Nasubiri kwa hamu kusikia tamko la Dr Asha Rose Migiro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nasubiri kwa hamu kusikia tamko la Dr Asha Rose Migiro

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by We know next, Oct 12, 2010.

 1. W

  We know next JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ningefurahi sana, na natamani sana kusikia tamko la Mama yetu aliyebeba Bendera ya Tanzania ktk Umoja wa mataifa, Dr Asha Rose Migiro, kuhusiana na uchaguzi unaotukabili wiki chache zijazo. Nasema hivyo kwa sababu kuu 2;

  1. Kwa kutumia nafasi yake kama Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, anayetoka Afrika, tena Tanzania, naamini kabisa anauwezo wa kutoa tamko la Kisiasa kuwaasa watanzania kuhusu uchaguzi huu, kwani nina uhakika kabisa joto hili la kisiasa atakuwa analipata live toka kwa wahabarishaji wake. Nina imani kubwa na tamko lake kuwa linaweza kuwafanya watu wakafikiri kidogo kwa mipango yoyoye ambayo si mizuri inayopangwa kwa uchaguzi huu.

  2. Akiwa kama Mtanzania, ambaye anaifahamu vizuri nchi yake, na kwa vile yuko katikati ya watu wa mataifa, lazima atakuwa na wakati mgumu kwa hali inavyoendelea kwa sasa hapa Tanzania. Naamini kuwa akitoa tamko lake binafsi, kama mtanzania, bila kutumia nafasi yake anaweza kabisa kutufanya Watanzania tukafikiria mara mbili, bila kujali tofauti zetu za kiitikadi.

  Naamini kuwa uadilifu wake kama Dr Asha Rose Migiro, ndio uliomfikisha pale na wala sio kwamba ni Mwanachama wa Chama fulani.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hana jipya atakalolisema..yaani hapa sisi tunangoja tamko moja tu la matokeo ya kumtangaza Dr.Slaa kuwa raisi mengine mi naona ni matangazo ya neti za hati punguzo tu watu wanazozibia michicha isiliwe na kuku
   
 3. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Hivi unajua procedures na ethics za Umoja wa Mataifa hasa kuhusiana na mtendeji wake kujihusisha na masuala ya nchi aliyotoka? Lakini pia kwa nini umbebeshe Dr Migiro wakati Katibu Mkuu wake yupo na pia Umoja huo una msemaji wake kule New York na pia hapa Tanzania?
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Huyu mama hana tofauti na wenzie wana CCM, JK, et al. Usitarajie lolote jipya kutoka kwake. Kwanza likwisha sema baada ya kuchaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu kuwa yeye si kwa ajili ya Tanzania tu bali kwa mataifa yote!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks Mkuu

  we love to politicize everything these days
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,357
  Likes Received: 3,116
  Trophy Points: 280
  Atasema tofauti zaidi ya kuponda upinzani kweli......kwani yule ni mwana ccm damu labda km atavaa moyo tofauti na ule wa kusema "nitaipenda ccm daima"
  ngoja tusubiri
   
 7. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Atoe tamko!!!! anjipenda hajipendi? tena mtum wenyewe Asha.mnhhhhhhh
   
Loading...