Nasisitiza, wakati wa Katiba mpya ni sasa

Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
2,017
2,208
Nasema hivi, hatutakuja kupata tena nafasi nzuri na kwa muda muafaka wa kutengeneza katiba mpya iliyo nzuri kama sasa, namaanisha wakati wa utawala wa rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hassan.

Zingatia na kumbuka yafuatayo:

1) Rais wa sasa anakubalika katika pande zote za Muungano, na tayari ni mwenyekiti wa chama tawala. Kwa fursa hii sidhani kama kuna siku wazanzibari wanaweza inua vichwa kuulalamikia muungano wakati fursa ya kutengeneza katiba bora ya nchi imepatikana chini ya utawala Mzanzibari.

2) Binadamu, na hasa Watanzania tuna tabia ya kusahau haraka matukio yaliyopita na kushughulika na ya wakati uliopo ndio maana huwa vyepesi serikali kuondoa watu kwenye agenda moto kwa mbinu ya kutengeneza tukio mbadala. Watu husahau na kuanza kujadili jambo jipya!

3) Watangazia wakati huu bado tuna kumbukumbu ya yaliyotokea katika tawala zilizopita. Jinsi rais anavyoweza kufananishwa na mungu, akaziba midomo ya watu wote, watu wakapotea, vyama vya siasa, taasisi za kiraia, bunge, mahakama na hata majeshi vyote tukanyooshwa na kuwekwa katika msitari mmoja. Baadhi ya watu kujitwika mamlaka yasiyohojiwa, akina Sabaya, Makonda n.k

Kiongozi mmoja akafikiri kwa niaba ya taifa zima. Akaamua na kulipia ujenzi wa miundombinu mingine isiyo na tija mfano airport ya chato. Watu kubambikiwa kesi na kodi za kutesa na kuumiza. Watu kufungwa na kesi zisizosikilizwa. Mtu unakaa mahabusu kuliko adhabu ya kifungo cha kosa husika. Mambo ni mengi kiasi kwamba hata kutamka tu kuwa mkubwa anaumwa unawekwa ndani!

Huyu mama ana busara, ni mstaarabu, ana upeo mkubwa wa masuala ya kitaifa na kimataifa.Ni mwana diplomasia na ni mwanasiasa!

Tukipoteza nafasi hii, kamwe haitatokea tukapata katiba inayobalance maslahi ya zanzibar na Tanganyika.

Ngoja ngoja huumiaza matumbo. Hebu tujifanye yanatokea yakutokea kama yaliyotokea kwa jpm. Wewe unayesoma hapa unadhani huyu makamu wa rais wa sasa, ikitokea akawa rais, kwa kauli zake zenye dalili ya ubabe na uhafidhina, kweli unaamini tunaweza kumuomba akatupa katiba mpya ya maana?

Huyu sanasana atatupa katiba ya marehemu samweli sita au akaishia kusema katiba si kipau mbele chake. Hawezi kutupa katiba yenye kujali maslahi ya Zanzibar, yenye kurekebisha masuala ya muungano maana huwa namsikia akisema atakayethubutu kuuchezea muungano atakipata cha moto!! Hadanganyi, anamaanisha. Na kumbuka hapo bado ni makamu tu wa rais.

Binadamu ni kama moto wa kibatari, waweza zimika wakati wowote. Maadamu tuko na kiongozi ambaye mimi binafsi naamini anaweza kutupatia katiba mpya na bora, tupige kelele bila kuchoka mheshimiwa atupatie katiba mpya.

Jambo la msingi lakini ikiwa pia ni zawadi kwake kwa kufanikisha jambo hilo, na nawaomba watanzania wote kwa umoja wetu tukubali kumuachia nchi aiongoze muhula huu na kumpitisha bila kupingwa muhula ujao, aongoze hadi 2030.

Hii itamuondolea hofu ya kuandika katiba mpya halafu ikamtoa madarakani. Hii itamfanya atende kazi yake kwa amani, aweke mambo sawa, ahakikishe katiba mpya imepatikana, sheria zimerekebishwa, na nchi imetulia.

Uchaguzi mkuu wa 2025, kwa kutumia katiba mpya tuchague viongozi wa serikali ya mtaa wabunge na madiwani tu. Rais samia apitishwe tu na a-demonstrate jinsi mambo yanapaswa kuwa chini ya katiba mpya.

Mheshimiwa rais, nakushauri, weka rasimu ya katiba ya jaji warioba mezani, inatosha. Wananchi tuliielewa na tuliikubali. Kama kuna mapungufu tutayarekebisha wakati inatumika, na bahati nzuri wewe utakuwa bado rais!

Kwa nia yako njema unayonafasi ya kuleta miswaada bungeni kwaajili ya kufanyiwa marekebisho pale patakapokuwa hapajakaa sawa. Mpaka inafika 2030 utakuwa umefunga kazi. Utaacha umejiandikia jina lako kwa wino wa dhahabu. Na naamini kwa kufanya hivyo utafunguliwa mbingu kwa mwenyezi mungu mapema hata kabla alah hajakuita kwa ajili ya kazi za kimalaika huko mbinguni.

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ----- kazi iendelee!
 
Nilikuwa nakukubali lakini nilpofika hapa ndio nimegundua hujui kwanini unataka katiba mpya.

“JAMBO LA MSINGI LAKINI IKIWA PIA NI ZAWADI KWAKE KWA KUFANIKISHA JAMBO HILO, NA NAWAOMBA WATANZANIA WOTE KWA UMOJA WETU TUKUBALI KUMUACHIA NCHI AIONGOZE MUHULA HUU NA KUMPITISHA BILA KUPINGWA MUHULA UJAO, AONGOZE HADI 2030.
" data-src="/proxy.php?image=https%3A%2F%2Fcdn.jsdelivr.net%2Fjoypixels%2Fassets%2F6.5%2Fpng%2Funicode%2F64%2F1f44f.png&hash=45e86c1870d011d49fb22f6c4d69ae35" data-lb-sidebar-href="" data-lb-caption-extra-html="" data-single-image="1"> <img src=" title="" width="" height="" />

Huu ndio ule upuuzi wa siku zilizopita.
 
Mawazo yako ni sahihi kwamba asiachwe akapiga hivi hivi, lakini angalia ugumu wa suala hili kwa kiongozi aliyeko madarakani asimamie kuandika katiba mpya halafu imtoe madarakani. Si wengi wenye ubavu wa kukubali jambo hili. Hii ilitokea kwa De Klerck wa South Afrika na baadhi ya wastaarabu kama akina Kaunda.

Kama Mama hana nia ya kugombea tena Urais, mama anaweza sema potelea mbali kwakuwa sihitaji tena urais ngoja niwape watu kitu wanataka. Hapo anaweza kuchukua wazo lako. Lakini kama ana nia ya kugombea urais, na bado anataka kuendelea kuongoza nchi, hawezi kuanzisha suala la mabadiliko ya katiba kwa sasa mpaka apate kipindi chake cha mwisho.

Swali ni je, kuanzia sasa mpaka ashike kipindi chake cha mwisho, Mwenyezi Mungu anauamuzi gani kwake? Sasa mimi najaribu kukushawishi wewe ili ukubaliane na mimi kuwa Ni BORA tu sacrifice Miaka 5 ya URAIS ili tupate katiba bora kuliko kuikosa kwa gharama ya kushiriki uchaguzi ambao hata hivyo hutatangazwa hata kama utashinda.
Mimi hoja yangu kubwa ni sisi binadamu kutokuwa na guarantee ya uhai.

Mama Samia Ni kiongozi wa pekee sana kwa kuzingatia anatoka upande gani wa muungano, hana mtandao, hana kabila huku bara, wahafidhina wengi hawapo akina Mkapa, Kingunge, Kambarage. Tusisubiri litokee lamajuzi kabla mchakato haujaanza. Wanaofuatao hawataweza kufanya vizuri mpaka miaka mingi ijayo huku kukiwa na vurugu nyingi za kiuongozi hasa wakati wa chaguzi!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom