Natabiri jaribio lolote la kubadilisha Katiba na ukomo wa Rais litaibua mazito

mtanzania in exile

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
808
1,000
Natabiri yakuwa jaribio lolote la kubadili katiba na kurefusha ukomo wa Rais litazuwa Moto wa kisiasa ambao haukuwahi kutokea tangu kuwepo kwa Taifa hili.

Yani hamtoamini wala kudhania. Itakuwa ni siku mbaya na nzito kwa Taifa ndipo sote tutaamini kweli kuna deep state in side state.

Nasali Jambo hili lisitokee wala kusemwa tu. Madhara yake yatatutesa sana kama Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
Hakutotokea lolote lile, watanzania domo kubwa bila vitendo. Wabunge wote ni ccm wakitakacho kitapita tu, ataekataa atafukuzwa uanachama. Wote wanajua kuwa asilimia kubwa yao wameingia bungeni kwa mlango wa nyuma, kwa hiyo watabaki kimya! Ama wananchi wa kawaida ni mahodari wa kupiga domo tu hakuna atakaefanya lolote kuzuia suali hili endapo CCM wakiamua kulijadili.
 

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
7,564
2,000
Kwanza kabisa, niseme mimi si mtetezi wa Magufuli wala CCM. Ni mtetezi wa haki na mchambuzi wa siasa na mantiki.

Magufuli nishamsema sana, hivyo, ninachoandika hapa si kwa sababu ya kumtetea Magufuli.

Twende kwenye hoja baada ya dibaji hiyo.

Magufuli ameshasema mara kadhaa hataki kuongeza muhula wa urais.

Kwa nini mnafanya hili suala kuwa hoja?

Hususan kama kuna makosa mengi sana ambayo Magufuli ameshayafanya ambayo yanaweza kujadiliwa kama hoja halali, factually, na si speculation?

Mimi naona wapinzani wa Magufuli kuongelea hili kunaonesha yafuatayo.

1. Hawana focus. Wanakuwa kama mtu tajiri mwenye hela nyingi sana (wana hoja nyingi sana halali za kumsema Magufuli) lakini ambaye bado anaenda kukopa hela benki kwa riba kubwa sana (licha ya kuwa na hoja nyingi halali za kumsema Magufuli, wanaenda kukopa hoja qmbayo haina uhalali ya kuhusu makisa ambayo hayajafanyika,kiasi cha kufanya watu wahoji umqkini wao).

2. Hawajadili mambo kwa facts. Bali kwa speculations.

3. Wanahukumu kosa ambalo wanafikiri litatetendeka, badalq ya kuhukumu kosa lililotendeka. Hili ni jambo hatari. Kwa msingi huu, Magufuli anaweza kuamka siku moja akasema ameota wapunzabi wanataka kumpindua. Akawafunga wote.

4. Wanapoteza muda na nguvu kujadili speculations wakati kuna mambo muhimu ya kubana sasa hivi kama wizi wa kura katika uchaguzi, tume huru yq uchaguzi, katiba mpya etc.

5. Wanaonesha paranoia. Kitu ambacho hakifai katika uongozi.
Unataka watu wasubiri kosa litendeke ndio waseme , acha kupotosha kigeugeu Cha Jiwe kinajulikana nchi nzima leo aseme hili kesho lile . Mfano halisi huu was kutaka wabunge wa upinzani kwa nguvu , wakati kwenye kampeni aliwaambia wananchi wasimchanganyie mabunzi na mabetri kwenye tochi . Nileteeni Gwjimaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa as concrete example .
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,446
2,000
Kwa hizi kelele za kijinga za kuangalia mtu badala ya mfumo mtaendelea kulalamika kila siku, wakati wenzenu wanawachezea, wanaiba kura, wanaendelea kuwatawala kimabavu.

Mkiendelea hivi, uchaguzi wa 2025 mtapigwa tena hivihivi, whether Magufuli anaendelea kuwa rais au haendelei is immaterial.

Kwa sababu bila mabadiliko ya msingi, anaweza kupachika mtu wake akaongoza kwa remote control.
Nilikueleza, ni-'address' mimi na siyo hao unaowaingiza kwenye mjadala ambao umekushinda kuuchangia na sasa unaingiza maneno yasiyosaidia chochote kama hayo ya "kelele, kijinga" n.k.

Sijui kama unaelewa kiasi ulichojifunua wewe ni mtu wa aina gani kutokana na uliyochangia katika mada hii.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,446
2,000
Anazuga hataki wakati sikuyoyote bunge likianz rasmi huo mswada kuna mbunge atauanzisha nak wakiupitisha atalazimishwa kukubali hapo watanzania dole litakuwa lishatuingia hatuna budi kutulia nalo

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu hawezi kulazimishwa. Ni yeye mwenyewe ndiye atakayekuwa kinara wa kulazimisha wampitishe aendelee kutawala. Hata wasipompitisha, kwani hana bunduki zaitakazomhakikishia anabaki?
 

Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,249
2,000
Hakuna cha deep state wala jeep! Deep state gani hii ya kufavor chama kilekile kuendelea kudidimiza nchi miaka na miaka? Tena kwa kodi ya wanamchi? Daah!
Labda anamaanisha vigogo wastaafu wa Ccm na serikali.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,116
2,000
Unataka watu wasubiri kosa litendeke ndio waseme , acha kupotosha kigeugeu Cha Jiwe kinajulikana nchi nzima leo aseme hili kesho lile . Mfano halisi huu was kutaka wabunge wa upinzani kwa nguvu , wakati kwenye kampeni aliwaambia wananchi wasimchanganyie mabunzi na mabetri kwenye tochi . Nileteeni Gwjimaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa as concrete example .
1.Jiwe hataongeza muda.
2.Hata asipoongeza muda hilo halimzuii kuweka kibaraka wake, au rais ajaye kutofuata katiba na kuharibu mambo.
3.Kwa sababu ya namba 2 hapo juu, mjadala wa mtu mmoja kuongeza muda bila kujadili mambo ya msingi kuhakikisha rais yeyote anayekuja anabwanwa, si mjadala wa mambo ya msingi.
4.Kwa sasa kila mtu atasema lake, tuufuatilie uzi huu mpaka 2025 tukijaaliwa tuangalie nani katabiri sawa.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,116
2,000
Nilikueleza, ni-'address' mimi na siyo hao unaowaingiza kwenye mjadala ambao umekushinda kuuchangia na sasa unaingiza maneno yasiyosaidia chochote kama hayo ya "kelele, kijinga" n.k.

Sijui kama unaelewa kiasi ulichojifunua wewe ni mtu wa aina gani kutokana na uliyochangia katika mada hii.
Nakuchanganya wewe na watu wengine wanaofikiri kama wewe kwenye kundi moja.

Kusema kwamba mjadala wa kumjadili mtu mmoja si muhimu, tunahitaji mjadala wa kubadilisha mfumo kuna tatizo gani?

Kusema kwamba, hata mkimzuia Magufuli kujiongezea muda, hamjamzuia kupachika kibaraka wake na kuongoza kwa remote control kuna makosa gani?

Siasa za Afrika zinazunguka katika personalities.

Tunaangalia watu, badala ya mfumo.

Na kwa siasa hizi, mtatawaliwa sana.Mkiendelea hivi, mtapigwa hata 2025, hata 2030.

Maana Magufuli msiyemtaka ataondoka bila kuongeza muda, lakini atapokewa na "Magufuli" type mwingine atakayeendeleza kuangalia interests za watu wachache.

Sasas hapo napo mtashangilia mmemzuia Magufuli kuongeza muda wa urais?

Mchezo mnaocheza ni mchezo wa kushindwa.

Kwa sababu, hata mkifanikiwa, bado mmeshindwa.

1. Magufuli akiongeza muda wa urais, mmeshindwa, kwa sababu ataendeleza uozo wake.
2.Magufuli akishindwa kuongeza muda wa urais, akamuweka kibaraka wake au mtu mwingine wa CCM akaja kuchukua nchi - kitu ambacho bila kubadili katiba/ tume ya uchaguzi ni wazi kitatokea tena- bado mtakuwa mmeshindwa, kwa sababu atakuja mtu mwingine wa CCM atakayeendeleza ujinga wa kila siku wa CCM.

You are playing a lose-lose game.

Whatever the outcome, you lose.
 

Babu Kivu

JF-Expert Member
May 7, 2013
430
500
Hili la 'kuongeza muda' si tuhuma mpya toka Upinzani kwenda kwa Raisi wa JMT.

Hata Jakaya alishazushiwagwa. Saa hii yuko Msoga.

Naungana na Msimamo wa Kiranga.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,116
2,000
Hili la 'kuongeza muda' si tuhuma mpya toka Upinzani kwenda kwa Raisi wa JMT.

Hata Jakaya alishazushiwagwa. Saa hii yuko Msoga.

Naungana na Msimamo wa Kiranga.
Hawa wapinzani walianza kulalamikia hili kabla ya uchaguzi wa 2020.

Nikawauliza, mnasema Magufuli ataongeza muda 2025, ina maana mshakubali 2020 mmeshindwa?

They are such crybabies.

Yani Magufuli akitumia habari za kuhukumu watu kwa makosa ambayo anafikiri watayafanya miaka mitano ijayo, anaweza kuwafunga wote kwa kesi za kutunga.

Halafu watamsema dikteta.

Yani tunataka kumhukumu mtu kwa kosa ambalo hajalifanya, kasema hatalifanya, katiba haimruhusu kulifanya na hatuna historia ya rais yeyote kulifanya huko nyuma?

Kabla ya kumhukumu Magufuli kwa hili, jiulize swali moja.

Wewe unaweza kukubali kuhukumiwa kwa kosa ambalo unabashiriwa kulifanya mwaka 2025?
 

profftobe

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
906
1,000
Ndungai ndiye katumwa kutekeleza hili. Na soon than later hili ndilo litakuwa habari kuu tza. Lakini...
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,738
2,000
Nakuchanganya wewe na watu wengine wanaofikiri kama wewe kwenye kundi moja.

Kusema kwamba mjadala wa kumjadili mtu mmoja si muhimu, tunahitaji mjadala wa kubadilisha mfumo kuna tatizo gani?.
Hili la 'kuongeza muda' si tuhuma mpya toka Upinzani kwenda kwa Raisi wa JMT.

Hata Jakaya alishazushiwagwa. Saa hii yuko Msoga.

Naungana na Msimamo wa @Kiranga.
wekeni akiba ya maneno jamani lisemwalo lipo na katika ngazi za Kata na Wilaya lilishapitiishwa kosa ni uropokaji
Nani anaweza kuniambia Kangi Lugola, Kessi au Juma Mkamia wameenda wapi au makosa yao ni nini zaidi ya kumtabiria au kumnyanyua mkulu?
 

Black BackUp

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
631
1,000
Kama ndiyo itapita hii hoja yako kikatiba, Wewe mtoa mada upo upande gani? "Magufuli Aendelee ama Asiendelee"?
 

Ndinani

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
6,291
2,000
Hiyo hoja umeitoa wapi?
Huna haja ya kuuliza hii hoja kaitoa wapi kwani wenye akili walisha liona hili siku nyingi!! Jiwe aliamza kwa kupangua majaji na kuwaweka wale wataomlinda; Executive imejaa wateule wake na wanaonesha Uhuru wa mawazo huwaondoa kwa mfano CAG Assad; amehakikisha wabunge wote pamoja na spika wao ni “watoto “ wake hivyo watafuata maelekezo yake !

Hizi ni mbinu za awali za dictator anayetaka kuhalalisha kukaa kwake madarakani kwa muda mrefu!!
Kumbuka ni hivi karibuni wamejipitishia sheria ya kujilinda na uharamia wanaofanya wakiwa madarakani!! Kwanini wapitishe sheria kama hiyo iwapo hawafanyi ujangili?
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,116
2,000
wekeni akiba ya maneno jamani lisemwalo lipo na katika ngazi za Kata na Wilaya lilishapitiishwa kosa ni uropokaji
Nani anaweza kuniambia Kangi Lugola, Kessi au Juma Mkamia wameenda wapi au makosa yao ni nini zaidi ya kumtabiria au kumnyanyua mkulu?
Ushaambiwa haya maneno yalikuwepo tangu enzi za Kikwete, na sasa Kikwete yupo Msoga kastaafu hajaongeza hata mwezi.

Mimi sipendi kusingiziwa kesi ya uongo, na najitahidi sana nisisingizie wengine kesi za uongo.

Unaanzaje kumpangia mtu kesi ya jambo atakalofanya 2025?

Kwa nini mnaacha kusema makosa ambayo Magufuli kashayafanya, yanajulikana, mnarukia makosa mnayobashiri atafanya mwaka 2025?

Kwa nini mnaacha kuzungumzia masuala ya msingi ya katiba mpya na tume huru yatakayomdhibiti rais yeyote wa Tanzania, Magufuli au kibaraka wake yeyote atakayemuweka, na mnamuangalia mtu mmoja Magufuli?

Magufuli asipoongeza muda na kumuweka kibaraka wake aendeleze mambo yake, mtajisifia mmemtoa Magufuli wakati utawala wa mabavu anauendeleza kwa remote control?

Mna uhaba wa makosa ya Magufuli? Mbona Magufuli kila siku anachemsha upya?

Wale waliosema Kikwete ataongeza muda leo wako wapi? Ndiyo nyie?

Mnataka Magufuli afanye nini ili mkubali haongezi muda?

Maana kasema haongezi muda. Katiba haimruhusu.

Mnataka afanye nini ili mkubali kwamba hataongeza muda?

Nenda mahakamani kafungue kesi ya kupinga Magufuli kuongeza muda wa kuwa rais mwaka 2025 basi upate haki yako.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,116
2,000
Ninapoona maneno yanayonibishia ni mengi kuliko ninavyoweza kuyajibu, huwa napenda kurejea vitabu.

Vitabu vumeandikq mengi.

Magufuli anahitaji kuwa kichaa zaidi ya kichaa kutukana legacy ya Political Godfather wake, Benjamin William Mkapa, ili kupangua Term Limits zilizowekwa kikatiba.

Tuliosoma kitabu cha Mkapa kinachoitwa "My Life, My Purpose: A Tanzanian President Remembers" tunaweza kuunganisha haya mambo.

Na kwa ambao hawajasomq kitabu, nawapatia makala ya kuhusu hili jambo.

Makal hii, ya kuhusu jinsi gani Baba Benjamin Mkapa alichukia ma rais wanaotaka kuongeza muhula wa urais, kwenye kitabu chake Mkapa, akielezea jinsi alivyompinga rais Salmin Amour wa Zanzibar na jaribio lake la luonheza muhula wa urais, inapqtikana hapa.

View attachment 1640451
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,446
2,000
Kusema kwamba mjadala wa kumjadili mtu mmoja si muhimu, tunahitaji mjadala wa kubadilisha mfumo kuna tatizo gani?
Kuna tatizo gani mtu/watu kusema "Magufuli anahadaa watu kwa kusema hataongeza muda", hasa tukijua asivyokuwa mtu muungwana katika mambo mengi. Mtu huyu mmoja ndiye amejitwalia madaraka yote nchini na yeyote anayejaribu kumpinga anakipata cha moto!
Kwa nini wewe udhani (utabiri) hataongeza muda, au wewe ndiye yeye?
Nimekueleza, hata mfumo uliokuwepo, pamoja na ubaya wake, lakini taifa halikuwahi kuwa na hali mbovu kama ilivyo hivi sasa.
Matumaini ya kubadilisha mfumo huo yalikuwepo na yangeweza kuendelea na hata kufanikiwa, chini ya huyu mtu mmoja unayemtetea kwa sababu uzijuazo wewe hakuna njia ya kubadilisha chochote; lakini wewe umekazania "watu wabadilishe mfumo"!

Ni nani kaandika "mjadala wa kubadilisha mfumo" ni tatizo. Ni wapi umesoma ikielezwa kwamba watu hawawezi kujadili kubadili mfumo kwa sababu tu wameandika kuhusu kutomwamini Magufuli juu ya kujiongezea muda?

Unazungukazunguka tu humo humo na vijimane hivi visivyokuwa na maana yoyote.
Kusema kwamba, hata mkimzuia Magufuli kujiongezea muda, hamjamzuia kupachika kibaraka wake na kuongoza kwa remote control kuna makosa gani?
Watu watamzuia vipi "kujiongezea muda" kwa kujadili tu kwamba haaminiki kwa lolote analotamka kutokana na historia yake toka aingie kwenye utawala na kufanya mambo ambayo hayajawahi kufanywa na kiongozi mwingine aliyemtangulia. Kusema tu "kutamzuia"?

Hili unalozua la "...kupachika kibaraka wake...", mbona wewe unalisema..., hili ndilo litakalomzuia kujiongezea muda yeye?
Nikuulize wewe, kuna "makosa gani" watu kujadili hilo la kujiongezea muda, kiasi kwamba linakusumbua wewe na kusingizia kuwa wataishiwa nguvu za kufanya mambo mengine, kama "kubadili mfumo"?
1. Magufuli akiongeza muda wa urais, mmeshindwa, kwa sababu ataendeleza uozo wake.
2.Magufuli akishindwa kuongeza muda wa urais, akamuweka kibaraka wake au mtu mwingine wa CCM akaja kuchukua nchi - kitu ambacho bila kubadili katiba/ tume ya uchaguzi ni wazi kitatokea tena- bado mtakuwa mmeshindwa, kwa sababu atakuja mtu mwingine wa CCM atakayeendeleza ujinga wa kila siku wa CCM.
'Assumption' yako ya kwamba kujadili Magufuli kuogeza muda kunasitisha mambo mengine yote ya kujikwamua na huyu mtu ni mbovu. Na hapo hapo una 'speculate" kuwa atamteua mtu mbaya zaidi yake, yote haya wewe unayatoa wapi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom