Nassari kufikishwa mahakamani kwa kuchimba visima bila kibali.

Lion's Claws

Member
Apr 3, 2012
30
14
Kuna tetesi hapa A town kuwa Nassari anaandaliwa zengwe la kufikishwa mahakamani eti kwa kuchimba visima alivyoahidi wakati wa kampeni bila kibali cha serikali. Magamba wanadai ni kitendo cha rushwa ndiyo maana amechaguliwa. Mwenye habari zaidi atujuze. Magamba wanazidi kuweweseka. Chanzo minong'ono mtaani
 
Nawapeni ushauri wana arusha, Anzeni kuwaadabisha hao wanaofungua mashtaka ya kizushi!!
 
hahaha wao mbona waligawa wali an maharahe kule igunga? au kwa vile wao wameshika makali?
wale wale waliomshtaki lema ndio wanatumika leo tena
 
Mimi nafikiri kama ni makosa kuahidi miradi ya maendeleo wakati wa kampeni, basi waanze kwanza kumshitaki JK aliyepita nchi nzima akitupatia ahadi lukuki za miradi ya maendeleo, tena kuna mwelekeo wa ahadi nyingine kutotekelezeka. Bora hata huyo Nassari aliyeahidi visima ambavyo tayari kaanza kuvichimba!
 
ahahahahahaha.......hii nayo imenitoa, Kwa hiyo JK akitununulia MV BUKOBA mpya hapa aswekwe ndani? Kutimiza ahadi uliyoahidi wakati wa kampeni sio tatizo.
 
Kuna tetesi hapa A town kuwa Nassari anaandaliwa zengwe la kufikishwa mahakamani eti kwa kuchimba visima alivyoahidi wakati wa kampeni bila kibali cha serikali. Magamba wanadai ni kitendo cha rushwa ndiyo maana amechaguliwa. Mwenye habari zaidi atujuze. Magamba wanazidi kuweweseka. Chanzo minong'ono mtaani

Rushwa ya aina gani hiyo.. Hawa jamaa akili yao ipo kwenye kisigino nini?....

Muda naona unakaribia wa kuitoa CCM Madarakani kabla ya 2015.... Kama wanataka kuona Peoples power wajaribu..
 
Kuna tetesi hapa A town kuwa Nassari anaandaliwa zengwe la kufikishwa mahakamani eti kwa kuchimba visima alivyoahidi wakati wa kampeni bila kibali cha serikali. Magamba wanadai ni kitendo cha rushwa ndiyo maana amechaguliwa. Mwenye habari zaidi atujuze. Magamba wanazidi kuweweseka. Chanzo minong'ono mtaani

Ulitokea mzozo kidogo kuwa mwenyekiti Wa Serikali ya mtaa alikuwa akigoma kudondoka saini ili visima visichimbwe kisa hakijulijani,wananchi kwa umoja wao walitoka huko walikokuwa baada ya kupata taarifa hizo na kwenda ktk ofisi hizo kushinikiza mwenyekiti huyo afanye kile kimemuweka ofisini.
 
mm nafikir tusiumize vichwa, kama wanadai alichimba wakati wa kampeni basi wamfungulie mashtaka hayo na hapo ukweli utajulikana kama alita rushwa au alikuwa anatimiza ahadi zake. kwa mujibu wa taarfa nilizopata ni kwamba visima vilianza kuchimbwa siku 2 tu baada ya matokeo ya uchaguzi.

ngojeni niwaambie kitu hivi unaja kwa jinsi tulivyochoka jani la mgomba ni wazi kuwa hata ahadi wa peples power sisi tunaweza kuzisaidia zitimie kusudi tu tuwapin down?wasijisumbue ila ukweli ni kwamba wananchi walianza kuchimba ili kuonyesha kuwa NASSARI ni mtu anayetimiza ahadi na yeye alikuwepo wakati huo. na wala haikuwa wakati wa kampeni bali baada tu ya matokeo ya uchaguzi.
 
Tetesi hizo ni za uwongo, Sioi slimpongeza na alisema hatakwenda mahakamani au unataka kusema anataka kutumia watu kama ilivyokuwa Arusha?
 
Ninachowapendea jamaa zangu wa Chadema wana umoja sana hata kwenye habari za udaku uwa wanakuwa kitu kimoja.
 
Yesu aliwauliza wayahudi ''Ni nani kati yenu Punda wake akitumbukia shimoni siku ya Sabato ataacha kumtoa kwa kuwa ni sabato??'' Nami nawauliza magamba, ni nani nje yenu atakubali kuwaona wananchi wakiendelea kunywa maji taka hata miaka 50 baada ya uhuru? Nassary hakubaliani na huu ujinga ndio maana ameamua kuwakomboa wananchi, hata muhonge mahakimu na majaji wote ukombozi utakuja tu.
 
Kuna tetesi hapa A town kuwa Nassari anaandaliwa zengwe la kufikishwa mahakamani eti kwa kuchimba visima alivyoahidi wakati wa kampeni bila kibali cha serikali. Magamba wanadai ni kitendo cha rushwa ndiyo maana amechaguliwa. Mwenye habari zaidi atujuze. Magamba wanazidi kuweweseka. Chanzo minong'ono mtaani

Rushwa baada ya uchaguzi siyo rushwa inaitwa Ahadi za uchaguzi.
Hata kikwete mbona anaendelea kutoa rushwa?
Kikwete naye afikishwe mahakamani kwa kuahidi kujenga barabara.
 
Mfa maji bwana haishi k.........?hawa dawa kuwachuna magamba tusisubiri wajivue,peoples p.,
 
Back
Top Bottom