Abdul Mganyizi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2019
- 1,044
- 1,996
Nianze kwa kusalimia ndugu zangu wana JF itifaki imezingatiwa. Watanzania wote wanamshukuru Mh Rais kwa elimu bure kwa kuwa ameruhusu watanzania wengi kufika shule wale waliokuwa wanashindwa.
Lakini hii elimu bure inayotolewa ndio mada yangu yakujadili leo. Mimi ni Mwalimu wa shule ya msingi mkoa fulani na wilaya fulani jina kapuni. Wakati Mh mwenye nchi anaingia madarakani niliomba kwenda chuo kikuu.
Sasa nilivyorudi nilishangaa sana kuona mambo yamebadilika sana. Walimu wenzangu wakaniambia kuwa tuliambiwa hatakiwi mwanafunzi yoyote darasa la saba kufeli. Sasa mimi nikauliza sasa itawezekanaje maana Mwalimu kazi yako kufundisha tu ila mtihani anafanya mwanafunzi.
Nilichoelezwa kuwa mtihani anafanya Mwalimu na sasa hivi shule zinashindanisha walimu, ukiona shule imefelisha jua walimu ndio wamefeli. Sasa mwaka jana ndio nikashuhudia vizuri kwenye semina Afisa Elimu anavyotoa miongozo kwa wasimamizi kuhusu huko wanakoenda kusimamia wahakikishe wanashirikiana na wakuu matokeo kuwa mazuri.
Leo hii ukishapangiwa kusimamia unakuta walimu washajipanga muda mrefu, wanafunzi hawafanyi chachote wanasubiria waletewe mtihani mzima.
Inasikitisha kila nikiitazama Tanzania ijayo. Sasa baada ya matokeo ya mwaka jana Mkurugenzi anawaita maafisa elimu kata na Afisa elimu na kusema "nawapongeza sana sana, mbinu iendelee kuwa hiyo hiyo ila mwakani ufaulu uwe asilimia mia sio tena 93".
Sasa nikitazama wanafunzi ambao hata jina lao kuliandika ilkuwa mtihani lakini wamefaulu tena kwa alama nzuri nasikitika sana. Sasa afisa taaluma ni rafiki yangu nikawa nateta nae, namuuliza hii ni sahihi kweli hata kwa Mungu tunaenda kujibu nini, anasema hii ni sahihi kwa kuwa mwenye nchi ndicho anachokitaka.
Yeye anataka kusikia wamefaulu, wamefauluje hilo halimuhusu. Kila mmoja abebe mzigo wake naye miaka yake kumi ikiisha ataondoka ndicho anachokitaka Rais wa nchi.
Poleni watanzania pamoja na wazazi kwa ujumla sisi walimu tunachokifanya kwa wanao kwa kuwafanyia mtihani wa mwisho wakati wamekaa shuleni miaka saba wakisubiri kufanya mtihani wa mwisho. Mungu ibariki Afrika na Tanzania kwa ujumla.
Sent using Jamii Forums mobile app