Nassari Backlash on Sera ya Majimbo- It seems CCM CADRE ARE SCARED TO DEATH! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nassari Backlash on Sera ya Majimbo- It seems CCM CADRE ARE SCARED TO DEATH!

Discussion in 'Great Thinkers' started by George Maige Nhigula Jr., May 10, 2012.

 1. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana Jamii ya wazalendo,

  Ni dhahiri kabisa sera ya majimbo ya chadema yenye lengo la kurejesha mamlaka kwa wananchi, na kuondoa mamlaka ya wateule wachache kama wakuu wa mikoa na wilaya ambao wamekuwa wakiteuliwa kwa kulipana fadhila na kupeana ulaji bila ya kuwa na ridhaa ya wananchi na uwajibikaji wa moja kwa moja kwa wananchi imekuwa tishio kubwa kwa makada wengi wa chama cha mapinduzi. ambao wengi wao wamekuwa wakisubiri na kujipanga kupata ulaji wa chee bila kuwa na uwajibikaji wowote kwa wananchi.

  Wimbi tunaloliona kwa viongozi na makada wengi wa ccm kujitokeza na kutumia statement ya Nassari Joshua ambayo ilikuwa poorly phraised! na ambayo mwenyekiti wa chama Taifa Mh. Freeman Mbowe kuitolea ufafanuzi pale pale NMC na kuweka kumbukumbu sawa kuwa huo sio msimamo wa chama. Hii inaonesha kuwa wana ccm wengi wamepata kisingizio cha kuibeza na kuiponda sera ya majimbo ambayo ndiyo njia sahihi ya kuleta uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali zetu vizuri.

  Hii sio bahati mbaya kwa makada wa ccm to tie statement ya Nassari(Dogo Janja) Na Sera nzuri ya majimbo, kwani sisi sote tunajua kuwa wana ccm wengi hawaitaki sio kwa sababu ni sera mbaya la hasha! bali inakwenda kuondoa ulaji wa kupeana ukuu wa wilaya na mkoa ambao wengi wamekuwa wakipigana vikumbo kwa kujipendekeza au kufanya kila hila ili wateuliwe.

  Hali kadhalika sera ya majimbo itahamisha mamlaka mengi kutoka serikari kuu na kurejesha majimboni ambako watanzania ndio wanaishi, na watanzania wenyewe watapata fursa ya kuwachagua ma governor na leutenant governor, hivyo uwaziri hautakuwa na deal tena na wizara zitabaki kuratibu sera tu! kwa nani hajui kuwa watu wengi wanakimbilia kugombea ubunge ccm ili wawe mawaziri?

  Hivyo lazima watanzania tugundue nia ovu ya chama cha mapinduzi kuipiga mbao sera ya ya majimbo kwa mwamvuli wa kuepuka mgawanyiko wa nchi, hicho ni kisingizio ambacho hakina msingi, mbona hivi sasa tuna mikoa zaidi ya 25 na hakuna mgawanyiko sasa tukigawa majimbo ambayo yatakuwa yanajumuisha zaidi ya mikoa mitatu, huo mgawanyiko utatoka wapi?

  Ningependa sana kuona makamanda hususani viongozi wakuu wa chama wakaipigania sera hii kwa kutoa elimu kwa umma inayoeleweka, siyo hivi sasa walivyoiacha hewani ina ning'inia bila base na facts za kutosha, la sivyo kwa mwendo huu wa magamba kuposha wananchi wakati wao magamba wanajua fika kuwa SERA YA MAJIMBO ndo mwisho wa ulaji na vyeo vya kupeana.

  TUIPIGANIE SERA YA MAJIMBO KWA MAENDELEO YA NCHI YETU, UWAJIBIKAJI NA KUREJESHA MAMLAKA KWA WANANCHI,TUSIKENGEUSHWE NA DOGO JANJA BACKLASH!
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MJADALA NA UTOAJI MAONI HATA YALE YASIOKIPENDEZA CCM NI SHARTI KUPEWA UHURU WOTE UNAOSTAHILI BILA BUGHUDHA WALA VITISHO NDIPO KATIBA MPYA UTAKAPOWEZA KUPATIKANA KWA MURUA NA USHWARI

  Kama swala dogo tu la Mhe Nassari kusaidia kuibua mjadala mzito kitaifa ndio kama hivi inaonyesha kukitetemesha CCM hadi mfupa wa mwisho mwilini, je mijadala mizito ya Katiba Mpya tunayokusudia kuanzisha kote nchini hivi karibuni sasa chama hiki huenda kinapanga kufunga wangapi ili maoni yao yasisikike umbali wa pua zao wenyewe?

  Waheshimiwa Wana-CCM mliosalia katika jumba hilo hapo Chimwaga, napenda niseme hivi; Swala la katiba mpya lisiposhughulikiwa kwa akili zilizotulia, utaifa uliokomaa na busara zisizo mawaa;

  ... kuna uwezekano mkubwa taifa likapigwa dhoruba na mawimbi makali kushoto kulia bila kumletea mtu na au upande wowote mavuno ya kheri huko tuendako.

  Hili ni letu sote tukalifnyie kazi bila hila wala itikadi ndipo tupate kufika salama kama jamii moja wenye sababu zote kushikamana katika HAKI, MAJADILIANO, USHIKISHWAJI KWA KILA HATUA, NA UWAZI.
   
 3. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Ninaota jimbo kubwa na tajiri la kusini nyanda za juu-mbeya,iringa na rukwa linafuata sukumaland-mwanza,shinyanga na tabora. Wakwe.re mtakula jeuri yenu
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hakuna Nassari backlush wala explosion. CCM wameona wameshindwa na sasa wanaanza witch-hunt. Sera ya majimbo si kuigawa nchi kwani nchi iliisha unganishwa na Mwalimu. Sera ya majimbo ni njia pekee ya kuongeza mwendokasi wa maendeleo. Mtu mmoja kukaa magogoni akiendesha nchi kwa remote control ni sababu kubwa sana kufanya viongozi wa chini kutokuwa kuwa wabunifu. Kila wanalolifanya wanajiuliza mara mbilmbili je litamfurahishwa 'bwana mkubwa' ?

  CCM wanaposhindwa kuzishikia bango kauli za kina Jusa Ladhu na kuanza kum-demonise kijana mdogo asiye na uzoefu kwenye siasa ni dalili za disperate na hazitawasaidia na wimbo la mawazo ya kimageuzi lililojikita miongozi mwa majority ya watanzania.

  Hizi kelele zao ni sawa na mtu mwenye 'terminal desease who takes painkillers' while waiting for the death in peaceful manner.
   
 5. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,215
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280
  Tatito ni kwamba sera ya majimbo inakuwa misinterpreted na CCM. Hivi kwa nini wasiwaulize waziwazi CMD kwamba hiyo sera ikoje na inafanyaje kazi? Mbona majimbo ya Marekani yana sheria zinazotofautiana kidogo lakini bado Marekani ni moja?
   
 6. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Sera ya majimbo itapunguza wizi wa fedha za wananchi maana makusanyo yote yanakuwa controlled na uongozi wa jimbo kabla ya kuwasiliana na serikali kuu. Sasa CCM wamezoea kuzichota hazina ambako ndo kapu la fedha zote.
  Wakilifikiria hili, wanaamua kuwaongopea watanzania.
  Yana mwisho lakini
   
 7. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,677
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  Kama Nigeria, Congo ..... majimbo siyo dawa ya uwajibikaji. Ni njia ya waliokosa kura kupata mamlaka through divide and rule. Tupo wengi tunaopinga hili, let the ballotbox speak.
   
 8. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Kinachowasumbua ni kutaka kuendeleza failed legacies za Nyerere. Kwanini kushindwa kwa majimbo tutumie mifano ya Congo na Nigeria tu?Nchi karibu zote zilizoendelea zina Majimbo. Kwaninj basi msitaje hizo nchi?
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Zakumi,

  ..mimi naogopa nchi hii kuwa na serikali 13.

  ..serikali 3[znz,tgk,muungano], halafu hayo majimbo 10 yanayopendekezwa.

  ..I will be interested kumsikiliza mtu atakayekuja na idea ya kupunguza ukubwa wa serikali tuliyonayo, na wakati huohuo kuifanya iwe more efficient.

  ..mambo haya ukiwaachia wanasiasa wayazungumze basi siku zote watakuja na mbinu za kujiongezea ulaji tu.
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Jul 9, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nadhani swala hili kila mmoja wetu atalitazama kwa sura ya kutumia mifano ya nchi nyinginezo ama kutumia vitabu (elimu) lakini nadhani ni bora zaidi tujitazame sisi wenyewe tulipo kisha tutazame faida na athari zake na jinsi gani zinaweza kurekebishwa ama kuondolewa maana lengo ni kusonga mbele ktk maendeleo.

  Serikali ya Majimbo ni sera ya Chadema ambayo kwa bahati mbaya sana inatazama nchi nyinginezo. Kuna Uzuri wake na ubaya wake lakini kabla hatuja hukumu lolote ni vizuri zaidi kujipima sisi wenyewe. Tusimame mbele ya kioo na kujitazama who we are, where we at, na wapi tunataka kwendaKujitazama kiooni na kujitambua kabla ya maamuzi kufanye nini?

  Kuna kijana hapo juu kazungumza na kueleza majimbo yatakayo endeleo na majimbo ambayo yataachwa nyuma..tena kwa kusisitiza WAKWERE watakula jeuri yao. Je, hii ndio sura halisi ya Mdanganyika? Hivi kwelitunataka mgao sawa wa keki ya taifa ama tunataka kuchagua kundi la watu gani wanaostahili kupata kipande kikubwa cha keki hiyo..

  Hii ni hatari kubwa sana kisiasa yaani mfumo unaundwa ili kuwadhalilisha wengine na hasa Wakwere sijui kwa sababu ya JK ambaye hakuuweka mfumo huu, naye kaukuta na atauacha.. Ikiwa sera ya Majimbo inatokana na hisia za watu kuona majimbo fulani hayafaidiki na keki ya Taifa hivyo solution ni kuunda majimbo ambayo yatawapa nafasi kubwa ya kufaidika na mali zao.. Hapa yanajitokeza maswali mengi magumu zaidi.

  1. Hoja kubwa ya Muungano kuhusu Mafuta.. mathlan Mafuta yamepatikana Tanga, haya mafuta yatakuwa ya serikali ya muungano ama yatakuwa ya jimbo hilo hata kama mkopo umetolewa kwa Tanzania?.. Maana tukumbuke jimbo pekee haliwezi kuchukua dhamana ya kupewa mikopo mikubwa ya kimataifa unayohusu rasilimali za kitaifa kama hizi..Miradi ilokwisha wenkezwa kama Buzwagi, Songos, Makaa ya mawe na kadhalika itakuwa mali ya nani?.. ikiwa tunalipa watanzania wote deni lake.

  2. Uongozi wa haya Majimbo utafanyika vipi, Je kiongozi wa jimbo moja anaweza kwenda kugombea jimbo jingine japokuwa yeye ni mkazi wa Dar?..Kutokana namfumo uliopo viongozi wengi wanaishi majimbo wasiyowakilisha na wana Uhuru wa kuhama na kuendelea na nyadhifa zao. Je, mfumo wa Majimbo utawalazimu viongozi kuishi ktk majimbo yao? ni uhalali upi utatumika kumkubali mgombea kuwa mkazi au raia wa jimbo husika ikiwa leo Tanzania kila mtu anagombea anapotaka, kuishi anapotaka na kupewa transfer kona zote za Jamhuri.. Ni vigezo gani vitatumika kutenganisha jimbo haddi jimbo.

  Binafsi yangu pamoja na kwamba kuna haja kubwa sana ya kuondoa mfumo huu uliopo ambao unategemea serikali kuu kuepeleka maendeleo mikoani. Ni mfumo dume, mfumo unaowalazimisha wananchi wapiga kura kuchagua chama tawala laa sivyo watakosa maendeleo. Na hii imetumika sana toka tumeingia demokrasia na kwa bahati mbaya sana watu wameshindwa kuelewa kwamba mikoa yote ambayo haikuwachagua CCM toka 1995 ndio mikoa iliathirika zaidi.

  Kusini ambako kulikuwa ngome ya CUF wameathirika sana hadi majuzi ndio tunaona maendeleo yakisogezwa sogezwa. Mikoa ya Nyanda za juu na hasa Kilimanjaro imefaidika tu kwa sababu kuna viongozi wengi Wachanga ndani ya serikali ya CCM ambao wameshinda nafasi tofauti za kiutawala, hivyo kwa kutumia mapenzi yao ya asili kwa mkoa wao ndio tumeona mabadiliko haswa wakati Mbowe alipogombea Urais, wakazoa baadhi ya majimbo...

  Hakika Wabunge wa vyama vya Upinzani wana wakati mgumu sana ktk mfumo huu, hawa wanalazimika kupiga magoti kuiomba serikali ipeleke maendeleo majimboni mwao na sii kwamba fedha tayari ziko alllocated ktk majimbo hayo bali Waziri ndiye mweye kiroba chote na hutazama wapi na afanye nini au laa halazimiki.. He can easly explain tomorrow kwa nini sehemu fulani hawakufanikiwa maadam ktk umaskini huu sababu ziko nyingi. Bila mbunge kumbembeleza na kumlamba miguu Waziri au Naibu hutoka mtupu na haijalishi kuna umuhimu gani kwa wananchi wake..

  This is Sonething has to be done against Bureaucracy.. Na ushauri wangu baada ya kuwasoma Wadanganyika na hasa uongozi ulochoka na dhaifu. hakuna njia zaidi ya kupeleka madaraka mikoani. Acha mikoa ichague wakuu wake wa mikoa, wabunge, madiwani, Mameya na viongozi wote wa Halmashauri na serikali za mitaa ambao watawajibika kwa mkuu wa mkoa Regional Commision ambaye atakuwa kama Gawana na mwakilishi wa chama kilichoshinda. Uongozi wa serikali hii utatokana na nusu au zaidi ya pato la kodi walizokusanya ktk mkoa kila mwaka.. na nusu nyingine itapelekwa ktk serikali kuu ambayo itahudumia miradi na madeni ya Kitaifa ktk maendeleo.

  Na serikali kuu itawajibika kuepeleka maendeleo mikoani kutokana na pato la uwekezaji ktk miundombinu na miradi ya Kitaifa hivyo Mafuta yaliyopatikana Tanga itajulikana kwamba nusu ya pato lake litakwenda mfuko wa Taifa na kuingia ktk miradi ya kitaifa na kulipa madeni..Lakini umuhmu wa mfumo huu ni kuufanya mkoa unaozalisha zaidi kufaidika na rasilimali yake tofatui na kuwepo majimbo kutatulazimisha kesho mkoa wa Tanga kutaka kujitenga na jimbo kwa sababu wao ndio wenye Mafuta na wanaendesha uchumi wa jimbo..Sii rahsi kwa Tanga kujitoa ktk serikali kuu kwa sababu haina uhuru kamili wa Kitaifa..

  Kuiga serikali za Majimbo kuna athari zake maana ikumbukwe tu kwamba wenzetu waliunda majimbo yao kama sisi tulivyounda muungano wetu na Zanzibar.. majibmo hayo yalikuwa huru na yenye mamlaka kamili yakaungda UMOJA ili kujenga nguvu kubwa ya kiuchumi tofauti na sisi tunataka kuunda majimbo kwa kuigawa nchi vipande japokuwa tuna UMOJA hivyo tutauondoa UMOJA wetu.

  Kwa akili za Wadanganyika hii itakuwa mwanzo wa Ukabila, Udini na hata vita maana hili la Zanzibar tu na halali ya kuwepo majimbo mawili inatushinda..Kama hatuna solution na swala la Muungano itakuwaje rahisi tukate majimbo na uwapa mamlaka kamili ya kuunda serikali na bunge?..
   
 11. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Mkandara
  Kabla sijachangia, kuna makosa nikisema kwamba, umefanya tasmini kwa kuangalia vitu vilivyoko kwenye majimbo badala ya watu walioko kwenye majimbo?
   
Loading...