Nasita kuendelea kuandikia Gazeti

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Baada ya tafakari ya kina nimeamua kuacha kuandikia mojawapo ya magazeti ya nyumbani ili nijipe muda wa kushughulikia mambo yangu mengine binafsi na kujipanga upya. Unless mambo yakibadilika lakini nadhani kuna makala moja tu ambayo itatoka na itakuwa mwisho wa kuendelea kuandika.

Nawashukuru wote mlionisupport hadi sasa na ambao mmekuwa inspiration ya maandishi yangu mengi.

Tutaendelea kuwa pamoja hapa na kwa njia nyingine ambayo natarajia kuianzisha muda si mrefu.

Katika mapambano ya kifikra..

Humbly yours,

m.m. m.
 
Haya Mkjj, Tunakutakia mema tu siye.... i hope hamna mabaya yaliyokufanya uingiwe na hizo tafakari.

All the best...
psssss.... je unaweza kuya name hayo/hilo ma/gazeti?!
 
Btw, umeandika unasita, hivyo inamaanisha ni kama unatafuta ushauri... lakini ndani ya habari inaonekana umeshachukua uamuzi tayari... which is which?!!! can you enlighten us pls..
 
Tunashukuru sana kwa mchango wako. ni matumaini yetu kuwa hujashinikizwa kwa uamuzi huo uliouchukua.
tunakutakia kila la kheri kaka
 
Mbona unaonekana kama unabip....kichwa cha habari then habari yenyewe kama unaomba ushauri lakini umesha amua.Any way naona unatuaga rasmi labda.
Kama ni ushauri au maoni yetu tunaomba uendelee kuandika magazetini kwani mpiganaji hachoki hata akichoka amesha shinda.
Kama tatizo ni njaa tunaweza tukawa tunakuchangia ili kupata mchango wako mkubwa sana kwenye magazeti naamini kuna watu hapa hawapajui lakini wanapata mawazo na mchango wako kwa kupitia kwenye magazeti unayo yaandika.
 
sikusema nasita sita... nimesema nasita.. mwe hii lugha yetu. Kusita ni kukoma kufanya kitu.
 
Wala usikonde mchango wako tumeuona! na kila baraka kwa unalopanga kufanya!
 
sikusema nasita sita... nimesema nasita.. mwe hii lugha yetu. Kusita ni kukoma kufanya kitu.

Mkjj, kamusi sina hapa, lakini naamini wengi watakawo soma kichwa cha thread, wataelewa kuwa 'unasita sita' badala ya kwamba 'unakoma'.....
 
Bora mwana, maana kama tunaambiwa Unga uliomwagwa Bungeni hauna madhara yoyote, ELEWA NA NASISITIZA UNGA ILOMWAGWA BUNGENI, JAMANI ULIOMWAGWA BUNGENI HAUNA MADHARA, sasa sembuse wewe wakitaka kukuharibia ni mara moja, Kila la Kheri Mkuu, mimi nakupa 5.
 
nashukulu kusikia utakuja na njia ingine,,,otherwise mie nakuunga mkono uamuzi wako ili kkuwezesha kuchemsha ubongo jinsi gani utoke upya...1
 
sikusema nasita sita... nimesema nasita.. mwe hii lugha yetu. Kusita ni kukoma kufanya kitu.

Nasita, although correct, is ambiguous due to the double meaning na inaleta picha ya kuwa na shaka zaidi (first meaning) kuliko ya kusimamisha uandishi wako kwa gazeti hilo. Nasitisha au nakoma is more definite.

Naona unatumia full repertoire ya Kiswahili Mzee

http://perl.kamusiproject.org/cgi-b...n/lookup.cgi?Word=sita&EngP=0&SUBMIT2=Look+Up

-sita { English: hesitate } [derived: Arabic]
verb , [ photos: upload ]
Swahili Example: kila mmoja alisita
English Example: everyone hesitated

-sita { English: move (slowly or uncertainly) }
verb , [ photos: upload ]

-sita { English: stop } [derived: Arabic]
verb , [ photos: upload ]
Swahili Example: hoihoi zilisita
English Example: the shouting stopped
 
Natumaini hatutakusikia kwenye Payroll ya Rostam Aziz

labda hicho ndicho nakikwepa...??? unfortunately for him. he doesn't have enough money to put me in his payroll..

meanwhile.. I'm enjoying some congolese and oldtime music... "live" kwenye KLHN...
 
is that so? where did he say that...?

Mkuu, how could you miss that:

Tanzania Daima.
Jumanne, Julai 8

"Jamani asiwadanganye mtu kuwa mimi ninaweza kununuliwa, kwani bei yangu haijulikani, na sitegemei kunyamaza kwa wote wanaoshiriki katika kutafuna rasilimali za nchi," alisema Zitto.

Zitto alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki mjini Tanga alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara baada ya mkazi mmoja wa mjini humo kumuuliza kama kuteuliwa kwake katika kamati ya kuchunguza masuala ya madini kulikuwa na nia ya kununuliwa na kuukacha upinzani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom