Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,265
- 105,429
Unaweza kumhukumu Magufuli leo kwamba atamuua Mbowe 2025?Kuna tatizo gani mtu/watu kusema "Magufuli anahadaa watu kwa kusema hataongeza muda", hasa tukijua asivyokuwa mtu muungwana katika mambo mengi. Mtu huyu mmoja ndiye amejitwalia madaraka yote nchini na yeyote anayejaribu kumpinga anakipata cha moto!
Kwa nini wewe udhani (utabiri) hataongeza muda, au wewe ndiye yeye?
Nimekueleza, hata mfumo uliokuwepo, pamoja na ubaya wake, lakini taifa halikuwahi kuwa na hali mbovu kama ilivyo hivi sasa.
Matumaini ya kubadilisha mfumo huo yalikuwepo na yangeweza kuendelea na hata kufanikiwa, chini ya huyu mtu mmoja unayemtetea kwa sababu uzijuazo wewe hakuna njia ya kubadilisha chochote; lakini wewe umekazania "watu wabadilishe mfumo"!
Ni nani kaandika "mjadala wa kubadilisha mfumo" ni tatizo. Ni wapi umesoma ikielezwa kwamba watu hawawezi kujadili kubadili mfumo kwa sababu tu wameandika kuhusu kutomwamini Magufuli juu ya kujiongezea muda?
Unazungukazunguka tu humo humo na vijimane hivi visivyokuwa na maana yoyote.
Watu watamzuia vipi "kujiongezea muda" kwa kujadili tu kwamba haaminiki kwa lolote analotamka kutokana na historia yake toka aingie kwenye utawala na kufanya mambo ambayo hayajawahi kufanywa na kiongozi mwingine aliyemtangulia. Kusema tu "kutamzuia"?
Hili unalozua la "...kupachika kibaraka wake...", mbona wewe unalisema..., hili ndilo litakalomzuia kujiongezea muda yeye?
Nikuulize wewe, kuna "makosa gani" watu kujadili hilo la kujiongezea muda, kiasi kwamba linakusumbua wewe na kusingizia kuwa wataishiwa nguvu za kufanya mambo mengine, kama "kubadili mfumo"?
'Assumption' yako ya kwamba kujadili Magufuli kuogeza muda kunasitisha mambo mengine yote ya kujikwamua na huyu mtu ni mbovu. Na hapo hapo una 'speculate" kuwa atamteua mtu mbaya zaidi yake, yote haya wewe unayatoa wapi?