Nata kuwashtaki Vodacom

Selwa

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
543
524
Jamani hivi hii kitu inanitokea mimi peke angu?

Nimeweka kifurushi more than 15gb kimeisha ndani ya dakika 20 na sielewi ni kitu gani nimetumia maana simu ilikuwa inacharge. Nimenunua kifurushi kingine 10 GB nikazima data, nimeamka tena naambiwa kifurushi kimeisha. Sasa nataka kuwashtaki hawa Vodacom maana hii imetokea mara mbili sasa na naona nina fedha za kupoteza muda. naanzaje? maaana nasikia unaweza anza na TCRA kwanza.
 
Hamia airtel mkuu.mimi jana nilinunua mb70 sikuzitumia,lakini kila nikiingia mtandaoni naambiwa bando limeisha.hata sikuwaelewa.
 
Mie mhanga ktk hili pia mkuu!
Nimejiunga bundle ya 5000 dk kumi hazijaisha naambiwa kifurushi tee! Na niliingia JF na kucoment mara moja tu!!
Kitu huwa najiuliza kwann huwa mitambo haikosei kwenye kutoa data bure kwa wateja bali hukosea kwenye kuibia wateja tu!!!?
Am ndo tunalipa zile fain za boss wao na TALA??
 
Vodacom ni wezi hujui hilo?
Mimi mwenywe nilishawahi kuweka kifurushi cha 4gb zimepita sijui dakika ngapi eti kifurushi kimeisha.
Huduma kwa wateja nao sifuri kabisa.
 
Dah kumbe ni mchezo wao....aise kwa kweli nimepata nguvu za kuwashitaki
 
ila ujue endapo utawashtaki mahakaman, basi ujue wewe ndo una mzigo wa kuthibitisha kivipi vodacon wameshindwa kukupatia huduma uliyo lipia,
na wao pia lazima wata rise defences nying za kupinga hizo tuhuma zako,
sasa hiyo battle ukishinda, utapata pesa nyingi, sio tu ulizolipia hilo bando, bali hata gharama za kesi, na malupulupu mengne meng, lakini wakishinda voda sasa, hapo ndo utakwanguliwa hela za kutosha mbali na kwamba washakupiga hela za kutosha.

ushauri wangu we usiende mahakaman ila kama unataka nenda for your own risk!
 
Back
Top Bottom