Nasubiria wagombea binafsi - hawa wa CHADEMA, CCM, CUF siwaamini tena

Natania

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
256
250
Lazima niseme ukweli kuwa mwanzoni niliweka matumaini ya kumpigia kura at least mmoja wa wagombea toka upinzani kwani CCM nilishaichukia toka enzi za akina Mrema miaka ya 90.

Lakini siku za hivi karibuni nimegundua kumbe hata upinzania ni walewale tu. Chadema na mikwara yao waliweza kunivutia mwanzoni ila kwa sasa hata nikiwa usingizini siwezi kumchangua kiongozi yeyote kutoka CHADEMA. Hili sakata la Zito, Kitila limeivua CHADEMA nguo zote na madudu mengi hayana majibu mpaka leo.

Yaani kwa sasa kama mtu ukiamua kuzingatia yaliyomo kwenye katiba bila kujali watendaji wake basi katiba ya CCM inamaneno mazuri na ya maendeleo -Tatizo ni hao wanaojiita viongozi wa CCM.

Nasema kwa sasa matumaini yangu YA KISIASA yamebakia kwenye wagombea binafsi -huenda hawa wakawa majasiri wa kufanya yale ya moyoni kuliko watu kama akina Slaa ambao wanakaa kimya kwenye madudu ya chama chao na kupigia kelele madudu ya chama tawala -hawa wakipewa nchi watakuwa hatari zaidi ya wanaChadema wanavyodhani.

Nimemaliza na haya ni maoni yangu, toa na wewe ya kwako!
 
Mhadzabe

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,887
2,000
Hao 'majasiri kutoka wagombea binafsi' unaowataka wametoka chama gan?
 
Natania

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
256
250
Hao 'majasiri kutoka wagombea binafsi' unaowataka wametoka chama gan?

Wagombea binafsi hawatakiwi kutoka kwenye chama chochote, hata kama kabla ya kugombea walikuwa CCM, CHADEMA, CUF as long as wanagombea kama wagombea binafsi, ukiritimba na madudu ya vyama hautakuwepo (at least).
 
Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,855
2,000
Menu yako iko tayari:
Mtikila, Hamad Rashid, Deo Kisandu.

Wengine wataraijiwa ni:
Zitto, Kafulila, Nape, Shibuda......
 
Natania

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
256
250
Menu yako iko tayari:
Mtikila, Hamad Rashid, Deo Kisandu.

Wengine wataraijiwa ni:
Zitto, Kafulila, Nape, Shibuda......

Mtikila akiachana na mambo ya vyama, yaani akiwa mgombea binafsi kura yangu anayo - kwa nafasi ya urais wa Tanganyika
 
kalou

JF-Expert Member
Aug 22, 2009
4,942
2,000
endelea kukipigia kura chama chako c.c.m.....siku hizi buku 5 hupati hata unit moja ya luku...sijui kama utaendelea kuandika post ikifika 2016 kwa mwendo huu..
 
Natania

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
256
250
endelea kukipigia kura chama chako c.c.m.....siku hizi buku 5 hupati hata unit moja ya luku...sijui kama utaendelea kuandika post ikifika 2016 kwa mwendo huu..

Bila shaka umeamua kujiandikia tu bila hata ya kusoma kile nilichokiandika. Aliyesema ataipigia kura CCM nani?
 
kalou

JF-Expert Member
Aug 22, 2009
4,942
2,000
Bila shaka umeamua kujiandikia tu bila hata ya kusoma kile nilichokiandika. Aliyesema ataipigia kura CCM nani?

Kwa hatua waliofikia c.c.m hakuna cha kufikiria mara 2..wameshindwa...bahati mbaya lazima kwenye sanduku la kura lazima uchague c.c.m au upinzania(so far)...kwa hiyo acha unafiki wako wa ki c.c.m
 
Natania

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
256
250
Kwa hatua waliofikia c.c.m hakuna cha kufikiria mara 2..wameshindwa...bahati mbaya lazima kwenye sanduku la kura lazima uchague c.c.m au upinzania(so far)...kwa hiyo acha unafiki wako wa ki c.c.m

duuu kazi kwei kweli! mimi nazungumzia wagombea binafsi ambao nao watakuwa wapinzani. shida sijui ipo wapi?
 
kalou

JF-Expert Member
Aug 22, 2009
4,942
2,000
duuu kazi kwei kweli! mimi nazungumzia wagombea binafsi ambao nao watakuwa wapinzani. shida sijui ipo wapi?

Nimeiona hii comment sehemu...ngoja tucheke wote..

hata ccm ifanye madudu gani
tunadunda tu. wamepandisha
ushuru wa magari. foleni Dar
zinaongezeka. wakapandisha
mafuta. tumo tu kwenye toyota
zetu. wakapandisha na umeme.
bado tunakula nao. wakaharibu
miundombinu ya maji. wanatuona
tunaoga. wapepandisha bei ya bia.
tunalala bar kabisa. ccm haituwezi
wa tz...

Usiku mwema mkuu
 
Mhadzabe

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,887
2,000
Wagombea binafsi hawatakiwi kutoka kwenye chama chochote, hata kama kabla ya kugombea walikuwa CCM, CHADEMA, CUF as long as wanagombea kama wagombea binafsi, ukiritimba na madudu ya vyama hautakuwepo (at least).

Usitanie bwana Natania Umesha sema wagombea binafsi, obvious hawatatokea au kugombea kwa mbeleko wa chama chochote, hata kama ni kweli hapatakuwa na ukiritimba wa aina hii iliyopo unayodhani ipo katika political parties, ila tegemea kutakuwa na " ukiritimba wa mtu binafsi" Je,aina hii ya ukurutimba mpya utakuwa nafuu na huu ambao unashirikisha watu wengi? (wanachama)
 
Last edited by a moderator:

Kimox Kimokole

Verified Member
Jun 9, 2010
967
1,000
"Mimi sina Chama"

Hii kauli inakera sana, utamsikia mtu anatoa kauli hiyo na kujinasibisha kama MCHANGIAJI HURU asiye na chama lakini ukitazama comments/threads zake utagundua mtu huyu anaegemea upande fulani wa chama. HUU ni UNAFIKI wa kiwango cha juu kabisa kwa Mwanadamu.

Mwalimu Nyerere (RIP) aliwahi kusema "Neutrality is the high level of irresponsibility, unapokuwa neutral maana yake hutaki kuwajibika"

Desmond Tutu nae akasema "A neutral person in the situations of injustice is always on the side of the oppressor".

Hivyo hawa wanaojitangazia U-Neutral wajitazame!!!!
 
Natania

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
256
250

Usitanie bwana Natania Umesha sema wagombea binafsi, obvious hawatatokea au kugombea kwa mbeleko wa chama chochote, hata kama ni kweli hapatakuwa na ukiritimba wa aina hii iliyopo unayodhani ipo katika political parties, ila tegemea kutakuwa na " ukiritimba wa mtu binafsi" Je,aina hii ya ukurutimba mpya utakuwa nafuu na huu ambao unashirikisha watu wengi? (wanachama)

Hata wanaogombea kupitia kwenye vyama wanakuwa na ukiritimba binafsi na ukichanganya na ukiritimba wa chama basi unakuwa na matatizo mawili at a go. Si ni afadhali ku-deal na tatizo moja?
 
lyinga

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,498
0
"Mimi sina Chama"

Hii kauli inakera sana, utamsikia mtu anatoa kauli hiyo na kujinasibisha kama MCHANGIAJI HURU asiye na chama lakini ukitazama comments/threads zake utagundua mtu huyu anaegemea upande fulani wa chama. HUU ni UNAFIKI wa kiwango cha juu kabisa kwa Mwanadamu.

Mwalimu Nyerere (RIP) aliwahi kusema "Neutrality is the high level of irresponsibility, unapokuwa neutral maana yake hutaki kuwajibika"

Desmond Tutu nae akasema "A neutral person in the situations of injustice is always on the side of the oppressor".

Hivyo hawa wanaojitangazia U-Neutral wajitazame!!!!

Kwanza elewa tz mambumbu tulivyokuwa wengi mtu anaposema mimi si mwana siasa au hayupo upande wowote huwa namfananinisha na zombi siasa ni uwanja mpana na ndio maisha yetu yakila siku mtu anaposema hayupo kwenye siasa huyo atakuwa ni marehemu ambaye atakuwa ametoka kwenye ulimwengu huu tuliopo yupo kwenye sayari nyingine siasa ni kila kitu katika maisha tunayoishi ya kila siku mfano maji, umeme, usafiri, afya, huduma nyinginezo za kijamii hivi vyote vinaendeshwa na hao wanasiasa ambao wana uwezo wakuamua leo kitu gani kipande na kitu gani kishuke kitu ambacho kinakugusa mojakwamoja wewe mwanadamu utake usitake sasa anaposimama mtu na kusema yeye si mwana siasa ni wakumsaidia apate elimu kwanza ajitambue pili apewe elimu ya uraiya na ndio maana hawa waliokwisha jitambua yaani wanasiasa wanatumia udhaifu wetu kufanya jinsi wanavyotaka mfano mzuri ni kwenye kipindi cha uchaguzi mwananchi wa kawaida utamkuta amenungunika na kukwazika kwa kipindi cha miaka 5kutokana na uongozi mbovu lkn inapofika siku ya maamuzi ya msingi ya kupiga kura haendi lkn kiongozi anapopatikana mbovu kwa uchache wa kura yuleyule mwananchi ataanza kulalama hapa ni kwasababu hajitambui na ndio maana nchi za wenzetu km marekani hata mgonjwa alielazwa hosp lazima apige kura kwa vile anajua thamani ya kura yake hapa ndio unapoona manufaa ya elimu ya uraia inapofanya kazi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom