Nasimama na Mbowe dhidi ya kikundi cha "waasi" ndani ya CHADEMA wanaotaka kumpoka uenyekiti

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Kwa hili la uasi ndani ya CHADEMA nasimama na Mbowe,kuna kikundi ndani ya CHADEMA kimepanga na kimeshaota mizizi kikiwa na lengo la kukupoka uenyekiti wa Chama. Hoja kuu ya kikundi hiki ni "elimu" na "uchungu wa matumizi ya fedha za ruzuku".

Mbowe shtuka! Kwani hata "majasusi" wako akina "mkulima wa bamia" na "Meya wa stendi kuu ya mabasi ya mikoani" wameungana na kikundi hicho bila wao kutambua.

Vita uliyonayo unahitaji msaada kutoka nje kwani "umaviwa na panya wenye njaa" tulia kwanza uone utatokaje kwani wenzio wamejipanga wakapangika.

Kundi hili limesheheni wabunge na viongozi waandamizi mikoa na majimbo sasa usikurupuke.Unatakiwa ufanye yafuatayo ili kuwamaliza nguvu;
1.Kuelekea uchanguzi Mkuu ndani ya chama "wafyeke" ili wasikusumbue wakati wa kupiga kura na kupitisha maazimio kwenye mikutano.

2.Pandikiza mtu wako "mpya" sio hao niliokwambia hapo juu kwenye makundi sogozi ya wabunge na viongozi ili afuatilie mijadala na yao na kukutonya kinachotokea

3.Makundi hayo pia yameanza kuleta mijadala dhidi yako humu JF

4.Ikibidi omba msaada wa vyombo vya dola kama ulivyoomba mwaka 2013 ili kumdhibiti Zitto.

5.Usipuuze mambo madogo kamanda

Nawasilisha
 
Kuna habari nyingine zimezidi uwezo wa ubongo wako achana nazo laa sivyo unabaki uchi kama hivi ulivyo.
kwahiyo unataka kutushawishi kuwa we unaweza kuwa mshauri wa Freeman
kuna members tunafungua uzi za maana humu halafu mod wanafuta
wanaacha upuuzi huu wako ambao hauna faida kwa CCM MBOWE
tena kwa upande wako ni hasara kwa kuwa unakufanya uonekane zuzu
Hahahahhaaaaa eti wewe ni naibu?
 
Mbumbumbu wanapata madaraka makubwa ya kiuongozi kama vile ubunge, unaibu waziri na ukuu wa mikoa kwakua wana 'fit in' kwenye jamii mbumbumbu. Werevu wanakua 'estranged' na kuonekana hawana 'uzalendo'.
 
kwahiyo unataka kutushawishi kuwa we unaweza kuwa mshauri wa Freeman
kuna members tunafungua uzi za maana humu halafu mod wanafuta
wanaacha upuuzi huu wako ambao hauna faida kwa CCM MBOWE
tena kwa upande wako ni hasara kwa kuwa unakufanya uonekane zuzu
Hahahahhaaaaa eti wewe ni naibu?
Huyu dada mada zake zinaharibu hali ya hewa hapa JF.
 
mbumbumbu wanapata madaraka makubwa ya kiuongozi kama vile ubunge, unaibu waziri na ukuu wa mikoa kwakua wana 'fit in' kwenye jamii mbumbumbu. Werevu wanakua 'estranged' na kuonekana hawana 'uzalendo'.
Kuna watu wana madaraka (ubunge, uwaziri n.k.) lakini ukitazama uwezo wao wa kufikiri na kutenda..unaishia kushangaa tu!
 
kwahiyo unataka kutushawishi kuwa we unaweza kuwa mshauri wa Freeman
kuna members tunafungua uzi za maana humu halafu mod wanafuta
wanaacha upuuzi huu wako ambao hauna faida kwa CCM MBOWE
tena kwa upande wako ni hasara kwa kuwa unakufanya uonekane zuzu
Hahahahhaaaaa eti wewe ni naibu?
Kipimo cha uzi wa maana ni ipi?kwani huna taarifa ya kikundi cha uasi dhidi ya Mbowe?
 
Kinachonitafakarisha hiki ninacho sikiasikia
hapa kuwa we ni naibu
kama ni kweli tumefikia kuwa na mawaziri wajinga kiasi hiki
mzimu wa Kambarage na borito ukagone
kuighenja Tanzania mbai
 
Back
Top Bottom