Nassari afyatuka: Kama maji hatuna flyover za nini?

Nassari aliongea vizuri sana, kwa wale waliofuatilia bunge! Tatizo la serikali yetu na serikali nyingi sana za nchi maskini ni tatizo la kipaumbele na mipango mahsusi. Mambo yanaishia kwenye makaratasi, pesa zikitoka, nusu analipwa mkandarasi iliyobaki italeta maajabu kweli? Kazi tyunayo!
 
Kun mbunge mmoja nadhani ni wa upinzani huyu anaponda kuwa wizara ya maji ivunjwe kwa kuwa imeshindwa kuleta maji.

Huyo ni mbunge ni wa Namanyere, hajaoga kwa siku tatu alipokuwa Namanyere akasema yeye ni mwanamke je mwanamke itakuwaje. Ni Ally Kessy kwa kweli amenifurahisha sana.

Si mmejijaza Dar sababu vitu muhimu ni shida kupatikana sehemu nyingi? Embu maji yaboreshwe uone kama makampuni hayatasambaa
 
mkuu watanzania walio wengi wanaishi vijijini..wanatumia mudamwingi kwenda kutafuta maji na hii ni kwarika zote vijana,wamama,watoto,na wazee..hawa walitakiwa muda mwingi watumie katika shughuli za kilimo,na watoto wanatakiwa kuwa shule badala ya kuwaste the whole day kutafuta maji..by the way maji ni afya pia..you should think twice mkuu..
Godwinnko,
ninachosema hapa ni kuwa tuko nyuma sana, hili suala la maji lilitakiwa kuwa limeshatatuliwa siku nyingi sana, haingii akilini watanzania kulalama kwa kuokosa maji leo, juzi nimesoma uji mmoja humu kuhusu gharama za kuchimba kisima, it was never more than 5m. tatizo letu kubwa zaidi ni ujinga kuliko hata ufisadi (hasa kwa viongozi wetu) sasa fikiria mtu anaiba mahela mengi kiasi kwamba hujui atayatumia lini, ni ujinga wa kufikiri tu, hata kama anataka kuiba ili watoto wake waje wayatumie in maana yuko tayari kufanya kizazi chake kiwe kama konokono, hakuna haja ya kufikiri tena, hakuna haja ya kufanya kazi tena; baba alishaiba katutengea, kazi ni kula tu, mimi nisingependa kuwa na watoto wa aina hiyo, ningependa kuwa na watoto ambao wangetumikisha akili yao ku exprole the universe, ili ikiwezekana siku moja na sisi tugundue angalau kitu kimoja basi tuwauzie wenzetu. vigogo wa leo wako tayari kuwanunulia watoto wao mitihani, wako tayari kuwapa watoto wao kazi bila qualifications tena wanawatafutia sehemu zenye mshahara au (ulaji) mnono kama BOT TRA nk. nk.

Tanzania kamwe haiwezi kuendelea kwa mtindo huu.... naona uvivu ku type maana hakuna jipya nitakalosema hapa yote mnayajua...

I HAVE THOUGHT THRICE...
 
Last edited by a moderator:
Kati ya miujiza ambayo sitaki kuiamini ni hili la jiji la dsm kukosa maji mpaka leo. Yani bora tutembee kwenda makazini hata ikibidi kwa miguu, lkn tuwe na maji, maajabu kabisa yani mnashindwa kutuletea maji tena ambayo tutayanunua? Noma kwelikweli.
 
Habari jamvini,
Naamini sitakuwa kuwa nje ya mada,kwani ukiondoa asilimia 60 ya magari binafsi yanayozunguka dar,ukawa na madaladala route zote Mara ya zilizopo sasa.msongamano utaendelea?

Lakini pia tujadili njia mbadala ya kuondoa msongamano wa magari dar.
SIO Dar tu hata Arusha mjini tunataabika na foleni ya magari tunahitaji flyovers.
 
tatizo la viongozi wetu ni kwamba wanafikiria mwisho Dar es salaam...utaongelea flyover lakini ipact yake ni kwa watu wachache sana(sio kwamba nasema flyovers ni mbaya).
ila imekuwa ni kawaida ya wanasiasa..unakuta ni mbunge wa huko mbali lakini analalamika kuwa Dar mifereji haifanyi kazi mvua zikinyesha....
Waziri wa ardhi ni nadra kumsikia mikoani ama wilayani..ila kila siku utamsikia anahangaika na viwanja na maeneo ya wazi ya Dar.

Tatizo lingine ni kuwa wanaiba sana mpaka wanajisahau, Tanzania haikuwa nchi ya kulalamikia maji leo hii Davie, tuna almasi mwadui, dhahabu almost every where, tanzanite only here, asali na mbao Tabora, mbuga za utalii ndio usiseme (kuna nchi zinategemea utalii tu kama seychelles lakini ziko njema) tuna samaki kama wale wa Magufuli, tuna... you name it.... umaskini wa Tanzania uko kwenye akili za wale 'walioteuliwa' kutuongoza.
 
Kun mbunge mmoja nadhani ni wa upinzani huyu anaponda kuwa wizara ya maji ivunjwe kwa kuwa imeshindwa kuleta maji.

Huyo ni mbunge ni wa Namanyere, hajaoga kwa siku tatu alipokuwa Namanyere akasema yeye ni mwanamke je mwanamke itakuwaje. Ni Ally Kessy kwa kweli amenifurahisha sana.

Yule siyo upinzani mkuu ni mwanaccm aliyeelimika...
 
tatizo la viongozi wetu ni kwamba wanafikiria mwisho Dar es salaam...utaongelea flyover lakini ipact yake ni kwa watu wachache sana(sio kwamba nasema flyovers ni mbaya).
ila imekuwa ni kawaida ya wanasiasa..unakuta ni mbunge wa huko mbali lakini analalamika kuwa Dar mifereji haifanyi kazi mvua zikinyesha....
Waziri wa ardhi ni nadra kumsikia mikoani ama wilayani..ila kila siku utamsikia anahangaika na viwanja na maeneo ya wazi ya Dar.

Na ndio maana mapinduzi ya kweli ya kijamii, kifikra, na kiutawala yataanzia huko huko mbali na sio Dar. Huko mbali wakijitambua tu, ah, nchi imekombolewa hii.
 
Maji ni mahitaji muhimu kwa maisha ya binadamu kuliko hata kitu kingine kwako unaweza ukawa na umeme bila maji ni kazi bule unaweza ukawa una sera nzuri za maendeleo lakini bila maji malengo yako yakahalibika.kila kitu kitahitaji maji kwa uwepo wake
 
Huyo ni wa CCM siyo upinzania hata yule alomnanga magembe akamwambia alijua katika mawaziri ambao wasingerudi na yeye ni mmojawapo, naye kanifurahisha sana, anasema mkurugenzi anarudishwa kazini kwa undugu na upendeleo naye ccm
 
Ndugu zangu mseme mnavyosema nchii hii (mrema anasemaga nji hii............) tusitegemee jipya toka kwa hawa watu wanaoitwa chama tawala aka... Chama cha majambazi.... Nasema hakuna jipya hapa leo tuna miaka 51 ya uhuru nini maji bwana, madawati tu kwa shule zetu za msingi tu ni mtihani mkubwa ambao hata jk hajui aanzeje kuutatua vp .kwa shule za msingi mpaka leo watoto tena mjini tu wanakaa nchini... Tembeleeni shule za mjini....tu acheni vijijini... Harafu wakina zomba, na wakina rejao wanaitetea hii serikali... Zile pesa tu za epa zingetengeza madawati mangapi..... Zile za dip green, za meremeta.... Wale waliouza twiga.... Wetu wangefirisiwa tungepata shi ngapi hapo??? Madini yetu leo tanzanite haisikiki tena.... Na ni tz pekeyakee ulimwengu mzima yenye hayo madini.... Akharaaaaa mpaka hasira wandugu... Harafu manasema tuna serikali... Kweli miaka 50 hata malaria tu imetushinda.... Hivi niwaulize wakina katiba mpya... Na majebere na wengineo kama mpaka mwaka 1990 tulikuwa na viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yetu mbalimbal; kama pamba na kadhalika... Vinda vya nguo takribani 45... Acha viwanda vinginevyo leo pita morogoro hapo vyooote*(polyster,..... Kanivasi.. Moroshoe, moproko... Magunia... Ceramic...) vyoote vimekufa... Na vilikuwa vinatoa ajira kwa zaidi ya wakazi 30,0000 wa mkoa wa morogoro... Leo ni magofu tu wahindi wamefanya.... Kama walivyo fanya reli... Ndio maana mpaka leo najiuliza hivi hawa wanaoishabikia hiii serikali ni watz kweli..... Miaka hamsini hata net za mbu tuombe msaaada kwa bush kweli????? Ndugu zangu,....... Hakuna jipya... Narudia tusitarajie jipya toka kwa jk... Na wenzie wa ccm.. Woote ni wakunyonga tu... Watu wanakufa kwa kukosa hata mlo mmoja tu kwa siku.. Wao wakobize na kurundika madola uswis na kuwaibia watanzana.... Adui no 1. Wa umaskini wa watz ni hiii serikali ya ccm kataaa ukubali.... Ovaa
 
Ameongea jambo la msingi sana!
Swala la maji ni muhimu zaidi ya bara bara
 
Ahadi ya ccm kila mtanzania maji ya bomba kufikia mwaka 2000. Miaka 12 baadaye kila mtanzani kidumu mkononi anahangaika kutafuta maji si mijini sio mashambani.
 
tatizo la viongozi wetu ni kwamba wanafikiria mwisho Dar es salaam...utaongelea flyover lakini ipact yake ni kwa watu wachache sana(sio kwamba nasema flyovers ni mbaya).
ila imekuwa ni kawaida ya wanasiasa..unakuta ni mbunge wa huko mbali lakini analalamika kuwa Dar mifereji haifanyi kazi mvua zikinyesha....
Waziri wa ardhi ni nadra kumsikia mikoani ama wilayani..ila kila siku utamsikia anahangaika na viwanja na maeneo ya wazi ya Dar.

Mkuu, unachosema ni kweli kabisa. Wengi wanatoa hoja zinazohusu Dar, na hii inatoa picha kwamba wengi baada ya kupata kura hawaishi maeneo waliyopatia ubunge.
 
tanira1 Sio barabara za kifahari, dhumuni ni kupunguza msongamano ili tuwahi kazini tuweze kushughulikia maji, imagine mtu una drive 21 km for three hours (tegeta to masaki) kila siku X2 means 6 hours back and forth... think.

hakuna suala la kujadili hapa,

Sasa ww wa Tegeta Masaki flyovers unayotetea wakuwekee wapi? au unamaanisha Mwenge na Morroco?
 
irani watatuletea maji na madaktari 1000 halafu watapeperusha bendera ya tz ktk meli zao za mafuta, very simple!
 
Kaka maji yashughulikiwe mwaka 2012 tangia CCM iko madarakani miaka 51 leo ?

awamu ya kwanza yalikuwepo katika kila kijiji mkuu. Kijijini kwetu yalikuwepo hadj nyumbani kwetu kulikuwa na bath tabs nakumbuka. Then yalitokomea late 80s na ma tabs yetu yakaishia kupata kutu. Kifupi waafrika hatuna uwezo wa kutunza mafanikio hata kidogo. Hapa ninaposema haya pale kijijini maji ni ya kufuata km 1 kisimani. Kuliwahi kuwa na mradi wa RIDEP pia kama sikosei ambapo vijiji visivyo na bomba vilikuwa na visima na pumps za kukanyaga kwa miguu au kupump kwa mikono. Kusema ukweli wizi umeturudisha nyuma sana. Pump zetu pale village zilikuwa mbili na moja katibu tarafa albeba na kutengenezea machine yake ya kusaga. Hii ndo TZ.
 
Godwinnko,
ninachosema hapa ni kuwa tuko nyuma sana, hili suala la maji lilitakiwa kuwa limeshatatuliwa siku nyingi sana, haingii akilini watanzania kulalama kwa kuokosa maji leo, juzi nimesoma uji mmoja humu kuhusu gharama za kuchimba kisima, it was never more than 5m. tatizo letu kubwa zaidi ni ujinga kuliko hata ufisadi (hasa kwa viongozi wetu) sasa fikiria mtu anaiba mahela mengi kiasi kwamba hujui atayatumia lini, ni ujinga wa kufikiri tu, hata kama anataka kuiba ili watoto wake waje wayatumie in maana yuko tayari kufanya kizazi chake kiwe kama konokono, hakuna haja ya kufikiri tena, hakuna haja ya kufanya kazi tena; baba alishaiba katutengea, kazi ni kula tu, mimi nisingependa kuwa na watoto wa aina hiyo, ningependa kuwa na watoto ambao wangetumikisha akili yao ku exprole the universe, ili ikiwezekana siku moja na sisi tugundue angalau kitu kimoja basi tuwauzie wenzetu. vigogo wa leo wako tayari kuwanunulia watoto wao mitihani, wako tayari kuwapa watoto wao kazi bila qualifications tena wanawatafutia sehemu zenye mshahara au (ulaji) mnono kama BOT TRA nk. nk.

Tanzania kamwe haiwezi kuendelea kwa mtindo huu.... naona uvivu ku type maana hakuna jipya nitakalosema hapa yote mnayajua...

I HAVE THOUGHT THRICE...

tembea uone ndugu yangu. Umesema ya TRA nikakumbuka. Pale TRA ya ARUSHA kuna mabinti wawili mapacha wa kichaga waliajiriwa mwaka jana. Walinifanya niwaze sana kwa kweli. Nji hii haiko salama tena.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu mseme mnavyosema nchii hii (mrema anasemaga nji hii............) tusitegemee jipya toka kwa hawa watu wanaoitwa chama tawala aka... Chama cha majambazi.... Nasema hakuna jipya hapa leo tuna miaka 51 ya uhuru nini maji bwana, madawati tu kwa shule zetu za msingi tu ni mtihani mkubwa ambao hata jk hajui aanzeje kuutatua vp .kwa shule za msingi mpaka leo watoto tena mjini tu wanakaa nchini... Tembeleeni shule za mjini....tu acheni vijijini... Harafu wakina zomba, na wakina rejao wanaitetea hii serikali... Zile pesa tu za epa zingetengeza madawati mangapi..... Zile za dip green, za meremeta.... Wale waliouza twiga.... Wetu wangefirisiwa tungepata shi ngapi hapo??? Madini yetu leo tanzanite haisikiki tena.... Na ni tz pekeyakee ulimwengu mzima yenye hayo madini.... Akharaaaaa mpaka hasira wandugu... Harafu manasema tuna serikali... Kweli miaka 50 hata malaria tu imetushinda.... Hivi niwaulize wakina katiba mpya... Na majebere na wengineo kama mpaka mwaka 1990 tulikuwa na viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yetu mbalimbal; kama pamba na kadhalika... Vinda vya nguo takribani 45... Acha viwanda vinginevyo leo pita morogoro hapo vyooote*(polyster,..... Kanivasi.. Moroshoe, moproko... Magunia... Ceramic...) vyoote vimekufa... Na vilikuwa vinatoa ajira kwa zaidi ya wakazi 30,0000 wa mkoa wa morogoro... Leo ni magofu tu wahindi wamefanya.... Kama walivyo fanya reli... Ndio maana mpaka leo najiuliza hivi hawa wanaoishabikia hiii serikali ni watz kweli..... Miaka hamsini hata net za mbu tuombe msaaada kwa bush kweli????? Ndugu zangu,....... Hakuna jipya... Narudia tusitarajie jipya toka kwa jk... Na wenzie wa ccm.. Woote ni wakunyonga tu... Watu wanakufa kwa kukosa hata mlo mmoja tu kwa siku.. Wao wakobize na kurundika madola uswis na kuwaibia watanzana.... Adui no 1. Wa umaskini wa watz ni hiii serikali ya ccm kataaa ukubali.... Ovaa
Nimeipenda hii ingawaimenitia uchungu ulivyomention viwanda vya mkoani Moro. Hivi wanaweza kusema vimekufaje? Tulikuwa na kiwanda cha mazulia kilosa wakati km huu wa maonyesho walikuwa wanatuletea macarpet, table mats nk leo hii ni 0000. CCM imeua na kuuza kila kitu nadhani wataanza kuunza binadamu km bado hawajaanza. Tusimame pamoja jamani rushwa imezidi maskini au upinzani wanaumia ccm wso wanatajifika. Ninahasira hapa nilipo. Wanafunzi hawana mikopo hela zipo uswiss, madaltari wanaongea hakuna wakuwasikiliza.
 
Back
Top Bottom