisuu
 
Ukisoma section 2 TISS Act Kuna kitu kinaitwa 'Active service' huyu jamaa ana kiapo cha usalama,wapinzani watachezeshwa akili pasipokujua jamaa yupo kazini

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani usalama wa taifa au usalama wa CCM kwahiyo akirudi CCM ndo amerudi usalama wa taifa mbona tuna mawazo mafupi sana kuona taifa ni sawa na CCM we unajua watu wangapi wanafanya kazi usalama wa taifa na wapo wapi? tuache hizi fikra kuwa usalama wa taifa ni CCM, Polisi CCM, jeshi ni CCM hivyo ni vyombo vya taifa sio vya CCM kuna viongozi wa hivyo vyombo wanakosa ueledi ndo maana unaona kama ni vyombo vya CCM ila sisi kama raia hatupaswi kutengeneza hii kasumba ya kuwamilikisha CCM inchi yetu na vyombo vyake, Membe apingwe kwa mengine sio eti kwasababu alikuwa afisa mwandamizi usalama wa taifa kazi aliyofanya kama raia mwengine yoyote kwani Marando karudi CCM.
 
Ungejua maana ya chama dola usingesema hivo.
Hivo vyombo vyote vinalinda ccm na sio taifa, sababu havipo huru.Ilipo ccm vipo.
Vingekuwa vinalinda taifa na utaifa, wasiojulikana wasingekuwepo,tungeongozwa na wazawa na sio wakuja.
 
Membe hawezi kaaa chama cha matamko we subiri uchaguzi uishe kama hajarudi CCM mapemaa, tena kuunga juhudi za raisi.

Ukiona mtu anahama sehemu harafu anaaga vizuri tena kwa ustarabu mzuri jua anawaza kurudi tena.
 
Mkuu, huu sio utabiri bali hiyo ndio hali halisi maana hawanaga ujanja.
 
Membe, hata kama italazimika upinzani kumpokea, ni sawa, lkn wawe makini sana wanapofanya naye siasa, kumbuka Membe ni Usalama tena mubobevu kama alivyo Mrema huwa hawasitaafu, akikosa anachokitafuta atarudi CCM kama kina Mrema, Lowassa, Sumaye na wengine wengi waliokuwa watumishi wa serikali.
Maneno yakoyana hoja nzuri na yenye mashiko.
Hata hivyo siku hazifanani.
Membe kafukuzwa CCM pale alipoazimia kuchukua fomu kushindana na Jiwe.
Upinzani hatugombani na watu wa Usuingia upinzani, sisi tunatafuta Dola na tukishinda hatuwezi kuwaepuka polisi,Usalama na Majeshi .
Membe ni mtaji kwa Upinzani, akishinda kwa nguvu za ushawishi alionao na msaada wa wapinzani, Faida itakuwa kwa ngome ya Upinzani.
Akishindwa kama ilivyokuwa kwa Lowasa, bado upinzani utafaidi wingi wa kura za uraisi na kuonngeza Posho na wingi wa wabunge kwa kambi ya upinzani.
na yeye atabakia kuwa ni mwnachama wa kawida tuu hadi chaguzi za vya zitakapo kuja tena baada ya miaka 4 ijayo hivi .

Nothing to worry.
Lakini najuwa CCM wanaogopa kudondokea pua ndio maana wanaleta fitina za hapa na pale.
 
Kwani usalama wa taifa au usalama wa CCM kwahiyo akirudi CCM ndo amerudi usalama wa taifa mbona tuna mawazo mafupi sana kuona taifa ni sawa na CCM we unajua watu wangapi wanafanya kazi usalama wa taifa na wapo wapi? tuache hizi fikra kuwa usalama wa taifa ni CCM, Polisi CCM, jeshi ni CCM hivyo ni vyombo vya taifa sio vya CCM kuna viongozi wa hivyo vyombo wanakosa ueledi ndo maana unaona kama ni vyombo vya CCM ila sisi kama raia hatupaswi kutengeneza hii kasumba ya kuwamilikisha CCM inchi yetu na vyombo vyake, Membe apingwe kwa mengine sio eti kwasababu alikuwa afisa mwandamizi usalama wa taifa kazi aliyofanya kama raia mwengine yoyote kwani Marando karudi CCM.
Mkuu kwa Tanzania usalama wa taifa ndio huo huo usalama wa CCM.
 
Maneno yakoyana hoja nzuri na yenye mashiko.
Hata hivyo siku hazifanani.
Membe kafukuzwa CCM pale alipoazimia kuchukua fomu kushindana na Jiwe.
Upinzani hatugombani na watu wa Usuingia upinzani, sisi tunatafuta Dola na tukishinda hatuwezi kuwaepuka polisi,Usalama na Majeshi .
Membe ni mtaji kwa Upinzani, akishinda kwa nguvu za ushawishi alionao na msaada wa wapinzani, Faida itakuwa kwa ngome ya Upinzani.
Akishindwa kama ilivyokuwa kwa Lowasa, bado upinzani utafaidi wingi wa kura za uraisi na kuonngeza Posho na wingi wa wabunge kwa kambi ya upinzani.
na yeye atabakia kuwa ni mwnachama wa kawida tuu hadi chaguzi za vya zitakapo kuja tena baada ya miaka 4 ijayo hivi .

Nothing to worry.
Lakini najuwa CCM wanaogopa kudondokea pua ndio maana wanaleta fitina za hapa na pale.
Hakuna mtu anayekataa upinzani kusajili wanaccm hasa wenye ushawishi kama Membe, lkn tunatoa tahadhari tu kuwa wawe makini kwa sababu kuna matukio kama yake yameshatokea huko nyuma kwa wana CCM kujiunga na upinzani dkk za lalasalama kisha wakikosa wanachotafuta hurudi walikotoka.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom