Nasubiri fisadi mmoja wa mfano

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,982
45,900
Nasubiri kwa hamu kuona fisadi mmoja wa mfano ambaye atawajibika kwa matumizi mabaya ya fedha za uma.

Nasubiri hili likichagizwa na uwepo wa mahakama ya mafisadi.

Nasubiri kuona fisadi huyo akipewa adhabu kali ambayo itawafanya mafisadi wengine kufikiria mara mbili pale wakiona fedha za wananchi zikipita.

Nasubiri kuona mali zilizopatikana kwa ufisadi zikitaifishwa na kuuzwa hatimae fedha zikarudishwa kwenye akaunti zilikochukuliwa.

Nasubiri kuona kifungo kisichopungua miaka 30 na kazi ngumu.

Nasubiri kuona hayo nikikumbuka, maisha ya tabu waliyopata watanzania wote kwa kukosa dawa, madawati, ada, vitabu, ajira, kisa tu fisadi kaamua kujibinafsishia fedha zetu zikawa zake.

Namsubiri kwa hamu kubwa fisadi wa mfano.
 
Haahaaaa, nje ya ccm hutakaa umuone, mie nasubiri Lugumi, na mabehewa feki.
 
Mafisadi wakubwa wanapewa cheo hawa wadogo wadogo ni kuwasumbua tu kwa hiyo futa kabisa wazo hilo
 
Fisadi wa mfano ana kinga!! na hata kama asingekua na kinga kumpata isingekuwa rahisi maana maisha yake ni angani!! labda angefungwa huko huko angani!!
 
Back
Top Bottom