Nassari amwambia Ndugai, ubunge hauondoi ubinadamu au majukumu ya kifamilia, hajutii kufukuzwa ubunge

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,274
47,339
Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru, Joshua Nassari amesema kuwa ni kweli Mwezi Novemba 2018 na Januari 2019 hakuhudhuria Bunge kwa kuwa alikuwa na matatizo ya kifamilia

Ameeleza kuwa mke wake alikuwa na matatizo ya kiafya ambapo alihitaji uangalizi wa karibu wa kifamilia na kitabibu kutoka nje ya nchi ambapo alikuwa naye nchini Marekani akipata matibabu hayo

Mnamo Januari 27 mwaka huu, mke wake alijifungua mtoto huku nchini Marekani na kesho yake Januari 28 vikao vya Bunge vilikuwa vinaanza na kumuacha na machaguo mawili, kuhudhuria Bunge au kumuuguza mke wake

Anasema alichagua kumuuguza mke wake lakini aliandika barua kwenda kwa Spika kupitia anuani aliyopewa na Msaidizi wa Spika ili kumueleza matatizo anayopitia yeye na famialia yake na kushindwa kuhudhuria Bunge

Aidha, amefafanua kuwa ana haki ya kuulizwa au kuhojiwa na ofisi ya Bunge kuulizwa kulikono na pia anamini kuwa Spika kama mzazi au mlezi wa Bunge ana uwezo wa kurejea maamuzi yake

Mwisho huku akisisitiza kuwa hajutii uamuzi aliochukua ameeleza kuwa asipopata haki yake ataitafuta popote ikiwa ni kuanzia Mahakamani

Inaripotiwa atatua Mahakamani Hili Ni jambo jema:Hatua nzuri na ya maana zaidi.
Leo P habari
Screenshot_20190317-121049.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha ubwege wewe

In God we trust
Mkuu siyo ubwege. Tuweke siasa pembeni. Huyu mbunge hakufanya vizuri na hakufuata taratibu! Japokuwa nina uhakika kuwa angekuwa ni wa CCM asingefukuzwa, lakini siwezi kutetea uzembe. Mtu ukijua kuwa unaishi kwenye msitu wenye wanyama wakali ni lazima uchukue tahadhari. Halafu kuna kuongopa kwa kusingizia kuuguza wakati kuuguza hakukuwa sababu halisi!
 
Dharura ya kuuguliwa na mke ni kubwa na ya msingi.
Tatizo ni kuwa je aliomba na kupewa ruhusa ya Spika kama sheria na kanuni zinavyotaka au alijisepea tu???

Pia kuna mtu anaweza pata msiba wa mzazi, mwenzi au ndugu wa damu.
Huwezi toweka kazini kwa wiki moja kisa ulikuwa na msiba. Unahitaji kuomba na kupewa ruhusa hata kama msiba ulikuwa umetangazwa kwenye vyombo vya habari kama ule ya Ruge (May he rest in peace).
Utaratibu ni kupata ruhusa. Kujiruhusu ni utovu mkubwa wa nidhamu hasa kwa kiongozi.

Je alipata ruhusa au alijiruhusu?
Mh. Mbunge akitufafanulia hili itakuwa vizuri. Watu tushaanza kumuundia bifu Ndugai...hebu atupe mwanga kidogo tufanye yetu.
Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru, Joshua Nassari amesema kuwa ni kweli Mwezi Novemba 2018 na Januari 2019 hakuhudhuria Bunge kwa kuwa alikuwa na matatizo ya kifamilia

Ameeleza kuwa mke wake alikuwa na matatizo ya kiafya ambapo alihitaji uangalizi wa karibu wa kifamilia na kitabibu kutoka nje ya nchi ambapo alikuwa naye nchini Marekani akipata matibabu hayo

Mnamo Januari 27 mwaka huu, mke wake alijifungua mtoto huku nchini Marekani na kesho yake Januari 28 vikao vya Bunge vilikuwa vinaanza na kumuacha na machaguo mawili, kuhudhuria Bunge au kumuuguza mke wake

Anasema alichagua kumuuguza mke wake lakini aliandika barua kwenda kwa Spika kupitia anuani aliyopewa na Msaidizi wa Spika ili kumueleza matatizo anayopitia yeye na famialia yake na kushindwa kuhudhuria Bunge

Aidha, amefafanua kuwa ana haki ya kuulizwa au kuhojiwa na ofisi ya Bunge kuulizwa kulikono na pia anamini kuwa Spika kama mzazi au mlezi wa Bunge ana uwezo wa kurejea maamuzi yake

Mwisho huku akisisitiza kuwa hajutii uamuzi aliochukua ameeleza kuwa asipopata haki yake ataitafuta popote ikiwa ni kuanzia Mahakamani
 
Kwani kawajibu wananchi au Spika?

Jr

Nakuheshimu sana kaka mshana Jr.Katika hili hata kama amemjibu spika basi hata wananchi wake waliomchagua majibu hayo yanawahusu,hivi jiulize katika utoaji wa huduma kwa jamii kila mtumishi akiwa na excuse za kifamilia nchi inaweza kusonga mbele?
Jibu hapana;Na ndo mana kuna utaratibu wa kufuatwa ili kudhibiti mambo kama haya.
Kuna ofisi za umma uki miss kazini hata siku 3 bila sababu ya msingi tambua hauna kazi

iPhone 7plus
 
Ameeleza kwamba alishiriki kikao Cha septemba na January alimwandikia speaker Barua inayosambaa mitandaoni ya tarehe 29/01/2019 baada ya kusahauri na msaidizi wa spika afanye hivyo.

Ameeleza kwa uchungu matatizo ya ndoa kuhusu mke wake kupata changamoto za uzazi lakini alifanikiwa kujifungua tarehe 20/01/2019 nchini Marekani.

Ameeleza asingeweza kumwacha mke wake mgonjwa akawahi bungeni kusaini posho.

Ameeleza kuwa Kama mume responsible angemwangalia kwanza mke na siyo kumwacha hospital akimbilie bungeni.

Ameeleza kuwa hajawahi kuitwa na kuhojiwa kabla ya kufukuzwa ubunge.

Toka spika aandike bariua hiyo amempigia simu inaita haipokelewi na hata alimtafuta msaidizi wake alimweleza atamjulisha spika kuwa Nassary anampigia lakini hakuna response ya spika.

Amehoji Nini kipo nyuma ya pazia mbona wapo wabunge wengi wapo nje ya BUNGE na wengine wanauguza kwa MUDA Sasa na hawajavuliwa ubunge?

Ameeleza dhamira ya kwenda kutafuta haki mahakamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom