Nasumbuliwa na tatizo la kutoka jasho kila napokula chakula (Hyperhidrosis)

spidernyoka

JF-Expert Member
Jan 2, 2020
5,985
15,469
Habarini wakuu,

Mimi ni kijana mdogo wa umri siku za karibuni nimekua nikisumbuliwa na kutoka jasho (sweating) kipindi napata kula.

Nakua natoka na jasho sehem ya mbele ya kichwa na uso yani forehead. Tatizo hili limekua linanikosesha raha hususan pale napoanza kusweat hata vile vipindi visivyo na joto.

Naombeni ushauri wa kitaalam na uzoefu wowote kuhusiana na hili tatizo.

Asanteni
 
Habari,

Kama ni kutoka jasho wakati wa shughuli yoyote, hiyo yaweza kuwa ni kawaida kabisa.

Ila kama utokaji wako wa jasho unaona hauendani na hali halisi basi ni vyema kufika hospitali na kupata ufumbuzi halisi.

Tatizo husika ni mtambuka kuanzia kwenye vichocheo/hormones, mishipa ya fahamu au infection kama fangusi.

Mgawanyo wa utokaji jasho waweza kusaidia kudadisi shida halisi kama unaweza kumpata physian kwa kuanzia, itakuwa vyema.
 
Habari

Nashukuru sana mkuu je waweza elezea zaidi kitaalam nadhani nitaelewa kwa kua nahusiana nayo kidogo jasho linalotoka hapa ni forehead tu na si mwili mzma na ni kipindi nakula tu nawaza je ni kwel nmepata damage ya parotid gland na how common is this?
 
Kwa maeneo yenye data kama Marekani ni 2.8 ya jamii wana tatizo kama hilo.

1: Localized/kwa sehemu moja ya mwili, sababu yaweza kuwa ni maambukizi ya fangusi.

2: Localized and more distributed. Sababu yaweza kuwa fangus, uoga uliopitiliza/anxiety, tatizo la sukari/kuwa chini, tatizo la vichocheo/homoni kama adrenaline, thyroid hormones kama Tsh, T3, T4 pia tatizo la mfumo wa fahamu/nerve ambayo inaweza kuwa overactive ikihusisha nerve moja au bandle zima la nerve fulani.

Daktari atakaekuona, akichukua historia yako vizuri na kufanya ukaguzi wa jumla wa mwili, ndipo atashawishika kujua ni vipimo vipi afanye. Ila inaweza kuhusisha upimaji wa mkojo, sukari, thyroid hormones, monofilament test ya nerve.
 
Mimi nikila chakula na nisitoke walau vijijaaho kwenye pua sijisikii kama nimekula chakula chenye nguvu.
 
Unapania sana chakula kijana ama una kula kwa uroho mfumo wako wa fahamu unakuwa unafanya kazi kubwa kweli kweli yaani unapagawa kiufupi.

Kama ambavyo mtu anapagawa na kutokwa na jasho akiwa labda kaokota pesa.

Mtazamo tu mzee
 
kwamba unaweza kupagawa na wali maharagwe
 
Mimi nikila chakula na nisitoke walau vijijaaho kwenye pua sijisikii kama nimekula chakula chenye nguvu.
Hio ni kawaida lakini kuna tatizo ambapo unaweza ukawa unatokwa na jasho jingi kipindi unakula kutokana na kutokea hitilafu ya mfumo wa taarfa mwilini ambapo mwili unaagiza tezi za jasho kutoa zaid jasho kipindi unakula ilhali makusudio halisi ilkua ni kuongeza mate mdomoni kupitia tezi za mate
kiufupi mwili unakosea kwa kutoa jasho jingi badala ya kuongeza mate mengi mdomoni kurahisisha shughul ya kula na mmeng`enyo wa chakula
 
Kapime sukari.
Acha kujipa/kujitakia magonjwa hyperhidrosis haipo hivyo..

Unasweat maeneo gani?

Kichwani na shingoni?

If yes you are experiencing gustatory sweating.
Muhimu mwone kwanza daktari.

Uwe na afya njema kijana mdogo.
 
Nimejicheck sukari npo sawa mkuu jana nlichek RBG
 
Kapime sukari.
Acha kujipa/kujitakia magonjwa hyperhidrosis haipo hivyo..

Unasweat maeneo gani?

Kichwani na shingoni?

If yes you are experiencing gustatory sweating.
Muhimu mwone kwanza daktari.

Uwe na afya njema kijana mdogo.
nasweat kwenye fore head tu ni fore head na ni wakat wa kula tu na si katika masuala mengine
 
Kapime sukari.
Acha kujipa/kujitakia magonjwa hyperhidrosis haipo hivyo..

Unasweat maeneo gani?

Kichwani na shingoni?

If yes you are experiencing gustatory sweating.
Muhimu mwone kwanza daktari.

Uwe na afya njema kijana mdogo.
Yamkini ni kwel sio hyperhidrosis lakin pia mkuu umenpa ugonjwa ambao sina gustatory sweating (freys syndrome) Complain yangu ni kutokwa na jasho kwenye fore head kipindi nakula chakula bila kujali room temp ya hapo nilipo
 
Back
Top Bottom