Nassari wa Arumeru Mashariki kushtakiwa kwa uhaini? Anatafutwa na Polisi

Polisi wanatumika vibaya na kuzidi kudhalilishwa. Kwa hili wangeminya tu. Manake hivi sasa wanaonekana kufanya kazi kwa kuchagua kosa lipi lishughulikiwe, lipi liachwe kutegemeana na ama maagizo ya serikali ya CCM au wao wenyewe kuhangaika kujikomba kwa watawala. Mikutano ya kisiasa ya vyama vyote nchini haikosi kauli za "kufikirisha" na "kuchangamsha". Wala hazitishii amani yoyote zaidi ya manyanyaso na adha wazipatazo wananchi siku kwa siku toka kwa dola na vyombo vyake. Hivyo, kuwang'ang'ania akina Nassari huku unawagwaya akina Lusinde, Mkapa, Tyson, n.k. ni aibu!
 
Mkuu Mwakalinga siku hizi una comment as if unakaribia kuvaa gwanda au ni macho yangu.

Mkuu Feedback ukombozi dhidi ya magamba niliuanza siku nyingi kwa uwezo wangu mdogo nilionao.So hizi ni harakati za sasa za kuungana na wenye malengo yanayoshabihiana na mimi kwa njia yoyote ile ili mradi tuwaadabishe Magamba kwa faida na maendeleo ya nchi yetu.
 
Last edited by a moderator:
Tanzania ni moja na tutasonga mbele pamoja tutainama pamoja,tutainuka pamoja. Sasa NASSIR anavyotoa kauli ya Mhe Raisy asikanyage kaskazini ana maana gani?.Nikiongozi tena wakitaifa huyu jamaa na Chama chake kina mtegemea CDM, Moye anyanyuka na kusawazisha kauli za vijana wake baada ya kugundua kuwa KATOA AGENDA YAO YA SIRI YA UKASKAZINI INAYO WATAFUNA WAPINZANI.

...Sasa kama huyo kiongozi wangazi ya juu kaambiwa hivyo sasa sisi watanzania walalahoi tukiwapa hii NCHI YETU NADHANI TUTAFANJWA KUWA WAKIMBIZI NDANI YA nchi yetu,, yaana nawaogopa sana hawa CDM ZAIDI YA gonjwa lolote......
 
Mkuu wa mkoa aliwahi kutoa tamko la kuzuia watu ambao siyo wa Arusha kuja Arusha...Na huko Msoma Mkuu wa wilaya kama sikosei alimtaka Tundu lisu na wengine ambao siyo wahuko waondoke haraka sana...mama uko hapo...Mbona hukunyanyua masaburi yako kulalamika acha ujinga hata hivyo Nasari hakuiimanisha kama mnavyo potosha CCM...
 
Ulianza vizuri lakini ghafla ukaamua kuchanganya mboga pamoja na samadi ya binadamu humu; hebu kaa pembeni kidogo tutakutazama baadaye huko tukipta nauli.

Marehemu Ditopile alipozuia watu 'WENYE MATONGOTONGO' (sie tunaotoka mikoani) kutokukanyaga Dar wala kuota kutafuta uongozi mkoani hapo labda kulisahaulika mtu wa kumfungulia mashitaka ya UHAINI au? Bure kabisa kwa hili la selective administration of justice katika nchi moja na mazingira yale yale

Sasa mazingira kama hayo hayo yakitokea kwa kiongozi wa kambi ya upinzani sasa ndio ipate kuonekana nongwa?????
 
Tanzania ni moja na tutasonga mbele pamoja tutainama pamoja,tutainuka pamoja. Sasa NASSIR anavyotoa kauli ya Mhe Raisy asikanyage kaskazini ana maana gani?.Nikiongozi tena wakitaifa huyu jamaa na Chama chake kina mtegemea CDM, Moye anyanyuka na kusawazisha kauli za vijana wake baada ya kugundua kuwa KATOA AGENDA YAO YA SIRI YA UKASKAZINI INAYO WATAFUNA WAPINZANI.

...Sasa kama huyo kiongozi wangazi ya juu kaambiwa hivyo sasa sisi watanzania walalahoi tukiwapa hii NCHI YETU NADHANI TUTAFANJWA KUWA WAKIMBIZI NDANI YA nchi yetu,, yaana nawaogopa sana hawa CDM ZAIDI YA gonjwa lolote......

Ni aibu sana kujibishana na mtu ambaye hata kuandika vizuri maneno ya kawaida kabisa hawezi, yaani bado anajifunza kuandika lakini anayo kompyuta au simu. Post ya kwanza tu unaweka utumbo wa propaganda za ajabu...huwezi hata kujificha siku ya kwanza hii.

Nimeanza kuona umuhimu wa signature ya Invisible. Aliona mbali.
 
Tanzania ni moja na tutasonga mbele pamoja tutainama pamoja,tutainuka pamoja. Sasa NASSIR anavyotoa kauli ya Mhe Raisy asikanyage kaskazini ana maana gani?.Nikiongozi tena wakitaifa huyu jamaa na Chama chake kina mtegemea CDM, Moye anyanyuka na kusawazisha kauli za vijana wake baada ya kugundua kuwa KATOA AGENDA YAO YA SIRI YA UKASKAZINI INAYO WATAFUNA WAPINZANI.

...Sasa kama huyo kiongozi wangazi ya juu kaambiwa hivyo sasa sisi watanzania walalahoi tukiwapa hii NCHI YETU NADHANI TUTAFANJWA KUWA WAKIMBIZI NDANI YA nchi yetu,, yaana nawaogopa sana hawa CDM ZAIDI YA gonjwa lolote......

Mkuu lazima wewe utakuwa mwendawazimu.
 
ng'wizukulu ; umeongea maneno mazito na pengine yana ukweli ... lakini nadhani huu haukuwa wakati mwafaka kwake kuwekwa bayana .

sote mabadiliko tunayahitaji lakini sio kwa style ya hatari namna hii .
 
Juzi juzi mkuu wa mkoa mmoja alilazimika kuomba kuhama mkoa wa shy kwa kuwa aliwahi kuropoka akiwaambia wasukuma wasiende na ngombe wao katika jimbo la kwake. Alipata shida kuongoza mkoa huo.

Issue hapa ni kujua tangu lini wakajua kutafsiri matamko ya kisiasa? Nani kawafundisha siasa polisi?
Ningeelewa kama kiongozi wa serikali angepeleka malalamiko polisi kushtaki ili Nasari akamatwe na kushtakiwa. Lakini hii ya polisi kuingilia masuala ya kisiasa, yanalichafua jeshi la polisi na kuiharibia CCM.
 
Kweli katika utumbo wanasiasa waliongea wa bwana mdogo nassari unaweza ukawa no1.Kweli ameenda mbali sana hadi kumpiga mkwara mkuu wa kaya.Shukrani za pekee zimwendee mbowe kwa kuokoa jahazi.Kama ningekuwa bungeni ningemwomba afute kauli.
 
Tanzania ni moja na tutasonga mbele pamoja tutainama pamoja,tutainuka pamoja. Sasa NASSIR anavyotoa kauli ya Mhe Raisy asikanyage kaskazini ana maana gani?.Nikiongozi tena wakitaifa huyu jamaa na Chama chake kina mtegemea CDM, Moye anyanyuka na kusawazisha kauli za vijana wake baada ya kugundua kuwa KATOA AGENDA YAO YA SIRI YA UKASKAZINI INAYO WATAFUNA WAPINZANI.

...Sasa kama huyo kiongozi wangazi ya juu kaambiwa hivyo sasa sisi watanzania walalahoi tukiwapa hii NCHI YETU NADHANI TUTAFANJWA KUWA WAKIMBIZI NDANI YA nchi yetu,, yaana nawaogopa sana hawa CDM ZAIDI YA gonjwa lolote......

HEBU TOKA HaPA NI PUMBA TUPU UNAONGEA **** WEWE kwanza unaonekana hata kusoma hujasoma..RAISY (rais);MOYE(mbowe);TUTAFANJWA(tutafanywa),YAANA (yani),NASSIR(nassari) la sivyo we ni mkimbizi unaogopa magwanda yakishika nchi mtarudishwa kwenu somalia peleka makalio yako..tafakari then andika sio wakurupuka tuuu
 
vijana wa mkoa wa pwani walisema rais ajye hawezi toka kazkazini na kikwete ndo anamjua rais ajaye mbona hawajakamatwa?
 
kumbuka kwamba unatakiwa pia kuwaogopa viongozi mafisadi, wenye kupanda na silaha za mota majukwaani katika mikutano ya hadhara na wenye kumiliki silaha za kijeshi kinyume cha sheria na bado polisi haina nguvu ya kuwafanya lolote. Angalau huyu hata polisi inaweza kumchukulia hatua. Ogopa zaidi viongozi wabovu lakini walio juu ya sheria.
 
INGAWAJE MABADILIKO YA KWELI NDANI YA NCHI HII KITOVU CHAKE A-TAUNI, TSUNAMI LAA KISIASA LITAKALOLIFUNIKA KABISA CCM NA MAFISADI WAKE SASA MIKONDO YAKE KUKUTANIA IDODOMYA

Wanabodi bado nakumbuka; Wanaharakati tulipoanza wengine walitubeza, CHADEMA ilipoanza kuwakabili sana MAFISADI kwingineko chama chetu hiki kikapata kubatizwa jina 'Vyama vya Msimu',

na hivi sasa, kwa kuwa CHADEMA imebadilika na kuwa zaidi ya msumari wa moto kwa MAFISADI hao hao na kwa jinsi hiki chama cha Rostam Aziz kinavyoendelea kuzama fasta ajabu kwa Kimbunga Cha Lema wenzetu sasa wanatukaba kwa kuua wanachama wetu.

Hebu mwenzenu mwachieni Mh Nassari akahimize kitu Utaifa mbeeeele kama tai LAKINI katika kweli, heshima kwa utu wa Mtanzania katika mazingira ya HAKI na HAKI tu na wala si kwa kutegemea tabasamu katika uso wa rais wa nchi na viongozi maswahiba wake!!

Naam, japo ni kweli mabadiliko ya kuikomboa nchi hii yalianza rasmi na ule umwagaji damu kule A-Town lakini hivi sasa Tsunami ya kisiasa yaja kutoka kanda ya Ziwa
(Bukoba, Mwanza, Mara na Shinyanga) ...

... na hivyo kuja kukutana na ule mkondo wa Kanda ya Juu Kusini
(Njombe, Mbeya, Iringa, Songea) na siku zitakapokutania pale katika Jiji la Idodomya basi hapo hapo ndipo CCM pamoja na MAFISADI wooote watakapoDIDIMIA kimoja na kusahaulika na historia hata kabla ya 2015.

Habari ndio hiyo wanabodi kwa wale waliodhania kwamba kimbunga CHADEMA ni kule kaskazini tu.
 
Kumbe kanda ya kaskazini ni Lulu ya Tanzania!
Ahaaaaa!!!! Endeleni kuipigania isijitenge sasa! Mkituletea za kipwani tunawabeep na ukaskazini nyama nyie!
Mbona UVCCM mkoa wa pwani walitoa tamko kwamba rais wa 2015 hatatoka Kaskazini? Je huu si ubaguzi wa kikanda?
 
Kama historia ya falme za Roma,Ufaransa, Ottoman, na vidikteta vichawi huku karibu na nyumbani kwetu,CCM itaanguka hata kama ikinusurika 2015 kimuujiza.
Tena kama kuna wana CCM wasafi hao nao watakombolewa maana wengi wanamtumikia kafiri wapate mradi wao
Mapinduzi ya kweli yanamkomboa mkandamizwaji na mkandamizaji pia
CDM tuwakomboe wanyanyaswaji na wale wanyanyasaji pia
 
Tanzania ni moja na tutasonga mbele pamoja tutainama pamoja,tutainuka pamoja. Sasa NASSIR anavyotoa kauli ya Mhe Raisy asikanyage kaskazini ana maana gani?.Nikiongozi tena wakitaifa huyu jamaa na Chama chake kina mtegemea CDM, Moye anyanyuka na kusawazisha kauli za vijana wake baada ya kugundua kuwa KATOA AGENDA YAO YA SIRI YA UKASKAZINI INAYO WATAFUNA WAPINZANI.

...Sasa kama huyo kiongozi wangazi ya juu kaambiwa hivyo sasa sisi watanzania walalahoi tukiwapa hii NCHI YETU NADHANI TUTAFANJWA KUWA WAKIMBIZI NDANI YA nchi yetu,, yaana nawaogopa sana hawa CDM ZAIDI YA gonjwa lolote......

Kama unaendekeza ukabila hamia rwanda au burundi kwa wahutu na watutsi . Swine
 
Back
Top Bottom