Nasubiri kuwajua waliochota mabilioni ya Escrow kupitia bank ya Stanbic

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,986
144,313
Kubenea aliahidi kuwataja waliokwapua mabilioni ya Escrow kupitia bank ya Stanbic iwapo atachaguliwa kuwa mbunge kwani akiongea ndani ya bunge atakuwa na kinga ya kutoshitakiwa.

Kwa bahati nzuri huyu mh.amechaguliwa kuwa mbunge wa Ubungo na ninavyomjua atatimiza ahadi yake hii.

Kubenea, tunakusubiri utegue kitendawili kilichowashinda wenye mamlaka.
 
kweli mkuu una mawazo kama yangu. kubenea ameahidi kuwataja waliobeba Escrow kupitia stanbic ndani ya BUNGE.
 
Nilikuwepo kwenye mkutano wake wa ufunguzi wa kampeni pale Mabibo nilisikia kwa masikio yote mwili nategemea atatekeleza ni kamanda ambaye si mwoga
 
Nilikuwepo kwenye mkutano wake wa ufunguzi wa kampeni pale Mabibo nilisikia kwa masikio yote mwili nategemea atatekeleza ni kamanda ambaye si mwoga
Na kwa jinsi serikali ya JK ilivyomtenda,bila shaka hii itakuwa ni nafasi yake ya kulipiza
 
Atawataja kwa number zao za magari wanayotembelea mkawatafute wenyewe huko mitaani! Wote walio lifumbua ishu ya escro wote isipokuwa Zitto hawatakuwepo bungeni walishatemwa! RIP Deo
 
Magufuli Amesema ATAANZIA Hapo, Kuwakamata, Kuwashitaki, Kuwafunga Na Kuwafilisi WOOTE Waliogawana Mabilioni Ya Pesa ZETU!!! Naomba Aapishwe HARAKA,
 
Mie naomba Mh. Magufuli aiombe Ile orodha ya wauza Unga kwa Mh. JK ili atutangazie Watanzania tuwajue....maana alisema kuna vigogo na viongozi wa dini
 
Awataje haraka kabisa ili kumrahisishia kazi Rais Mteule John Pombe Magufuli ktk mahakama yake atakayoanzisha ili kupambana na majizi ili aanze nao
 
Mama wa hela za mboga mboga ESCROW (Kimenyanyuka)wamemrudisha bungeni na mshirika wake(chege) wakawe mawaziri wakaibe pesa wajiuzuru.
 
Sahau kuwajua.
Waliomuweka Magufuli madarakani ndio waliochota hizo fedha.
Hawezi kuwageuka hata siku moja.
 
Kubenea aliahidi kuwataja waliokwapua mabilioni ya Escrow kupitia bank ya Stanbic iwapo atachaguliwa kuwa mbunge kwani akiongea ndani ya bunge atakuwa na kinga ya kutoshitakiwa.

Kwa bahati nzuri huyu mh.amechaguliwa kuwa mbunge wa Ubungo na ninavyomjua atatimiza ahadi yake hii.

Kubenea, tunakusubiri utegue kitendawili kilichowashinda wenye mamlaka.

Halafu mheshimiwa raisi mteule awapeleke mahakama ya mafisadi!
 
Back
Top Bottom