Nassari akisindikizwa na Kangi Lugola kutoa Shukrani Kanisani!!

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765

Mbunge Joshua Nasari na Kangi Lugora wakitoa shukurani zake kanisani.

Gladness Mushi wa Full shwangwe -Arusha

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari leo amefanikiwa kutoa sadaka ya shukurani katika kanisa la FPCT Kilinga wilayani meru mara baada ya kuchaguliwa kama mbunge wa jimbo hilo

Akiongea na Mamia ya wananchi wa jimbo hilo katika kanisa hilo Bw Nassari alisema kuwa ameamua kutoa sadaka maalumu ya kushukuru mungu mara baada ya kumaliza vema uchaguzi huku wapiga kura wake wote wakiwa salama tofauti na pale ambapo wengi waliadhimia

hata ivyo aliwataka viongozi wa vyama vingine kuhakikisha kuwa wanakuwa mstari wa mbele kutetea maslahui ny6a wananchi na kuachananna tofauti za kivyama ambazo kama zitaendelezwa basi zitachangia kwa kiwango kikubwa sana umaskini wa Meru

Akiongea katika kanisa hilo kwa ajili ya ibada hiyo mchungaji Langaeli Kahaya naye alisema kuwa wananchi wanapswa kuhakikisha kuwa kamwe hawamchagui kiongozi yoyote kwa ajili ya maslahi ya Rushwa kwa kuwa wote wanaotoa rushwa ndio wanaosababisha hata umaskini na umwagaji damu ndani ya nchi

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni mwiko kwa wananchi wma Jimbo la Arumeru Mashariki kujihusisha na Rushwa kwa vipindi vyote vya uchaguzi kwa kuwa mpaka sasa Rushwa imeshaacha madhara makubwa sana ndani ya jimbo hilo na pia Rushwa ni dhambi kubwa sana.
 
sijapata sababu ya uwepo wa huyo mbunge wa magamba au na yeye yupo arumeru siku hizi?
 
Hapo ni kanisani unless ukituthibishia kuwa Kange Lugora ni mwislamu na sio mkristu ndipo tutaanza kuhoji. kama ni mkristu mwenzake hakuna sababu ya kuhoji uwepo wake kanisani hapo na hata kumsindikiza mbunge mwenzie kumshukuru Mungu

Sijawahi kumuona Kanisani hapa kwetu Kibara. Ni zaidi ya ukristu wake. Sasa hivi kila magamba anajitahidi aonekane anawajali wananchi na njia pekee ni kujifanya wako sambamba na wapiganaji. Umesikia maajabu ya Lowasa kuomba kuhamia CDM?
 
Shukrani kwa mungu ni jambo kubwa sana hasa kwetu sisi wakristo na pia shukrani kwa wote waliokupigia kura kampeni na kuzilinda kura! tunakumbuka sana tulivonyeshewa pale Leganga kwenye ofisi za halmashauri kulinda kura! sasa bwana mdogo jikite kutekeleza ahadi zako! kero za maji!! barabara! shule!! afya na donda dungu la arumeru " ardhi" hiyo ndio njia pekee ya kutushukuru wana Meru kwa kukupigia kura na kuzilinda! bwana awe nawe na akulinde!!
 
Kwani Lugola hawezi kuwa mpambe wa Nassari?ama wanaivana kikazi si mnaelewa watu wa kask fulani wanavyokuwa pamoja kwenye issues hasa za kimaendeleo?
 
acha upofu wa udini kanisa ni sehemu ya kusali na kukutana na waumini wenzie ila kwa suala la wapiga kura amekuwa akiitisha mikutano mbalimbali kushukuru wapiga kura na kueleza mikakati ya maendeleo ya jimbo letu! au unataka aanze tena kuzunguka misikitini, kanisa katoliki, anagelikana, baptist, shia, sunni, mjahidina , jehova,budhist n.k kutoa shukrani? Na ufahamu hapo alipokuwa ni kanisa la lutheran ambapo yeye ni muumini hapo kuna makanisa mengi sana ya kikikristu arumeru hakwenda,na mbona umekimbilia kuulizia waislamu kwa nini hujaulizia wapagani wasiomuamini mungu ambao wapo huku, au wanaoamini dini ya kienyeji ambao hutambikia chini ya miti? milimani? kwenye mapango? mito mikubwa au misituni? unataka na kote huko aende akatoe shukrani? huo upofu utakutoka lini???
 
Shukrani kwa mungu ni jambo kubwa sana hasa kwetu sisi wakristo na pia shukrani kwa wote waliokupigia kura kampeni na kuzilinda kura! tunakumbuka sana tulivonyeshewa pale Leganga kwenye ofisi za halmashauri kulinda kura! sasa bwana mdogo jikite kutekeleza ahadi zako! kero za maji!! barabara! shule!! afya na donda dungu la arumeru " ardhi" hiyo ndio njia pekee ya kutushukuru wana Meru kwa kukupigia kura na kuzilinda! bwana awe nawe na akulinde!!
mkuu hapo umemaliza kila kitu,tunashabikia viongozi wetu wa cdm ili watuletee maendeleo leo sukari ni sh 2600 hapa mza kiwanda kipo hapo kagera tu,nitaipenda ccm kwa kipi ?
 
Nassari yupo Kanisani...safi sana..sasa waislam waliokuchagua shukrani zao utazitolea wapi?

amesema anamshukuru kwanza Mungu then anaenda kuwashukuru wananchi katika vijiji vyote 86..kwahiyo sio kwamba kamaliza kushukuru hapana..waislam atakutana nao kwenye mikutano vijijini
 
Shukrani kwa mungu ni jambo kubwa sana hasa kwetu sisi wakristo na pia shukrani kwa wote waliokupigia kura kampeni na kuzilinda kura! tunakumbuka sana tulivonyeshewa pale Leganga kwenye ofisi za halmashauri kulinda kura! sasa bwana mdogo jikite kutekeleza ahadi zako! kero za maji!! barabara! shule!! afya na donda dungu la arumeru " ardhi" hiyo ndio njia pekee ya kutushukuru wana Meru kwa kukupigia kura na kuzilinda! bwana awe nawe na akulinde!!
Mmmmm:A S-coffee:
 
kwel alianza na mungu na anaendelea na mungu kristo wasiokuwa wakristo imekula kwao..
 
Back
Top Bottom