Nassari: Kanisa la KKKT - Dayosisi ya Meru lina miradi ya maendeleo kuliko serikali

Sikonge City

Member
Jul 15, 2012
68
14
Akiongea katika mkutano mkuu wa 10 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Meru uliofanyika Ngarenanyuki, Mheshimiwa Nasari alitoa pongezi kwa kanisa hilo kwa juhudi zake za kuleta maendeleo ya jamii, akiorodhesha wingi wa miradi hiyo Joshua alisema Miradi ya Kanisa ni mingi kuliko hata ya Serikali.

Amesema anaungana na juhudi za kanisa hilo na kwa kuanzia yupo njiani kukamilisha taasisi yake ambayo kuanzia mwakani 2013 atasomesha vijana 400 shule za sekondari, ili kuinuia kiwango cha elimu Meru.

Pia amemtaka Baba Askofu Paul Akyoo na wana meru wote wamuombee kwani wabunge wapo kwenye kipindi kigumu, kuna fitina, chuki,masengenyo na uadui wa hali ya juu.

Akimpongeza Askofu Akyoo alimuhakikishia kuwa amebadilika na anaongea vitu vyenye maana na point nao wataendelea kumuombea.
Katika ibada hiyo pia alihudhuria mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na Mkurugenzi AICC Ndg. Elishilia Kaaya, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya kanisa hilo.

Pia alikuwepo Diwani wa kata ya Maji ya Chai CCM na Kaimu katibu mkuu wa kanisa hilo Ndg. Loti Nko.

Mwisho Mbunge huyo ametakiwa kutafuta mchumba na kuoa, jambo ambalo aliambiwa na Asf akyoo, naye alisema ameishaanza mchakato huo aombewe tu.
 
Huyu dogo kina Mbowe wasipokuwa makini ndio atakayeizamisha Chadema sasa sijui kama anafahamu hiyo miradi ya Kanisa fedha nyingi zinatoka serikalini.
 
Huyu dogo kina Mbowe wasipokuwa makini ndio atakayeizamisha Chadema sasa sijui kama anafahamu hiyo miradi ya Kanisa fedha nyingi zinatoka serikalini.

kah!serikali ina fedha nyingi tena?mbona imesema haina fedha za kuwalipa madaktari na walimu?ni kwa nini serikali itoe fedha nyingi kwa kanisa badala ya kuelekeza fedha hizo kwa miradi ya maendeleo kwa kutumia mifumo ya kiserikali?
 
Ndio maana Mh Ndugai alisema yale maneno, naanza kuamini kuanzia sasa hivi.
 
Kumbuka hilo sio kanisa katoliki ni lutheran
Huyu dogo kina Mbowe wasipokuwa makini ndio atakayeizamisha Chadema sasa sijui kama anafahamu hiyo miradi ya Kanisa fedha nyingi zinatoka serikalini.
 
Back
Top Bottom