Nassari afunika nyumbani kwa sioi sumari 15/6/2012

Kuitisha harambee ndio kutimiza ahadi? Kila siku JK na Lowassa wanaitisha harambee kwa hiyo wanatimiza ahadi.

Sioi anaweza hata kuitisha kaharambee ka kuchangia kununua unga wa uji wa watoto wa chekechea?
dhubuutu!!!! atajitokeza yeye pekee, manake hata mkewe atakuwa na udhuru, atakuwa kwa babake.
 
Sabodo hakuombwa kujenga visima bali ni dhamira yake binafsi ndio iliyomsukuma kusaidia kujenga visima baada ya kuona kijana ana nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo wana Arumeru

achana na huyo mtoto wa chekechea, yaani yeye wenzake wanaingia darasa pili yeye analilia kwenda baby class
 
Kama harambee inafanyika kwa ajili ya kutimiza ahadi fulani kuna ubaya gani?Ulitaka Nassari atoe fedha zake mfukoni wakati wananchi nao wanatakiwa kuchangia kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe na njia mojawapo ni hiyo harambee.
JK na Lowassa sijawahi kuwasikia wakiitisha harambee zaidi ya kuona wakialikwa katika kuzifanikisha,sijui unapata wapi habari kuwa wanaitisha harambee.

Mkuu hunajua kama Nassari kapata Sh15 milioni mfuko wa jimbo kazifanyia nini kama kuchimba kisima kafanya harambee yeye katoa ngapi?
 
Mkuu hunajua kama Nassari kapata Sh15 milioni mfuko wa jimbo kazifanyia nini kama kuchimba kisima kafanya harambee yeye katoa ngapi?

amepewa lini?embu tupa evidence ili nimbane mapema, je unajua gharama ya kisima kimoja?je nikikupa ahadi nitakusaidia kukujengea nyumba ina maana hutajenga ya kwako? Embu tuambie alipewa shilingi ngapi cash za kuchimbia visima ili tujue kama na yeye ni swahiba wenu
 
punguza ufinyu wa mawazo, sabodo si mwananchi wa arumeru,pili si mwanachama wa cdm, je kuna barua yoyote toka cdm aliyoandikiwa sabodo ya kuombwa msaada au ni yeye kwa roho ya kiibinadam aliamua kujitolea?

Roho ya kibinadamu kwa mfanyabiashara?
 
Sabodo hakuombwa kujenga visima bali ni dhamira yake binafsi ndio iliyomsukuma kusaidia kujenga visima baada ya kuona kijana ana nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo wana Arumeru

Maendeleo gani aliyowaletea hadi hivi leo? jana [MENTION]ritz [/MENTION]aliuliza mbona bei ya sukari hajashusha hadi leo? we mbunge mzima anakimbilia kupiga mapicha na wazungu, si utoto jamani huu?
 
Maendeleo gani aliyowaletea hadi hivi leo? jana ritz aliuliza mbona bei ya sukari hajashusha hadi leo? we mbunge mzima anakimbilia kupiga mapicha na wazungu, si utoto jamani huu?
Unataka asafiri akapige na wakina Beckham na boyz two men huko marekani pamoja nakufungua vimigahawa kama JK
 
Kuitisha harambee ndio kutimiza ahadi? Kila siku JK na Lowassa wanaitisha harambee kwa hiyo wanatimiza ahadi.

Kuitisha harambee ni kukusanya nguvu za wananchi ili kufikia lengo walilojiwekea. Na maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe. Kwahiyo dogo ameunganisha nguvu za wananchi ili kujenga kisima. Hilo linastahili pongezi maana wengi hawawezi. Na hiyo ndio kazi ya mbunge.
 
Unapanda jukwaani kuto ahadi ukimtegemea sabodo aje ajenge visima? huu si utoto jamani?

kusahau kubaya na kufanya mambo bila kumbukumbu nako ni kubaya zaidi. Afadhali huyu anayeahidi na kufanya harambee ya kuwasaidia watu wote hapo Arumeru. Baba yako mrisho kikwete aliahidi kwa kutegemea mfuko wa waturuki, wairani, wamarekani, waswedeni.Umeshawahi kumuhoji huyu?Aliahidi kuwaunganishia umeme wa gridi ya taifa wanaRuvuma toka Makambako kumbe akitegemea aende Sweden kuomba msaada huo.Wasweden wamegoma kumsaidia na yeye ahadi hiyo imeota mbawa.Mna lolote la kujivunia juu ya hili?Mnaorodhesha ahadi hata ambazo haziwezekani kuzitekeleza lakini bado nyie mnatamka.Mna matatizo makubwa.Siku zinakuja ambapo hakuna mwana ccm atakayesalia hata mmoja.
 
hongera dogo janja....usipoe endelea hivyo na utakuja kuwa mtu maarufu sana na wakuheshimiwa
 
Ccm nawafananisha na ngiri ambaye anakimbizwa na ngiri halafu baada ya nusu dk anasahau alikuwa anawindwa,hivi nyie ccm miaka 50 kila siku unatoa ahadi hiyo hiyo mnatofauti na ngiri?sasa hivi mmeamua kubadilisha tu acapela mara nguvu mpya...., kilimo kwanza, vua gamba ....n.k
 
CCM na mashabiki maslahi lazima wajifunze kusoma nyakati.kama ccm itaendelea kuwepo madarakani 2015 basi kuja kwa mwana wa Adamu kumekaribia.
 
Leo hii ccm inatoa ahadi badala ya kutekeleza walizolunda kabatini kwanza. Hivi ahadi yenu ya kujenga viwanja vya ndege vya kisasa mnaikumbuka huko Misenyi?Au mmesahau?Meli katika maziwa yote vipi mmeshaanza kupeleka?
 
Kuitisha harambee ndio kutimiza ahadi? Kila siku JK na Lowassa wanaitisha harambee kwa hiyo wanatimiza ahadi.

Kwa hiyo unakiri kwamba Kikwete hajatimiza ahadi zake. Asante kwa kuliona hilo, hii imekutoka bila kujijua.
 
Back
Top Bottom