Nassari alikana Mwananchi kuhusu Zitto na Urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nassari alikana Mwananchi kuhusu Zitto na Urais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngurati, Jul 23, 2012.

 1. n

  ngurati JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Katika barua yake kwenda kwa mhariri mtendaji mkuu wa Mwananchi. Hii ni sehemu ya waraka huo wa Nassari.


  Nukuu hiyo si ya kweli. Nimesikitishwa sana na upotoshaji mkubwa wa kunilisha maneno mdomoni uliofanyika katika sehemu kubwa ya habari hiyo (mbali na nukuu hiyo) kwa maslahi ambayo sijui ni ya nani.

  Wakati ukijiandaa kuchukua hatua kutokana na sababu ya pili ya kukuandikia barua hii ambayo nitaieleza punde hapa chini, naomba utafakari masuala kadhaa, ikiwemo; kwa nini ilichukua siku zaidi ya tano kwa habari hiyo kuandikwa?

  Pili, kutokana na usumbufu mkubwa ambao nimeupata kutoka kwa Watanzania wa maeneo mbalimbali wanaotarajia kuniona mwakilishi wao nikizungumzia masuala yanayowahusu wao, ambayo ni muhimu zaidi kuliko jambo jingine lolote kwa sasa.

  Lakini pia nikiwa Mtanzania anayetambua umuhimu na unyeti wa nafasi ya urais katika nchi hii na kwamba inaamuliwa kwa maslahi mapana ya umma wa Watanzania wala si uchu wa watu wachache, hivyo nisingeweza kutamka maneno hayo ambayo gazeti lako limeandika, naomba kukuandikia rasmi kukutaka ukanushe habari hiyo ukurasa wa mbele kwa uzito huo huo ulioipatia habari hiyo katika toleo tajwa.

  Lakini pia nikiwa Mtanzania ambaye ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho kinaamini kuwa kwa sasa suala la urais si kipaumbele, bali muhimu kwa wakati huu ni kushughulika kujua mizizi au vyanzo vya matatizo makubwa yanayowakabili Watanzania ikiwemo umaskini, ujinga, maradhi, ufisadi na utawala mbovu wa CCM, kwani serikali imekuwa ikishughulikia matokeo.

  Kama ambavyo chama changu, Watanzania wengine makini na mimi mwenyewe, naamini kuwa kwa sasa suala la muhimu kwetu kama taifa ni kutafuta mizizi au vyanzo vya matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya Watanzania.

  Kwa chama changu na mimi mwenyewe pia kama mwakilishi makini wa Watanzania, naamini kuwa siku zote suala la urais linategemea mahitaji ya Watanzania na kamwe haliwezi kuamriwa kwa kufuata matakwa na utashi au uchu wa watu binafsi.

  Lakini pia suala la nikiwa kama mwanachama mwaminifu wa CHADEMA na ninayeipenda nchi yangu kwanza, naamini kuwa suala la urais linafuata katiba, kanuni na taratibu za chama, hatua ambayo haijafikiwa kwa sasa.

  Naomba kusisitiza kuwa sijawahi kutamka, siwezi kutamka na sitarajii kutamka maneno hayo uliyoyaandika kwenye gazeti tena kwa kuninukuu na kuniwekea maneno mdomoni. Naomba kurudia tena kukutaka ukanushe habari hiyo ukurasa wa mbele kwa uzito huo huo ulioipatia habari hiyo katika toleo tajwa.
   
 2. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mbunge wa Arumeru leo ni mara yako ya pili kuikana taarifa yako, ulishawahi kuikana taarifa ya kuitenga nchi na kuanzisha taifa la Kaskazini, pia ukasema Vijana mtatembea kwenda Ikulu...

  Leo umelazimishwa kumkataa ZITTO kwa kushinikizwa? kuna siku utajasema Rais umtakaye ni kutoka hukohuko Kaskazini.

  Mimi binafsi ni shabiki wa ZITTO kwa vitendo 100% hata mkimchukia kwa Kabila lake au Dini na hukatazwi kumshabikia yoyote kwenye nchi hii bila kujali chama
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Slaa mpaka kaoa ili mipango yake ya kua rais ikamilike yule gwiji atawapiga chini hao akina zitto
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi kweli kwanini imechukuwa siku 5 kwa Mwananchi kuandika hii habari? Mkutano wa Kigoma ulifanyika week iliyopita, kwanini imewachukuwa muda wote huo kuandika hiyo habari?
   
 5. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nikiwa kama mwandishi wa habari, nimewahi kuandika humu ndani tabia chafu za mbunge Zitto Kabwe.

  Zitto anajiandikia habari, analazimisha ichapishwe bila kufanyiwa uhariri. Katika watu watakaoliingiza hili taifa katika hatari, ZITTO ni mmoja wao.

  Anafikia kuwahonga waandishi ili waandike habari zake na ziwekwe ukurasa wa mbele. Uongozi haulazimishwi, uongozi ni kazo watu wanapewa na wapiga kura. Jipangeni kuhusu Zitto.

  Kazi nzuri Nassari, CCM- Inamsadia zitto kwenye hizi propaganda za kuvuruga CHADEMA
   
 6. TODO

  TODO JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  dogo aangalie siasa ya bongo hapa ni pasua kichwa.kesho wakikuwekea maneno uliyoyasema utafanyeje?
   
 7. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,496
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  We ulitaka Nasari akubali tu kila linalozushwa kuhusu yeye!!...na ukaonge na utoto ..eti kalazimishwa kukanusha!! kwa

  ujinga wenu huu hamtafanikiwa!

  .....Ndugu yangu kwa umri wako huu na elimu yako hii ya kuja kusoma na kuandika....

  Unakosea sana kusema maneno kama hayo ya kuwa wewe ni mshabiki mpenzi wa Zitto!!

  Kwenye siasa hamana kitu kama hicho!! Nyie ndio mlikuwa mashabiki wa JK sasa hivi mnalia/tunali!!

  Uraisi hatubahatishi....hata kama mtu anapenda sana kuwa raisi na wewe unamshabikia kama mpenzi wako...lakini lazima

  tujiulize mara mbilimbili anaweza????
   
 8. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mwananchi wana agenda gani kwenye hili? Kwani magazeti mengine hayakuwa na wawakilishi siku ile? Siku moja tutafahamu nani yupo nyuma ya haya yote.
   
 9. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,496
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  Muke ya Musungu, umenena vema!

  Hizi tabia alikuwa nazo pi JK..kujipendekeza saaana na kutumia vyombo vya habari kujipalilia!
   
 10. makusanya

  makusanya JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Mh!hii sasa mbwa kala mbwa.nani mkweli nan si mkweli vitajulikana tu
   
 11. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Mwananchi na Zitto, hii si mara ya kwanza kuleta vioja.
   
 12. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Niliwai kusikia Zitto ana urafiki na mhariri wa Mwananchi Denis Msaki.
  gazeti la Mwananchi siku hizi naona linapoteza mvuto kutokana na habari zake.
   
 13. I

  Incredible JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 937
  Likes Received: 963
  Trophy Points: 180
  Juma lilopita nimesoma nadhani humu JF au gazetini kwamba mikakati ya EL kwenda ikulu inaambatana na magazeti kadhaa kununuliwa, wabunge na spika, pamoja na Chadema kuvurugwa. Naona mchezo umeanza tayari. Tutaona mengi.
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  hiyo ni kweli
   
 15. M

  MI6 Senior Member

  #15
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ikitokea hii ikawa ni njama ya CCM kuivuruga CHADEMA kupitia Zitto ntaamini magamba noma aiseee
   
 16. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  zito na ccm wana lao moja. Wanataka kusingizia udini kwamba ndo uliomfanya abaguliwe kugombea. Kuwa muislamu au mtu wa kigoma hukumfanyi apendelewe ili wananchi wasiiseme cdm!! Hii mizizi ya udini ambayo zito anashirikiana na watu waliojazana ccm kutaka wao ndio waenelee kupendelewa itatupeleka kubaya. Watu wanapokanusha taarifa zenu msikimbilie kwenye ukabila na udini!!
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Hakuna gazeti lingine lolote lililo-report hiyo habari?
   
 18. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2012
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Ila mmhhh! Zimepita siku tano ndio leo Mwananchi waandike, tena kama lead news! Something fishy here! Tutasikia mengi kuelekea 2015.

  Bado Mwananchi ni gazeti langu pendwa, ila msinikatishe tamaa kwa manyuzi yenye utata kama hii ya leo.
   
 19. M

  Molemo JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kuna mwandishi anaitwa Ramadhan Semtawa wa Mwananchi yeye ana kazi moja tu kuvuruga CDM kwa maslahi ya CCM.Nilivyoiona tu hiyo habari leo mwananchi nikajua kwa vyovyote Nassari hawezi kutamka Upumbavu kama ule.Ile ilikuwa habari ya kimbeya na kishenzi sana kuhusu CDM.
   
 20. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  hakuna gazeti lingine lililo-ripoti habari hii.
   
Loading...