Nasikitishwa na hili!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nasikitishwa na hili!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkeshahoi, Aug 4, 2010.

 1. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kuna hali naiona miaka ya karibu na na siipendi kwakweli.

  - wengi wa wahitimu wa elimu ya juu hawajui hata kuandika wasifu(CV) wao, achilia mbali kudanganya wasifu wao.
  - Wakufunzi nao wamegeuka wajasiriamali na hawana ari tena ya kutengeneza vizazi vya wasomi walioelimika bali waliohitimu..
  -Waajiri wengi, hasa wa kizalendo wanaajir kwa makaratasi... hwachukui juhudi ya ziada kumchunguza msailiwa, wanaishia kusoma CV na kuuliza maswali walioandikiwa.
  - Wanafunzi wengi wa elimu ya juu wamekuwa wazembe, hata undergraduate thesis/projects zao wanafanyiwa ... utadhani wale wazee wa ma-ofisini amabao hulipa watu hela ili wawafanyie kazi zao..!!
  - na mengine mengi tu, kifupi, USANII MWINGI SANA siku hizi .

  Athari zake kubwa ni kukosa ajira zenye ushindani hasa katika mashirka ya kimataifa na kuboronga kazi hiko vibaruani.

  TUJIREKEBISHENI.... MHiTIMU WA DIPLOMA/DIGRIII HALAFU BADO MBUMBUMBU NA MZEMBE.... NI AIBU....!!!!

  nawakilisha:A S angry::A S angry:
   
 2. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Mkuu umenena kweli

  Hii hali ni aibu kweli, na inasikitisha saana, vyuo vingi vitabu hawana walimu ndo hakuna kabisa unakuta mwalimu mwajiriwa wa UDSM ana vipindi Iringa, Dodoma, Arusha etc ukumbuke na hapo darasa anatakiwa afundishe, Muda wa kujiandaa apate wapi???matokea yake ndo tunapata graduates ambao hawaajiriki kabisa, Na kwa hili hatutaweza hata kidogo kuwashinda Wa KE na Waganda kwani vyuo vyao havina matatizo kama vyetu.

  Tukumbuke na swala la Lugha ni changamoto kubwa kweli inayowakabili wahitimu wetu, Ule muda muafaka wakenya waliokuwa wanasubiri ndo umefika kwani kwenye soko la ajira wanauzika
   
 3. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Uko sahihi lakini sioni sababu ya uzembe wa wanafunzai na kuwa na graduates wachovu...
  -utandawazi umeleta fursa kibao za kupata maarifa, has kuptia mitandaoni ktk search engines, electronic library and journals, discussion forums na mengine kibao.
  - vyuo vingi (ikiwemo UDSM) wanaendesha elimu kwa njia ya mtandao... IFM wana video conferences technology, Ofisi kibao zatumia teleconference systems.

  Nijuavyo mimi, elimu ya juu si kulishwa kaa mtoto wa njiwa. Mwanafunzi ana hatimaye muhitimu wajibu jifunze kuongeza maarifa ya ziada kivyavyako. Nyakati hizi usishangae kuona mwanafunzi anajisomea na anapata maaarifa kuliko ata profesa wanaokumbatia makaratasi ya zamani.

  TUKUBALI... UZEMBE UPO.... TUJIREKEBISHE!!:nono:
   
 4. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #4
  Aug 4, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa kama wazazi ndo wanshiriki kununua paper kwa watoto wao ili waonekane wakali mwategemea nini? It begins with you.
   
Loading...